Mungu Akikuita Amekuamini Usijitazame Ulivyo Analijua Hilo Na Akakuchagua

Mungu Akikuita Amekuamini Usijitazame Ulivyo Analijua Hilo Na Akakuchagua

Samson Ernest

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2014
Posts
1,237
Reaction score
1,744
Yer 1:6 SUV
[6] Ndipo niliposema, Aa, Bwana MUNGU! Tazama, siwezi kusema; maana mimi ni mtoto.

Watu kama Yeremia wapo wengi Leo, wanaotazama hali zao za nje, au mazingira yao, udogo wao, na mambo mengine mengi.

Wanapochaguliwa na MUNGU kumtumikia katika eneo Fulani, huanza visingizio vingi vya kuonyesha hawawezi kutokana na hali zao za nje.

Yeremia alitoa sababu ya utoto, neno hili ukiliangalia katika tafasiri zingine, linaonyesha ni kijana au mtu asiye na uzoefu katika eneo alilopewa.

Kwa maana nyingine Yeremia alionyesha unyenyekevu wake mbele za Mungu, wale wasiopokea wito haraka huonyesha unyenyekevu wao, wanaona hawataweza kufanya vizuri vile MUNGU anataka.

Yeremia alijua wajibu anaopewa hakuwa mdogo, alikuwa na utahamu mzuri, alijua majukumu ya nabii yalivyokuwa makubwa, maana nabii alikuwa ni msemaji wa MUNGU kwa watu wake.

Kwa jukumu hilo alijiona kibinadamu hana mamlaka ya kinabii ya kuzungumza na watu, KAZI ambayo ilikuwa nzito na hatari.

MUNGU hachugui mtu kutokana na umri wake au uwezo wake wa kibinadamu, humchagua kutokana na vile anaona Yeye, na akishamchagua Neema na nguvu zake huambatana na Huyo mtu.

MUNGU akishamchagua mtu hamwachi mwenyewe au peke yake, huweka au humpa upako wa kuweza kulifanya hilo jukumu kwa ufanisi mzuri.

Napenda uelewa kwamba, Mungu huangalia moyo wa utii kwa mtu kama alivyouona kwa Yeremia, akishajua ataweza kukutumia eneo Fulani, hataangalia mazingira yako uliopo sasa au umri wako mdogo.

Tunajifunza kwamba tunaweza tukawa na hofu za kawaida za kibinadamu, au tusiwe tayari kwa wito wa Mungu, hali hizo mbele za Mungu ni za kawaida na haziwezi kumzuia Mungu kumtumia Yule anayemtaka.

MUNGU akishamchagua mtu, huondoa hofu hiyo na kuweka ujasiri mkubwa ndani yake, sivyo hivyo Tu, anaweka maneno ya kuzungumza kinywa chako, na kumpa Mtumishi wake ulinzi wa kutosha.

MUNGU hawezi kukupa eneo ngumu la kumtumikia bila kukupa na ulinzi wake, alijua kile kilikuwa kinamtisha Yeremia, lakini alimpa maneno, na ulinzi wa kutosha.

Ikiwa Mungu amekuita kwenye eneo Fulani au ofisi Fulani itumikie pasipo hofu yeyote, mtazame Mungu utaona utajiri mkubwa aliokupa katika nafasi hiyo.

Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana
Samson Ernest
 
Naye alipokwisha kusema haya, makutano wakasema kwa sauti kuu,"nabii mkuu ametokea jf",kisha wakamletea wagonjwa na wenye shida mbalmbali ili awaponye.
Anayeponya ni Yesu na anafanya kazi mahali penye imani, waje nipo tayari kuwaombea, wakiamini watapokea uponyaji wao.
 
Mimi imani yangu huwa inaniambia mtu ukifa hapa duniani kuna pengo flani Mungu anakua kakupeleka kuliziba sayari nyingine huko.na mtu akizaliwa hapa kuna pengo huwa kaletwa kuliziba..
 
Somo zuri sana mtumishi. Naomba nisaidie kujua,
  • je nitajuaje kama Mungu ameniita? Nitaona nini?
  • Je nitajuaje ni huduma gani aliyonipa kati ya zile tano? Yaani nitajiuaje kama mimi ni mwalimu, nabii etc?
-Je nitajuaje Mungu anataka kunitumia kwa viwango gani, mf kitaifa au kimataifa?
- Je nitajuaje kama natakiwa kutumika siku zote chini ya mtu au niwe na huduma yangu mwenyewe.
Bado maswali mengi juu ya hili ila tuanze kwanza na haya, Asante kwa muda wako mtumishi 🙏
 
Mimi imani yangu huwa inaniambia mtu ukifa hapa duniani kuna pengo flani Mungu anakua kakupeleka kuliziba sayari nyingine huko.na mtu akizaliwa hapa kuna pengo huwa kaletwa kuliziba..
Jambo muhimu imani yako isiwe nje ya neno la Mungu
 
Somo zuri sana mtumishi. Naomba nisaidie kujua,
  • je nitajuaje kama Mungu ameniita? Nitaona nini?
  • Je nitajuaje ni huduma gani aliyonipa kati ya zile tano? Yaani nitajiuaje kama mimi ni mwalimu, nabii etc?
-Je nitajuaje Mungu anataka kunitumia kwa viwango gani, mf kitaifa au kimataifa?
- Je nitajuaje kama natakiwa kutumika siku zote chini ya mtu au niwe na huduma yangu mwenyewe.
Bado maswali mengi juu ya hili ila tuanze kwanza na haya, Asante kwa muda wako mtumishi 🙏
Asante sana kwa swali lako, kutokana na mazingira na malezi yetu, na kiwango chetu cha neno tulichonacho ndani, inaweza ikawa changamoto kwa baadhi ya watu wengi kujijua. Ila utaona msukumo mkubwa ndani yako kufanya jambo fulani katika hizo huduma, kadri unavyozidi kufanya utaona unajisikia vizuri na usipofanya unajisikia vibaya.
Unaweza usijitambue wewe, ila watu wakaanza kukuita mchungaji, au mwalimu, au mwinjilisti, au mtume, au nabii... Baada ya muda utajikuta umeingia rasmi kwenye eneo husika.
 
Oh Asante sana mtumishi wa BWANA barikiwa saaana 🙏
 
Mungu akikuita maana yake umeenda dead. Au jamii yetu tunamis use huo msemo.
 
Back
Top Bottom