Mume wangu ananipa laki 5 kila mwezi mama anadai hazitoshi nirudiane na x wangu

Mume wangu ananipa Laki 5 k

Kabla ya kuingia kwenye ndoa, kulikuwa na mwanaume niliyekuwa naye—ni mume wa mtu. Yeye ndiye aliyekuwa analipia ada yangu ya chuo, alikuwa ananipa pesa pamoja na kuhudumia wadogo zangu. Yaani, hata ada za wadogo zangu alikuwa akilipa. Nyumbani kila mtu alifahamu kuhusu msaada wake, kasoro Baba.

Kipindi hicho nilikuwa pia na huyu mume wangu, ambaye wakati huo alikuwa mchumba wangu. Alikuwa ananihudumia kwa mambo madogo madogo, lakini sikuwa nikiomba pesa nyingi kutoka kwake kwa sababu nilikuwa na mbaba wangu. Baada ya kumaliza chuo, sikuhangaika kutafuta kazi. Nilijaribu kufungua biashara, lakini haikufanikiwa, hivyo nikaamua kuolewa.

Kila kitu kilikuwa vizuri, lakini kipindi nikiwa kwenye ndoa niliendelea kuwa na yule mbaba wangu. Alikuwa bado ananihudumia. Shida ilianza baada ya mume wangu kuhamishwa kikazi, tuko mkoani sasa, na siwezi kuonana na yule baba kwa sababu pia nina ujauzito.

Changamoto ni kwamba kipato cha mume wangu ni kidogo sana, mshahara wake ni kama milioni 3 hivi. Anaweza kunihudumia, lakini hawezi kuhudumia ndugu zangu. Siwezi kumuomba pesa ya kumhudumia Mama yangu au kulipia ada za wadogo zangu. Kwa mwezi, mume wangu hunipa laki 5 kwa ajili ya matumizi yangu na kusaidia kwetu, lakini haitoshi hata kwa Mama yangu tu.

Niliwazoesha msaada wa pesa kiasi kwamba kila kitu wananiomba mimi. Nikiwaambia kuwa mambo yamebadilika, hasa Mama, hataki kunielewa. Ananiambia kuwa nilikurupuka kuolewa, na kama mume wangu hawezi kusaidia familia yangu basi niachane naye.

Mama yangu alimtafuta yule baba kuongea naye kuhusu kurudiana na mimi. Baba alisema kama bado nampenda, basi nirudi Dar es Salaam, na yeye atalea mimba yangu na kuendelea kunihudumia. Hata hivyo, alisema hawezi kunipa pesa wakati nikiwa mkoani!

Sina shida yoyote kwenye ndoa yangu. Mume wangu ananijali kwa kila kitu. Hivi sasa tunajenga, na sijachangia chochote, lakini kwa wema wake ameandika majina yetu wote wawili kwenye mali hiyo. Chakula na kila kitu kinapatikana, lakini sina amani kabisa.

Mama yangu kama ameninunia—wiki ya pili sasa hapokei simu zangu na anatuma tu meseji akisema, "Umekamua kuwa mbinafsi kujichagua wewe huku ndugu zako wakiteseka. Ikaa huko huko, lakini jua kuwa wewe si mtoto wangu!" Naomba ushauri, Kaka. Nafanyaje? Naona hii ndoa itanishinda, labda nilikimbilia kuolewa!
Achana na mama yako.
Endelea na mumeo, laana asiyo na sababu haimpati mtu. Asikufanye wewe ndio kitega uchumi chake.

Umekuwa sasa achana na mambo ya zamani, jenga familia yako.
Kumbuka majuto ni mjukuu.
 
Mshauri mama yako aanze kugongwa na huyo mbaba, ili akusaidie majukumu kwa sababu uko mbali, ili muweze kuvuna pesa kote ndio itakua faida kwenu, na wala hakuna tatizo mama yako akianza kumpa tunda huyo mbaba maana ndio biashara yenu ya kuuza uchi itakua nzuri na yenye faida
 
Mume wangu ananipa Laki 5 k

Kabla ya kuingia kwenye ndoa, kulikuwa na mwanaume niliyekuwa naye—ni mume wa mtu. Yeye ndiye aliyekuwa analipia ada yangu ya chuo, alikuwa ananipa pesa pamoja na kuhudumia wadogo zangu. Yaani, hata ada za wadogo zangu alikuwa akilipa. Nyumbani kila mtu alifahamu kuhusu msaada wake, kasoro Baba.

Kipindi hicho nilikuwa pia na huyu mume wangu, ambaye wakati huo alikuwa mchumba wangu. Alikuwa ananihudumia kwa mambo madogo madogo, lakini sikuwa nikiomba pesa nyingi kutoka kwake kwa sababu nilikuwa na mbaba wangu. Baada ya kumaliza chuo, sikuhangaika kutafuta kazi. Nilijaribu kufungua biashara, lakini haikufanikiwa, hivyo nikaamua kuolewa.

Kila kitu kilikuwa vizuri, lakini kipindi nikiwa kwenye ndoa niliendelea kuwa na yule mbaba wangu. Alikuwa bado ananihudumia. Shida ilianza baada ya mume wangu kuhamishwa kikazi, tuko mkoani sasa, na siwezi kuonana na yule baba kwa sababu pia nina ujauzito.

Changamoto ni kwamba kipato cha mume wangu ni kidogo sana, mshahara wake ni kama milioni 3 hivi. Anaweza kunihudumia, lakini hawezi kuhudumia ndugu zangu. Siwezi kumuomba pesa ya kumhudumia Mama yangu au kulipia ada za wadogo zangu. Kwa mwezi, mume wangu hunipa laki 5 kwa ajili ya matumizi yangu na kusaidia kwetu, lakini haitoshi hata kwa Mama yangu tu.

Niliwazoesha msaada wa pesa kiasi kwamba kila kitu wananiomba mimi. Nikiwaambia kuwa mambo yamebadilika, hasa Mama, hataki kunielewa. Ananiambia kuwa nilikurupuka kuolewa, na kama mume wangu hawezi kusaidia familia yangu basi niachane naye.

Mama yangu alimtafuta yule baba kuongea naye kuhusu kurudiana na mimi. Baba alisema kama bado nampenda, basi nirudi Dar es Salaam, na yeye atalea mimba yangu na kuendelea kunihudumia. Hata hivyo, alisema hawezi kunipa pesa wakati nikiwa mkoani!

Sina shida yoyote kwenye ndoa yangu. Mume wangu ananijali kwa kila kitu. Hivi sasa tunajenga, na sijachangia chochote, lakini kwa wema wake ameandika majina yetu wote wawili kwenye mali hiyo. Chakula na kila kitu kinapatikana, lakini sina amani kabisa.

Mama yangu kama ameninunia—wiki ya pili sasa hapokei simu zangu na anatuma tu meseji akisema, "Umekamua kuwa mbinafsi kujichagua wewe huku ndugu zako wakiteseka. Ikaa huko huko, lakini jua kuwa wewe si mtoto wangu!" Naomba ushauri, Kaka. Nafanyaje? Naona hii ndoa itanishinda, labda nilikimbilia kuolewa!
Ni chai ila kama inatokea hivi rahisi tu. Unamwambia huyo Mamayo akatembee na Ex wako yeye apate pesa nyingi.
 
Kama ana namba za huyo mbaba mwambie amalizane nae tu atatue shida zake za za wadogo zako,.

Ila kuna wazazi wengine wachachi sana🤒
 
Mwambie Mama yako amfuate huyo Baba awe mpenzi wake au mchepuko wake, huyo mama yako sio kabisa, ana tamaa sana huyo, mwambie huyo baba awe anamtia atampa fedha, ila nyie binadamu nyie
 
Mkuu,

Stories za JF kama hizi wewe chukulia kama zoezi la kufikiri kidhahania.

Mimi hupenda sana kuhoji na kuhakiki habari kabla ya kuzijadili.

Lakini, tukija kwenye mambo personal, uhakiki huo ni mgumu, kwa sababu by nature issue imekuwa reported kuwa ni personal, sasa kama imetokea kweli tunaihakiki vipi?

Na hata tukipenda sana kuhakiki mambo, kumkatalia mtu kuwa hiki halijatokea nako ni kugumu pia, na ni vibaya sana kumwambia mtu kitu hakijamtikea ikiwa kimemtikea kweli.

Kwa hiyo, chukulia hii habari kama zoezi la kufanya fikra za kidhahania kuwa hata kama halijatokea hivi, kuna wimbi kubwa la wazazi kuwauza binti zao to the highest bidder siku hizi.

Na hapa ndipo hata mtu akitaka kuwapinga team kataa ndoa, huwezi kusema kuwa hoja zao hazina mashiko kabisa.

Nakupa sehemu mbili sababu zipo nyingi za true stories hizo za watu binafsi

ukayajue usiyoyafahamu ya dunia

Insta
Iddi
Makengo
Kibongo bongo hapa

Na
Tn_
World
Waki westi
 
Kama ana namba za huyo mbaba mwambie amalizane nae tu atatue shida zake za za wadogo zako,.

Ila kuna wazazi wengine wachachi sana🤒
Kwa ufupi mama yake ni hamnazo, inaonekana anamdharau Mume WA mwanae wakati mambo ya uchumi hubadilika Mume WA huyo dada anaweza kupata uchumi mkubwa zaidi ina maana mama anaweza kumpa tunda mkwe wake
 
Huyo mbaba mwenyewe anasema kama bado ananipenda.. Eeeh sio yeye anampenda

Hapo lazima awapige la uso kwa Tamaa zao..

Na alimsomesha akasepa 🤣🤣🤣

Binti mjinga.. Though Mama yake alivyo hata kurogwagwa atamfanyia hivyo
 
Mume wangu ananipa Laki 5 k

Kabla ya kuingia kwenye ndoa, kulikuwa na mwanaume niliyekuwa naye—ni mume wa mtu. Yeye ndiye aliyekuwa analipia ada yangu ya chuo, alikuwa ananipa pesa pamoja na kuhudumia wadogo zangu. Yaani, hata ada za wadogo zangu alikuwa akilipa. Nyumbani kila mtu alifahamu kuhusu msaada wake, kasoro Baba.

Kipindi hicho nilikuwa pia na huyu mume wangu, ambaye wakati huo alikuwa mchumba wangu. Alikuwa ananihudumia kwa mambo madogo madogo, lakini sikuwa nikiomba pesa nyingi kutoka kwake kwa sababu nilikuwa na mbaba wangu. Baada ya kumaliza chuo, sikuhangaika kutafuta kazi. Nilijaribu kufungua biashara, lakini haikufanikiwa, hivyo nikaamua kuolewa.

Kila kitu kilikuwa vizuri, lakini kipindi nikiwa kwenye ndoa niliendelea kuwa na yule mbaba wangu. Alikuwa bado ananihudumia. Shida ilianza baada ya mume wangu kuhamishwa kikazi, tuko mkoani sasa, na siwezi kuonana na yule baba kwa sababu pia nina ujauzito.

Changamoto ni kwamba kipato cha mume wangu ni kidogo sana, mshahara wake ni kama milioni 3 hivi. Anaweza kunihudumia, lakini hawezi kuhudumia ndugu zangu. Siwezi kumuomba pesa ya kumhudumia Mama yangu au kulipia ada za wadogo zangu. Kwa mwezi, mume wangu hunipa laki 5 kwa ajili ya matumizi yangu na kusaidia kwetu, lakini haitoshi hata kwa Mama yangu tu.

Niliwazoesha msaada wa pesa kiasi kwamba kila kitu wananiomba mimi. Nikiwaambia kuwa mambo yamebadilika, hasa Mama, hataki kunielewa. Ananiambia kuwa nilikurupuka kuolewa, na kama mume wangu hawezi kusaidia familia yangu basi niachane naye.

Mama yangu alimtafuta yule baba kuongea naye kuhusu kurudiana na mimi. Baba alisema kama bado nampenda, basi nirudi Dar es Salaam, na yeye atalea mimba yangu na kuendelea kunihudumia. Hata hivyo, alisema hawezi kunipa pesa wakati nikiwa mkoani!

Sina shida yoyote kwenye ndoa yangu. Mume wangu ananijali kwa kila kitu. Hivi sasa tunajenga, na sijachangia chochote, lakini kwa wema wake ameandika majina yetu wote wawili kwenye mali hiyo. Chakula na kila kitu kinapatikana, lakini sina amani kabisa.

Mama yangu kama ameninunia—wiki ya pili sasa hapokei simu zangu na anatuma tu meseji akisema, "Umekamua kuwa mbinafsi kujichagua wewe huku ndugu zako wakiteseka. Ikaa huko huko, lakini jua kuwa wewe si mtoto wangu!" Naomba ushauri, Kaka. Nafanyaje? Naona hii ndoa itanishinda, labda nilikimbilia kuolewa!
Iyo familia ina laana ya kurithi...inahitaji ukombozi
 
Ungemshauri mama yako amchukue huyo mbaba.. ili faida yote ale yeye.
 
Kwa ufupi mama yake ni hamnazo, inaonekana anamdharau Mume WA mwanae wakati mambo ya uchumi hubadilika Mume WA huyo dada anaweza kupata uchumi mkubwa zaidi ina maana mama anaweza kumpa tunda mkwe wake
Na hapo utashangaa hadi anaenda kwa mganga amroge mwanae arudi kwa Mbaba
 
Mume wangu ananipa Laki 5 k

Kabla ya kuingia kwenye ndoa, kulikuwa na mwanaume niliyekuwa naye—ni mume wa mtu. Yeye ndiye aliyekuwa analipia ada yangu ya chuo, alikuwa ananipa pesa pamoja na kuhudumia wadogo zangu. Yaani, hata ada za wadogo zangu alikuwa akilipa. Nyumbani kila mtu alifahamu kuhusu msaada wake, kasoro Baba.

Kipindi hicho nilikuwa pia na huyu mume wangu, ambaye wakati huo alikuwa mchumba wangu. Alikuwa ananihudumia kwa mambo madogo madogo, lakini sikuwa nikiomba pesa nyingi kutoka kwake kwa sababu nilikuwa na mbaba wangu. Baada ya kumaliza chuo, sikuhangaika kutafuta kazi. Nilijaribu kufungua biashara, lakini haikufanikiwa, hivyo nikaamua kuolewa.

Kila kitu kilikuwa vizuri, lakini kipindi nikiwa kwenye ndoa niliendelea kuwa na yule mbaba wangu. Alikuwa bado ananihudumia. Shida ilianza baada ya mume wangu kuhamishwa kikazi, tuko mkoani sasa, na siwezi kuonana na yule baba kwa sababu pia nina ujauzito.

Changamoto ni kwamba kipato cha mume wangu ni kidogo sana, mshahara wake ni kama milioni 3 hivi. Anaweza kunihudumia, lakini hawezi kuhudumia ndugu zangu. Siwezi kumuomba pesa ya kumhudumia Mama yangu au kulipia ada za wadogo zangu. Kwa mwezi, mume wangu hunipa laki 5 kwa ajili ya matumizi yangu na kusaidia kwetu, lakini haitoshi hata kwa Mama yangu tu.

Niliwazoesha msaada wa pesa kiasi kwamba kila kitu wananiomba mimi. Nikiwaambia kuwa mambo yamebadilika, hasa Mama, hataki kunielewa. Ananiambia kuwa nilikurupuka kuolewa, na kama mume wangu hawezi kusaidia familia yangu basi niachane naye.

Mama yangu alimtafuta yule baba kuongea naye kuhusu kurudiana na mimi. Baba alisema kama bado nampenda, basi nirudi Dar es Salaam, na yeye atalea mimba yangu na kuendelea kunihudumia. Hata hivyo, alisema hawezi kunipa pesa wakati nikiwa mkoani!

Sina shida yoyote kwenye ndoa yangu. Mume wangu ananijali kwa kila kitu. Hivi sasa tunajenga, na sijachangia chochote, lakini kwa wema wake ameandika majina yetu wote wawili kwenye mali hiyo. Chakula na kila kitu kinapatikana, lakini sina amani kabisa.

Mama yangu kama ameninunia—wiki ya pili sasa hapokei simu zangu na anatuma tu meseji akisema, "Umekamua kuwa mbinafsi kujichagua wewe huku ndugu zako wakiteseka. Ikaa huko huko, lakini jua kuwa wewe si mtoto wangu!" Naomba ushauri, Kaka. Nafanyaje? Naona hii ndoa itanishinda, labda nilikimbilia kuolewa!
Umesomea chuo Cha ukahaba na ipo siku ukahaba wako wataulisi hao wadogo zako na kama wanaume wanaweza kuuza ushindi wao achana na upumbavu wanasemaj MJINGA NI MJINGATU HATA UKIMFICHA KWENYE CHUPA ATAWASHWA NA KUNYOSHA KIDOLE JUU shenzi kabisa ww
 
Sasa si afadhari ungekubali kuwa mke wa pili kwa huyo x wako?
Wanaume tunaooa nyakati hizi tuna kazi kweli kweli! Unakuja kuoa used kabisa! Eti na wewe uko kwenye majukumu yako unajua umeacha mke nyumbani kumbe ni x wa mtu!
 
fanya hivi ,mwombe mumeo mtaji wa Milion 6 ,mwelezi kina kirefu anasema

Ukinipa Milion 6 kwa mpigo mwezi wa 5 na 6 ,niende gairo au mbalali ...nikanunua mpunga niweke store hukohuko na nitapata mkataba.

Kwa kuwa gunia 1,huuzwa 70 k kwa Milion 6 naweza pata gunia 85 hadi 89au 90 niliweka store mwezi kama huu unauza hadi 160 k hivyo nitakuwa nimezalisha maradufu

Ukifanya hivyo mwaka mmoja tu ,utaanza kuwahudumia nduguzako

Pia ,mama Ako mwambie aache mbwembwe ....atakuwa liwa mwenyewe
 
Back
Top Bottom