Mume wangu hapendi ndugu zangu

Dada najidai anamjua sana mume wake mara ooho sio muhuni yani anachekesha sana kiukweli MME WAKE ANAMTAKA MDOGO WAKE... NA HUENDA AMESHAKULA MARA MOJA SASA DOGO ANABANA. akiweza amuamishe hapo nyumbani.
 
Hili ni tatizo kwa kizazi hiki cha shetani, wao walisaidiwa waliishi kwa watu lakini wakipata awataki watu waishi kwao. Wengine ufikia mbali zaidi awataki ndugu zao wala wa upande wa pili. Yaani mtu ataki ndugu wa upande wa kike wala upande wa kiume.
 
Ka
Kasema uwezo wa hostel hana

Ndio aendelee hivyohivyo kuvumilia kwani atakaa hapo milele. Degree ni miaka 3-5 avumilie.

Hapo sio kwao, sio kwake.
Hivyo avumilie yote.

Huyu Dada asitake mdogo wake akae Kwa ku-relax kama yupo Nyumbani.
Kwanza hiyo sio nzuri Kwa Afya ya ndoa.
Ni rahisi kuibiwa Mume na mdogo MTU.
 

Ubinafsi ni roho ya kurithi
 
Hili ni tatizo kwa kizazi hiki cha shetani, wao walisaidiwa waliishi kwa watu lakini wakipata awataki watu waishi kwao. Wengine ufikia mbali zaidi awataki ndugu zao wala wa upande wa pili. Yaani mtu ataki ndugu wa upande wa kike wala upande wa kiume.

Huko Kwa watu walikoishi hawakupata changamoto?
Hizo ni changamoto za kawaida.

Kizazi cha sasa ndio kinataka kuishi Kwa Watu Kwa ku-relax bila ya kuwa na changamoto Jambo ambalo haliwezekaniki
 
Kama mda umebakia mchache amalize chuo bora mvumilie hivyo hivyo tu sometimes, mtu mbinafsi ni kumpuuza kwa kumkomoa. Ndoa ni pamoja na ndugu.
 
Hili ni tatizo kwa kizazi hiki cha shetani, wao walisaidiwa waliishi kwa watu lakini wakipata awataki watu waishi kwao. Wengine ufikia mbali zaidi awataki ndugu zao wala wa upande wa pili. Yaani mtu ataki ndugu wa upande wa kike wala upande wa kiume.
Na wengi unakuta walilelewa kwa ndugu hivyo hivyo. Ila wakioa hawawataki ndugu. What a selfish race!
 
Ukisema hanipendi nanyong’onyea maana ananijali yani kuna vitu ananifanyia naridhika so nikimuhukumu kwa hili ntakua nakosea. Roho ya kimaskini siwezi Kupinga ila naikemea tu kwa jina la Muumba. Na ntafanyeje sasa ndo mume wangu wa ndoa
Pole sana, Wenye roho ya kokoto wapo wengi sana na wabinafsi, yaani anampenda mke au Mme tu, ndugu zake wakija sawa lakini wa upande wa pili ananuna hiyo pia ni roho mbaya, hata mtu akikaa kwenye sofa anaona kama analiharibu, kuna mdada mtoto wa ndugu yake aliletewa pale Mama yake alipata matatizo mtoto wa miaka 3, mmewe hataki akae kwenye sofa, na kulalamika anamaliza chakula na alipelekwa kwa muda tu, huyo Baba ni wawapi, kuna familia moja wao kwa Dada yao wanajazana hata usafiri wanaendesha, ila yeye ndugu wa mkewe akija ananuna hawezi kukaa sebule kama karudi kazini hawezi msalimia anapitiliza chumbani na anataka kupelekewa chakula huko, ni tabia tu ya uchoyo na roho mbaya
 
Mimi ni mwanaume na nakupa ushauri kutokana na experince kubwa niliyo nayo kutokana na kuwa na shida kama yako. Yalinipata mimi na nimeshaona yakipata familia kadhaa. Mimi nilikuwa natuhumiwa tuhuma kama ulizoandika. Ni hivi: wanawake wengi wenye tuhuma kama zako, hupofushwa na undugu, wakajiona kuwa wanalofanya wao ni sahihi kabisa, pia wakaona wanalofanya ndugu zao ni sahihi kabisa, kumbe ukichukuwa mtu neutral anaona kabisa wana makosa.
 
Kanuni za kuishi kwa watu usirelax, watendee wema wafadhili wako wataona umuhimu wako watakuthamini ni nature. Laws of attraction. Amka kabla yao somba maji, piga deki, fagia Uwanjani, safisha mazingira, safisha magari, waandae watoto kwenda shule, fanya nao homework. Sio unaamka saa tatu unawahi gombea rimoti na watoto. Unarudi mda uutakao. Unapolelewa nawe lipia gharama kwa kutoa nguvu na mda wako.
 
Vipi kuhusu hao ndugu wengine wanaokuja hapo kusalimia na anawatosa? Mimi siamini kwamba binti kamkataa, hapo issue ni gubu la mwamba, hataki ndugu wa mke waishi hapo.
Huyo baba kweli ni gubu na huenda hiyo tabia kairidhi kwa wazazi sasa kuitoa ni kazi sana na tabia nikama ngozi ya mwili, halafu utakuta yeye anataka mkewe awafanyie mema ndugu zake ni ujinga na upumbafu kabisa halafu ukute eti msomi duu Mungu amsaidie huyo dada.
 
Wanaume wachache sana wenye hizo mambo za kuchukia ndugu wa ukweni tena mwanafunzi atleast angekua hana ramani yupoyupo tu, mi nadhani huyo shemeji yetu aliomba mchezo akanyimwa jaribu kufatilia kiundani.
 
Huyo mwanaume anashinda nyumbani mda wote hadi apate huo mda wa kuchukizwa na shemeji.
Au alimtaka akachomolewa so anasaka sababu. Tabia za kuchukia ndugu nilidhani ni wanawake pekee. Kumbe na wanaume nao wapo
 
Huyo mwanaume anashinda nyumbani mda wote hadi apate huo mda wa kuchukizwa na shemeji.
Au alimtaka akachomolewa so anasaka sababu. Tabia za kuchukia ndugu nilidhani ni wanawake pekee. Kumbe na wanaume nao wapo
Wanaume wapo wengi sana wenye roho ya hivyo wanawake huwa tunazuga kama mwanaume ana roho ya hivyo unafunika funika ili kuficha aibu
 
mumeo ana chuki binafsi kwa mdogo wako hawezi kufikia hatua ya kufuatilia hadi mashuka ya kulalia. Siku ukipata muda wa kukaa nae akiwa na furaha mwambie kama kiutani kuwa nimeota unatembea na mdogo wangu ili ajue kuna kitu unahisi kwake. Pia, wala usimrudishe dogo kaa na mumeo mweleze ukweli kama hataki ukae na mdogo wako akwambie badala ya kuleta visa nyumbani.
 
Pole sana mkuu. Bila shaka mdogo wako kashamaliza chuo.
 
Huyo mumeo nimpe hongera japo hii ni chai yaani mtu atoke chuo alipwe hivyo pia hongera umechangamsha genge
 
Wanawake Huwa mnakosea sana KULETA ndugu zenu Kwenye familia, huendq hata hukumashirikisha mumeo ujio wa mdogo wako, au kama ulimshirikisha basi hakuridhia Kwa moyo mweupe mdogo wako kuishi hapo. NDUGU wanachangia sana kuharibu familia, ndoa ikiwa changa inahitaji utulivu na mnapaswa kukaa peke yenu kabla ya KUANZA KULETA ndugu , Kuna muda mkiwa peke yenu mnaenjoy sana hata sebuleni MNAWEZA kunyanduana , bafuni nk ila wakishaanzn kujazana ndugu , watoto, housegirl ni privacy inaanza kupotea unakuta inakuwa ngumu hata kumhug mkeo mbele za watu ukitoka kazini na pia mapenzi mnaanza kuviziana hadi watoto walale au ndugu watoke sebuleni wengine ni wabishi unakuta wanakaa sebuleni hadi saa Saba USIKU kisa tamthilia !
Ushauri
Mume wako hana tatizo , tatizo ni wewe uliyeletq ndugu Yako hapo, na Kwa maelezo Yako unatamani ndugu zako wangehamia hata hapo kwako, mke ataacha wazazi wake na ataambatana na Mume wake na sio ndugu zake! Elewa mume wako anataka Nini na Nini hataki ,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…