Muna Love: Wakati naolewa na Peter nilikuwa na mimba ya Casto ya miezi miwili

Muna Love: Wakati naolewa na Peter nilikuwa na mimba ya Casto ya miezi miwili

idawa

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2012
Posts
25,284
Reaction score
38,364
Muigiza Maarufu Bongo, Muna Love, amezungumza na waandishi wa habari leo nyumbani kwake maeneo ya Mbezi jijini Dar es Salaam na kuweka wazi jinsi ambavyo alikutana na Peter Zakaria Komu, mwanaume ambaye hivi karibuni ilisemekana kuwa ndiye baba wa mtoto wake Marehemu Patrick.

“Nilikutana na Peter jijini Mbeya tukiwa tunafanya kazi Safari Pool Table, tulikaa kwenye mahusiano kwa miezi miwili tukaingia kwenye ndoa, lakini kuna vitu nilivyokutana navyo kwenye ndoa hiyo nikaamua kuachika.

“Wakati naingia kwenye mahusiano na Peter nilikuwa nina mimba ya Casto ya miezi miwili, Casto aliikana mimba hiyo. Baadaye alirudi wakati mtoto Patrick akiwa na miaka mitatu. Kwa sababu nilizaa nikiwa kwenye ndoa na Peter ndiye alisimamia hata ubatizo ndizo picha zilizosabaa, lakini hata yeye Peter anaujua ukweli kuhusu mtoto huyo.

“Tulifanya taratubu na Casto za kubadilisha jina la mtoto pale RITA lakini kuna ugumu uliotokea, lakini tulikuwa tunaendelea kufuatilia,” amesema Muna.
 
mnh,kuna kitu kinaitwa assertive tactics in impression management..

msimcheke muna, labda na nyie mngekua kama yeye,mngefanya the same...

desperate need to repair image ambayo imekua tarnished,

pole Muna,mie nakuelewa unachofanya,

ila ,

iwe mwisho kuwasiliana na waandishi,

unamwaga petrol kwenye moto tayari…

wataendelea kukusema tu..

wanadamu wabaya..

watavunja ndoa yako for real
 
Back
Top Bottom