Mume wangu ananipa Kila kitu kasoro kitu kimoja tu. Nishaurini nataka kuvunja hii ndoa

Kijijini siwezi
 
Kijijini kama mjini saizi ,wewe hutaki kuingia ndani unataka uende Nje mjini kufanya nini? Danga na hao hao matajiri wa Kijijini
 
George kama George....
 
Uliolewa ukiwa na akili za kitoto, bado hazijakutoka. Kaa na mme wako, huko mjini unapataka kwa nini. Kaa na mume wako Biblia inasema utabarikiwa mjini na vijijini maana yake Mungu alitarajia watu waishi na vijijini.

Mwanamke mpumbavu huvinja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe.
 
wahenga walisema...
"mkataa pema pabaya panamwita"

ndugu mpendwa sana, mrembo muhitimu, maisha ni popote na mchagua jembe si mkulima 🐒

Binafsi sijaona sababu hata moja ya wewe kutofurahia ndoa yako, naiona tamaa tu ambayo nadhani mwisho wake sioni wema ndani yake bali majuto na maumivu ya kujilaumu sana baadae 🐒

nategemea kwa msomi wa chuo kama wewe kubadili changamoto kua ni fursa ya kuibua ubunifu ambayo inaweza kubadili standard ya maisha na kipato chenu apo kijijini, na kwakweli kuchochea mabadiliko ya maisha ya watu kijini apo 🐒

naona fursa ya kilimo, ufugaji lakini pia naona ujenzi wa hekalu lenu la kuishi kifahari sana kwa Utulivu, huku mjini mkileta mazao tu kwa nyakati tofauti tofauti, huku pia mkiangalia fursa za kuwekeza pia mjini 🐒

kumbuka tamaa mbele mauti nyuma, maisha yanaenda resi ajabu
kama hakupendi nawe humtaki basi atakubali ukapange na kuishi mjini yeye abaki kijijini na itakua ndio imeisha hiyo, haiwezi kua salama tena...
 
Kuna haja tupeleke ombi maalumu Kwa Melo kwamba wachangiaji wenye jinsia mbili mbili wapigwe marufuku humu

Yaani leo ana jinsia ya kiume, kesho kutwa anakuja na jinsia ya kike

Ni kutuchanganya wasomaji sasa 😜
 
Wewe ni pumbavu kweli fanya application za kazi kwenye mitandao uko uko uliko sio unakalisha matako tu unakaa kulaumu...angalia planB andazi kabisa wewe
 
Taja hicho kijiji tujue ni Songea ipi!? Maana Songea ilishafunguka mda sanaa...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…