Mume wangu alishinda tuzo ya JF, karudi nyumbani na tuchips hatufiki hata kumi, na kamshikaki kamoja

Jemima Mrembo

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2021
Posts
2,864
Reaction score
8,328
Yaani tangu alipoondoka saa 12 asubuhi kufuata zawadi yake ndio anaingia ndani muda huu, kalewa pomoni, anasema huko waliitiwa kula na kunywa.

Lakini jirani yetu hapa naye alishinda hizo tuzo, naona karudi na mazaga kibao, na pilau naisikia ikinukia.

Kweli mambo ya JF ni makubwa mno, hata tu kwa kiumbe huyu kurudi akiwa tilàlila inaonekana kweli mmewajaza mambo mambo mazuri. Shukrani na pongezi kwenu, tukiachana na huyu kiumbe wangu mtata.
 
Yaani tangu alipoondoka saa 12 asubuhi kufuata zawadi yake ndio anaingia ndani muda huu, kalewa pomoni, anasema huko waliitiwa kula na kunywa...
Asante timu nzima ya JamiiForums. Asante Maxence Melo, zawadi hakika ni maridadi kweli kweli, wengine wamerudi nyumbani wakitembea dog style. Very superb.

Mshana Jr, naomba upitie huu uzi
 
Asante timu nzima ya JamiiForums. Asante Maxence Melo, zawadi hakika ni maridadi kweli kweli, wengine wamerudi nyumbani wakitembea dog style. Very superb.

Mshana Jr, naomba upitie huu uzi
Nipo hapa bro .. Ukapotelea wapi? Niliona mkono tuu [emoji23]

Usiposhukuru kwa kidogo basi hata ukipewa kikubwa huwezi kusema asante!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…