Haya ndio nionavyo Mimi
Mosi, uwezo wa huyo mdogo wako kupanga chumba upo Ila unajisikia vibaya kwanini akapange na Hali wewe upo na anaweza kuishi kwako
Jibu ni rahisi mumeo hamtaki hapo kwake,Busara ni huyo kuhama hapo na mweleze ukweli mdogo wako kuwa inaonekana uwepo wako hapo mumeo hapendi na hujui sababu,hii itakusaidia mdogo wako kujua kuwa sio mapenzi yako yeye kuhama Ila Kero zimezidi toka Kwa mumeo.
Pili, unapenda Sana mumeo aonekane ni mtu mzuri kwenu ndio maana unajitahidi kuficha upuuzi wake,Hilo ni Jambo zuri lakini wakati mwingine sio Sawa aonekane yeye ni Malaika,nahisi ndio maana unahisi mdogo wako alienda kupanga basi mumeo ataonekana sio mtu mzuri,Kwa mazingira hayo kuwa muwazi sema kweli kuwa mumeo hapendi uwepo wa mdogo wako pale.
Tatu, ambalo ndio kubwa na wanabodi wengi wamesema ni kuwa mumeo anataka kumla supu huyo mdogo wako,na hivyo mdogo wako amegoma kuliwa supu,hiyo ndio sababu kubwa Kwa sababu zifuatazo:
* Mumeo hamhudumii huyo binti Kwa nauli wala Karo ya chuo na mambo mengine,kwahiyo wala sio mzigo kwake hata kidogo useme labda Maisha magumu ndio maana hamtaki hapo
* Huyo binti Mda mwingi yupo chuoni sio kwamba anashinda hapo na kuwafanya msiwe huru na nyumba yenu .
* Kama unavyosema huyo binti ana Tabia njema hivyo naamini hajawahi kuvunja heshima ya nyumba yenu.
Kitu pekee ambacho kimebakia hapo ni kuliwa supu na huyo mumeo.
Raisi mstaafu aliwahi kutuambia akili za kuambiwa changanya na zako.