Tukiandika tunaonekana walokole. Anyways kama wewe ni Mkristo..Omba. Yani simama kwenye maombi na kumuamini Mungu kweli kweli. Ninachoona hapa unalengwa wewe kuondolewa kwenye nafasi.
Kuna maneno umeyaandika hapa tayari shetani kashakudaka. Katika Mith 6:2 neno linasema "umetegwa kwa maneno ya kinywa chako, umekamatwa kwa maneno ya kinywa chako." Shetani anachofanya kakungoja utype.."sometimes ndoa hizi bora uwe single..umeolewa kwa ajili ya heshima tu". Usifikiri ulichotype kimeenda bure. Maana si unaona bora uwe single ok fine, haujakiri anything positive rather comments za humu zinazidi kukuvuruga kihisia na kiufahamu.
Wewe tena....unazidi kuharibu kwa maneno yako mwenyewe. Mungu aliumba dunia kwa neno, neno lako lina uwezo mkubwa wa kujenga ama kuharibu. Ukijiita wewe ni masikini..kweli utakuwa..what do you speak over your life, marriage, children, in laws, relatives??...jifunze kuwa na positive affirmations.
Nakuambia hili kwa sabbu mm ni mhanga. Nilikuwaga naongea negative kila mara katika maisha yangu. Sikuwahi kusogea. Kila ukurasa ulikuwa umefungwa. Nilipoanza kukiri kushinda kila siku mambo yakaanza kubadilika moja baada ya jingine.
Ni muda wa kumconsult Mungu miss. Ni muda wa kwenda kuongea naye what is happening and the changes you want to see happen in your marriage. God is able..I know it for sure. Mume wako ni mdogo sana mbele ya baba yake aliye mbinguni. Kama hilo agano mlilifunga mbele za Mungu, uwe na uhakika ni Mungu huyohuyo anaeweza kuirestore hiyo ndoa. Lakin sasa usiende mbele zake huku unajihesabia haki. Nenda mbele zake huku unatubu kabisa kutoka moyoni. Maana neno linasema wote tumetenda dhambi hata kupungukiwa na utukufu.
Utukufu wa Mungu ukiondoka lazima furaha na amani viondoke. Mimi ni shuhuda wa hii statement. Ilinichukua mwaka kugundua hili. Ask God where did you go wrong? Maana mpaka shetani kuingia hapo kuna mlango ulifunguliwa..na wewe kama mlinzi wa familia hukusimama nafasi yako. Naweza kuandika mengi lakin for consultation zaid am available PM. Ila kama utaona naongea nonsense please usimind..potezea hii comment..achana nayo madam. All the best.