Mume wangu alishinda tuzo ya JF, karudi nyumbani na tuchips hatufiki hata kumi, na kamshikaki kamoja

Mume wangu alishinda tuzo ya JF, karudi nyumbani na tuchips hatufiki hata kumi, na kamshikaki kamoja

Yaani tangu alipoondoka saa 12 asubuhi kufuata zawadi yake ndio anaingia ndani muda huu, kalewa pomoni, anasema huko waliitiwa kula na kunywa.

Lakini jirani yetu hapa naye alishinda hizo tuzo, naona karudi na mazaga kibao, na pilau naisikia ikinukia.

Kweli mambo ya JF ni makubwa mno, hata tu kwa kiumbe huyu kurudi akiwa tilàlila inaonekana kweli mmewajaza mambo mambo mazuri. Shukrani na pongezi kwenu, tukiachana na huyu kiumbe wangu mtata.
😀😀😀😀 pambana na kiumbe wako na hongera kwa kukitunza
 
Back
Top Bottom