miss chuga
JF-Expert Member
- Dec 25, 2019
- 303
- 660
- Thread starter
- #21
Huyu hanywi pombe kabisa yani ananiumiza sana akili, kuna kipindi dada yake alikuja nikafanya makusudi nikamuomba anisaidie kupika nia yangu nimuone Kama akirudi atakula alichopika dada yake pia nacho hakula hapo ndo nilipozidi kuona kuwa Kuna tatizo mahali.Mumeo kama ni mnywaji wa pombe mpikie vyakula vya kilevi.
Cheza na vitu vya kukaanga.. kama ndizi za kukaanga;, viazi na nyama za kukaanga.
Pia mpikie michemsho chemsho kama ndizi za kuchemsha na masupu supu ya nyama nyama za kuchemsha .
Kutegemea mtu alietoka kunywa bia ale wali maharage kisa umeunga na nazi ni upumbavu.
Hata mpishi atoke mbinguni kuna vyakula mtu alietoka kunywa pombe hawezi kula
Sasahivi nimeshakuwa Kama chizi sijiamini tena kila anayekuja akila chakula changu namuuliza hivi ni kitamu wananiambia ndio na wanavyokula pia unaona kabisa wanakifurahia sasa huyu mme wangu simuelewi, sijui anafanya hivi kunikomoa