Mume wangu hapendi kula nyumbani

Mume wangu hapendi kula nyumbani

huyo asha zira kula chakula jitafakali ulikosea wapi,na anakuhis nini,maana sio kawaida .mtu anaweza kukuchapa kisaikolojia pasipo kutumia fimbo.hata kama anakula pengine lazma siku moja moja ale nyumbani.
 
Unajua kupika ? Inawezekana unamchemshia mchuzi , ilhali mwenzio keshakutana na madikodiko kwa mama k!
Mf binafsi wife anajua sana kupika na kaniteka kwa hilo , ila kuna siku nilikula chapati Tabata kiwango cha sgr , mara kadhaa nikikumbuka huwa nachochora kwenda huko kwa chai.
 
Tukiandika tunaonekana walokole. Anyways kama wewe ni Mkristo..Omba. Yani simama kwenye maombi na kumuamini Mungu kweli kweli. Ninachoona hapa unalengwa wewe kuondolewa kwenye nafasi.

Kuna maneno umeyaandika hapa tayari shetani kashakudaka. Katika Mith 6:2 neno linasema "umetegwa kwa maneno ya kinywa chako, umekamatwa kwa maneno ya kinywa chako." Shetani anachofanya kakungoja utype.."sometimes ndoa hizi bora uwe single..umeolewa kwa ajili ya heshima tu". Usifikiri ulichotype kimeenda bure. Maana si unaona bora uwe single ok fine, haujakiri anything positive rather comments za humu zinazidi kukuvuruga kihisia na kiufahamu.

Wewe tena....unazidi kuharibu kwa maneno yako mwenyewe. Mungu aliumba dunia kwa neno, neno lako lina uwezo mkubwa wa kujenga ama kuharibu. Ukijiita wewe ni masikini..kweli utakuwa..what do you speak over your life, marriage, children, in laws, relatives??...jifunze kuwa na positive affirmations.

Nakuambia hili kwa sabbu mm ni mhanga. Nilikuwaga naongea negative kila mara katika maisha yangu. Sikuwahi kusogea. Kila ukurasa ulikuwa umefungwa. Nilipoanza kukiri kushinda kila siku mambo yakaanza kubadilika moja baada ya jingine.

Ni muda wa kumconsult Mungu miss. Ni muda wa kwenda kuongea naye what is happening and the changes you want to see happen in your marriage. God is able..I know it for sure. Mume wako ni mdogo sana mbele ya baba yake aliye mbinguni. Kama hilo agano mlilifunga mbele za Mungu, uwe na uhakika ni Mungu huyohuyo anaeweza kuirestore hiyo ndoa. Lakin sasa usiende mbele zake huku unajihesabia haki. Nenda mbele zake huku unatubu kabisa kutoka moyoni. Maana neno linasema wote tumetenda dhambi hata kupungukiwa na utukufu.

Utukufu wa Mungu ukiondoka lazima furaha na amani viondoke. Mimi ni shuhuda wa hii statement. Ilinichukua mwaka kugundua hili. Ask God where did you go wrong? Maana mpaka shetani kuingia hapo kuna mlango ulifunguliwa..na wewe kama mlinzi wa familia hukusimama nafasi yako. Naweza kuandika mengi lakin for consultation zaid am available PM. Ila kama utaona naongea nonsense please usimind..potezea hii comment..achana nayo madam. All the best.
 
huyo asha zira kula chakula jitafakali ulikosea wapi,na anakuhis nini,maana sio kawaida .mtu anaweza kukuchapa kisaikolojia pasipo kutumia fimbo.hata kama anakula pengine lazma siku moja moja ale nyumbani.
Hapana kiukweli huyo.mumewe kama anapita Bar kunywa pombeee hili ni jambo la kawaidaa kabisaaa minyama choma na bia vinanenepesha sanaa...! Kingine walevii hawalii kabisaa vyakula vya kawaida vya nyumbani sijui walii.. ugali nyamaa mandizii ya kupikaa wao ni vya kurost rost ndo zao. So huyo jamaa kama sio mlevi bhasi kuna shida kingine mazoeaa labda usiku huwa halii au anaona ale kidogo ila apungue so mwanamke amuulize jamaa
 
At the end of the day anaejua sababu ya hayo ni mumeo mwenyewe kwahiyo mimi nakushauri ujaribu kuongea nae kwa upole umuulize kwanini ukipika huwa hali alafu umsikie majibu yake!
Hayo majibu yake ndo yatakayokusaidia kujua kuna nini especially kama hayatamake sense,
 
Habari zenu wapendwa?

Naombeni msaada Mume wangu amekuwa pasua kichwa hapendi kula nyumbani, najua kupika nampikia vyakula vizuri lakini akija anakula tu kidogo anaacha wakati mwingine hali kabisa ukimuliza hana sababu.

Mwanzo nilijua labda napika vibaya lakini siyo maana watu wengine wakila hata wageni wanakifurahia sana chakula mpaka wananisifia najua kupika Ila mme wangu ndo tatizo anaweza akala hata vijiko 5 akasema ameshiba.

Hii hali kwakweli inaniumiza sana akili na uzuri ana mwili nahisi labda atakuwa anakula uko nje akija anakuwa labda ameshiba maana ka jinsi anavyokula hapa ndani alitakiwa awe hana hata afya yani kwa kifupi ni Kama tu hali Ila anagusagusa Kuna wakati hadi nawaza sijui kalogwa.
Vip saivi anakupelekea Moto?
 
Miss Chuga story za ndoa yake zipo Sana hii ndoa aliifosi Sasa inamrudia...
Atulie tu itakaa sawa huko mbeleni
Imebidi nipitie nyuzi zake
Sina uhakika kama alifosi ndoa lakini ndoa yake ilikuwa inaonekana itakuwa chungu kabla hata haijafungwa

 
Hao wageni wanakula free meal lazima wakusifie tu hata kama kibaya. Chunguza ujue kama anakula nje ama la. Kwani huwa hamtoki OUT uone huko anakula vipi?

Kwenye sherehe mkienda ulaji wake upoje? Je wakati wa uchumba alikuwa anafurahia mapishi yako? Mbona kama vile humjui kabisa mumeo?
Hata kama mke hajui kupika vizuri, bado tu siyo sababu ya mume kutokula nyumbani. Mbona hili ni tatizo la kurekebishika?
 
Unajua kupika ? Inawezekana unamchemshia mchuzi , ilhali mwenzio keshakutana na madikodiko kwa mama k!
Mf binafsi wife anajua sana kupika na kaniteka kwa hilo , ila kuna siku nilikula chapati Tabata kiwango cha sgr , mara kadhaa nikikumbuka huwa nachochora kwenda huko kwa chai.
Kwani mwanamke kutojua kupika ndiyo licence ya mume kula nje? Ukiona mwanaume anafanya hivi basi ujue ni mshamba fulani. Dunia ya sasa wakati mwingine unakaa na mkeo jikoni mnapika wote. Yale mambo ya mume kutoingia jikoni yamepitwa na wakati.
 
Inawezekana hujui kupika ila hawezi kusema hujui kupika sababu itakuuma Kila siku unapoingia kupika jikoni.

Inawezekena unapika chakula unachokipenda wewe sio unachokipenda yeye,hii ni common sana kwa wake zetu,Mtu anakaa jikoni kupika pilau masaa 5 wakati mi nataka ugali samaki wamchuzi na glass ya mtindi na Wala sio hilo pilau lako..

Inawezekena unajaza mafuta mengi ukidhani huo ndo upishi wakati mumeo anataka kubalance mwili,wadada baadhi wanaamini mafuta lazima yaelee juu ya mboga ndo amepika vzr

Inawezekena ana hasira na wewe,mwanaume akikuchukia wewe anachukia Kila kitu chako ndo mana wengi wao hasira wakishindwa kusi control anatekeleza Hadi watoto..

Inawezekena kuna sehemu anakula ambapo Wana mapishi mazuri kukuzidi,hii inatokea maana mapishi yametofautiana

Bottom line km hapendi kula sio big deal km sex life yenu ipo vzr ila km na sex nayo inasuasua basi ujue kuna shida..Kama umpi sex halafu chakula ndo unapoteza masaa jikoni unajisumbua tu hizo nguvu peleka chumbani tu..
 
Back
Top Bottom