Helw wana jf, tangu wiki mbili sasa nilikuwa nataka nirudi kuwashukuru kwa ushauri mlionipa kwenye thread yangu niliyoipa kichwa cha habari kama hiki hapo juu, kwa kweli napenda kutoa shukran kwanza kwa mwenyezi mungu kwa kutusaidia tatizo lile limeisha, najua ni mungu tu ndie aliyesaidia,jina la bwana lishukuriwe
Napenda kuwashukuru wale wote waliochangia thread yangu na kunipa ushauri mungu awabariki pia wale walionibeza mungu pia awazidishie walipopunguza pia shukrani za dhati ziwaendee wale walioenda mbele zaidi na kuguswa kwa namna moja au nyingine wakani pm na kunipa ushauri zaidi hawa si wengine ni Mu-sir, Fisherscom, Annony, jamal-tanga na kiraka nashukuru sana mungu awabariki sana ushauri wenu wote niliufanyia kazi kwa namna moja au nyingine.
Ilitokea tu amesafiri nje ya nchi aliporudi mambo yakawa poa na nilipomuuliza kafanya nini akaniambia hakuna alichofanya basi sijamuuliza mpaka leo. Nawashauri wote wenye tatizo kama langu, wasikate tamaa mungu yupo na anasaidia wote wenye kuelemewa na mizigo, mwisho kabisa nashukuru ile post ya michell ambayo watu wengi walicomment niifatilie pia na mimi niliipenda na kuifanyia kazi
Oooops at last am free now, nawapenda nyote, muendelee kuwa na upendo kwa wengine wote wenye matatizo, kwa kweli naipenda jf family, mungu ambariki mwanzilishi max na mods wote kwa kazi nzuri,kila siku inayoenda nazidi kufall in love nayo. ahsanteni.