Mume wangu ananipa Kila kitu kasoro kitu kimoja tu. Nishaurini nataka kuvunja hii ndoa

Daah Pole Mdogo wangu.....wewe ni George Aloyce ni Mwanamke?

Ndio maisha unavyoona Kassim Majaliwa akiwa Waziri Mkuu Usidhani alianzia juu... Alikuwa Mwl hulo huko Vijijini.

DCI Insp Kingai aliishi huko huko Maporini ndio akawa anapanda mdogo mdogo sasa yuko Dar.

Vumilia huko ndio kuna maisha.

Vyakula vya asili, chakula bei nafuu, hata Kupanga nyumba Bei poa sana.
Kwa mtumishi ana save pesa za kutosha
 
Yaani kutoka Kata ilipo kwenda Mjini ni safari ya Siku nzima?

Kweli Tanzania ni kubwa sana
 
Jamani huyu dada mueleweni kuna vijiji ukienda kama umezoea kukaaa mjini unaweza changanyikiwa akili......yaaani ni chombingo kweli kweli hadi unaogopa
 
Pole sana. Hayo mazingira siyo mabaya kabisa. Vumilia na mpende mume wako. Kikubwa tafuta kazi, kazi zipo nyingi utapata. Mtie moyo mumeo. Leo unamuona yupo huko iko siku atakuwa Dodoma makao makuu aya sehemu ya mjini yenye shughuli nyingi. Polisi wengi huanzia vijijini ila mwisho wanakuwa mjini. Vumilia mdada na mpende mumeo. Nimekuonea huruma kwa sababu unachotaka kufanya ni kitu kibaya mno kitakusumbua sana badaye maana maisha ya leo siyo ya kesho
 
Asante sana Kwa ushauri
 
Hali ni mbaya
 
Ni swala la mentality tu ila kwakuwa mwanamke mpumbavu huvunja ndoa Yake kwa mikono Yake mwenyewe na ww vunja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…