Mume wangu hapendi ndugu zangu

Wewe mleta mada usituamini wanaume nasisitiza usituamini kabisa.
Hapo dogo katongozwa katoa nje ndo ugomvi ulipo. Kutongoza sio lazima maneno hata matendo tu kama vile kushika titi na matako.
Mimi nimepitia huko ila tofauti ni kuwa nikitolewa nje sianzishi kisirani.Kwakuwa nakuwa mpole na sijali kama nimetolewa nje Kuna baadhi ya mashemeji hujileta tena na wanaliwa.
Ipo siku huyo dogo akiendelea kukaa kwako ataliwa na mumeo na itakuwa mwisho wa ugomvi.
 
Amemnyima tunda ndio maana ana hasira hizo zote. Jambo la msingi lina ndoa yako na umlinde mdogo ako pia. Hao hawatakuja kupatana ni mpaka kitokee kitu. Sio lazima uishi na mdogo ako kwa faida yake na faida ya ndoa yako.
 
umeolewa wewe unaleta na familia yako ndo maana na tunakulaga wote mnabaki kulaumu
 
Hoja yako ya kwanza sio poa.
Haifai umwambie ndg yako kuwa mmewe hapendi aishi pale...utasababisha ndg wote wamchukie
Tatizo tunapenda kuishi Kwa unafiki, je ni kweli hachukii ndugu zake?
 
Huyo mdogo wako anatakiwa ajitahidi kumkwepa huyo shemeji yake ili wasionane na anatakiwa ajitahidi Kuto kukaa sebuleni wakati shemeji yake yupo.
 
Wewe Tena!😁
Mhm nyie wanawake mnajileteaga majanga wenyewe. Sssa mdogo wako pisi kali alafu young lazima nitake kuonja...yaani naona mrembo anaenda kugegedwa na vijana wakati kidume nipo hapo na hela zangu naweza kukupa kile unachotaka. Tusitiane majaribuni
 
Mhm nyie wanawake mnajileteaga majanga wenyewe. Sssa mdogo wako pisi kali alafu young lazima nitake kuonja...yaani naona mrembo anaenda kugegedwa na vijana wakati kidume nipo hapo na hela zangu naweza kukupa kile unachotaka. Tusitiane majaribuni
Sio kila sketi lazima mvue jamani,wengine wawe ndugu zenu!
 
familia haijui haya yote na haina sababu ya kujua. Najaribu kuficha ila sasa malalamiko yamezidi ina maana ndugu zangu hawatakua wanakuja kunitembelea kwangu. Hata siku nikipata mtoto nani atanisaidia na uzazi sasa kama nikiwaondoa. Wanaume wanadhani ni rahisi kufukuza ndugu ila siku nikiumwa yeye ataweza kufanya yote bila msaada. Kuna incident ilitokea kwa ndugu yangu, mume aliwahi kufukuza ndugu wa mkewe na siku mkewe alifanyiwa operation wakamwambia dada yao tunaogopa kupigwa na shemeji tukija kwako. Yule dada aliuguzwa na watu baki
Familia yako inampendaje wakati yeye hawapendi?
 
Shida ni mila zetu. Mwanaume kuwapenda ndugu zako ni bonasi. Wewe kuwapenda ndugu zake ni wajibu. Wewe umeolewa yeye ameoa. Upo kwenye mji wake. So usawa sahau. Inatarajiwa iwahudumie ndugu zake na sio kinyume chake ingawa ingekuwa bora zaidi. So chagua moja. Kilinda ndoa ama familia. Katika hali yako huwezi kulinda yote mawili. Kuhusu mdogo wako naamini kuna countless alternatives. Kuhusu ndoa ikiisha ndo kwaheri. Jua vipaumbele vyako
 
Asante mkuu🤝
 
Huwezi kosa hostel ,ata kama zime jaa ela ndio Kila kitu,alafu usiogope et ukimuondoa dogo ataenda kuaribikiwa ,just tafuta hostel na Kila week end mwambie aje nyumban .
 
Kuna sehemu nimeona et "ni mzuri pisi kali .." unamaanisha huyo dogo ni pis kali au!!
 
Kwakweli nimepitia ushauri wa kila mmoja wenu. Na hakika nimejifunza kitu kikubwa na naamini kuna watu pia wamejifunza.

Kuna vitu nilisahau kuelezea kwenye post ya kwanza.

1. Katika watu wenye waume wanaojali kwakweli naweza kujiweka namba za juu, namshukuru Mungu kwa hili kwamba wapo wanaume wenye upendo na kujali hata kama wengine wamesema hanipendi, nimeamua niridhike na haya nnayoyaona huku. Hata mtu aje aseme anibadilishie ntang’aka. Shida niliyokua nayo ni hiyo tu na ushauri pekee nlioupata kwa wingi ni kwamba nimfukuze mdogo wangu nyumbani.

Nimegundua wanaposema ndoa sio lelemama nilikua najua ni ile mume kukupiga basi. Ila kumbe mda mwengine ndo kama hivyo changamoto za kifamilia unabaki dilemma kwasababu mume anakua na mahusiano mazuri na ndugu zake ila wewe wa kwako unatakiwa uwaweke mbali siku mkisambaratika yeye ana wa kumpokea wewe utaenda kulia na marafiki.

Nimeona wanaume wengi pia wameshauri kwamba mume ndo amenioa so natakiwa kuhudumia familia yake na sio yeye apende ya kwangu. Nikikua ntaelewa hii kauli maana kwa sasa ndoa bado changa.

Kuhusu kumtoa huyu mtoto, kwakuwa alishasema mwenyewe kuna mambo anayaweka sawa then atarudi nyumbani mmenishauri kuwa nnachotakiwa ni kuvumilia.

Sasa swali nililonalo, hii hali inaacha vidonda moyoni mwangu kama mwanadamu, nifanyeje ili niione ya kawaida maana mume hapa ni kwake bado hatujajenga kwenye nyumba yetu. Na sisi wadogo zangu wote ni watu waliosoma, huyu akimaliza chuo akipata kazi wala hana mpango wa kuendelea kukaa hapa nyumbani kwangu.

Siku nikihitaji msaada wa ndugu zangu ntaupata? Najua humu kuna watu washapitia kunyanyaswa na dada zao au kufukuzwa na mashemeji, uliiona hali ya kawaida? Ulimsamehe? Uliweka kinyongo?

Kuna mtu keshawahi kuvunja ndoa kwasababu ya undugu? Au kuna mtu keshawahi kuvunja undugu ili alinde ndoa? Mwishowe kulikuwaje? Huu ndo ushauri ambao sijaupata bado. Ni hayo tu.
 
Huwezi kosa hostel ,ata kama zime jaa ela ndio Kila kitu,alafu usiogope et ukimuondoa dogo ataenda kuaribikiwa ,just tafuta hostel na Kila week end mwambie aje nyumban .
Sasa hiyo weekend kuja nyumbani ndo balaa linapoanzia. Si bado atakuwa anashinda kwangu? Maana siku za wiki tu anarudi jioni kabisa hata hashindi hapa. Sasa weekend si ndo itakua kero maana na mume anakuwepo nyumbani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…