1.
Mungu si sawa na mganga wa kienyeji, kama humwamini Mungu si rahisi kuziona rehema zake kwani mwenye haki wake huishi kwa imani.
2.
hiyo nyumba yako inaonekana si ushuhuda mzuri wa ndoa takatifu. nlivyoelewa mimi ni kuwa mumeo alikuwa wa kwanza kutoka nje ya ndoa, na wewe kwa kuendekeza tamaa zako hasa mumeo alipopoteza appetite na wewe nawe ukaanza kutoka nje ya ndoa, ulipoona bado nyumba haijakaa sawa ukaanza kjichua tena unasema ulifurahia hako kamchezo, mwisho unageukia JF kutafuta ushauri, na bado una mawazo ya mganga. this is a fatal syndrome in your home! you need a complete overhaul of yourself and your family. kumgeukia Mungu kama unavyogeukia panadol ukiumwa na kichwa siyo sawa. Mungu wapaswa kumwendea kwa imani na lazima maisha yako pia yawe maisha ya mtu mwenye imani kwa Mungu.
3.
hapao kwenye ndoa yako mumemkaribisha ibilisi sasa anawaendesha mchakamchaka. mwapaswa kumkana ibilisi na mambo yake yote. mkichukua hatua ya pamoja wewe na mumeo ni vizuri, ila mumeo akiwa mgumu, wewe mwenyewe chukua a leading role. vaa utu wema wa mke mwema na ingia kwenye maombi bla kuchoka Mungu atasikia kilio chako
ubarikiwe sana