Mliofuatilia mambo ya Kenya, unabii wa huyu nabii ulitimia?Ndugu wapendwa, kama ilivyoandikwa katika Mt 24:11, hizi ni siku za mwisho; manabii wengi wa uongo wametokea na kuanza kuwadanganya wengi. Fuatilia Youtube na mitandao mingine utaona video nyingi za manabii wanaoeleza kwamba wameambiwa na Mungu waseme waliyoyasema.
Miongoni mwa manabii hao ni wale waliotabiri yatakayotokea mwaka huu katika nchi mbalimbali duniani.
Ni muhimu kukumbuka kwamba sifa kuu ya nabii wa uongo ni kutotimia kwa maneno aliyosema. Hivyo mwaka huu ukipita, tusipoona kutimia kwa unabii walioutoa, basi tunapaswa kuelewa kwamba hao sio manabii wa kweli ni manabii wa mchongo, wanaotumia jina la Mungu kuwadanganya wengi.
Na tukiishawatambua, tujiepushe nao tusije tukapotezwa. Hata kama watatoa ishara au kufanya miujiza, tusidanganyike.
"Ikiwa kile nabii anachotangaza kwa jina la BWANA hakikutendeka au kutimia, huo ni ujumbe ambao BWANA hakusema. Nabii huyo amesema kwa ujuaji. Msimwogope huyo." (Kum 18:22)
sasa kuna unabii wa onyo kwamba msipoomba kitu fulani kitatokea. Watu wameomba kivyao. Hicho kitu hakikutokea. Hapo vipi?Ndugu wapendwa, kama ilivyoandikwa katika Mt 24:11, hizi ni siku za mwisho; manabii wengi wa uongo wametokea na kuanza kuwadanganya wengi. Fuatilia Youtube na mitandao mingine utaona video nyingi za manabii wanaoeleza kwamba wameambiwa na Mungu waseme waliyoyasema.
Miongoni mwa manabii hao ni wale waliotabiri yatakayotokea mwaka huu katika nchi mbalimbali duniani.
Ni muhimu kukumbuka kwamba sifa kuu ya nabii wa uongo ni kutotimia kwa maneno aliyosema. Hivyo mwaka huu ukipita, tusipoona kutimia kwa unabii walioutoa, basi tunapaswa kuelewa kwamba hao sio manabii wa kweli ni manabii wa mchongo, wanaotumia jina la Mungu kuwadanganya wengi.
Na tukiishawatambua, tujiepushe nao tusije tukapotezwa. Hata kama watatoa ishara au kufanya miujiza, tusidanganyike.
"Ikiwa kile nabii anachotangaza kwa jina la BWANA hakikutendeka au kutimia, huo ni ujumbe ambao BWANA hakusema. Nabii huyo amesema kwa ujuaji. Msimwogope huyo." (Kum 18:22)
hao manabii wa uchaguzi wameweka backdoor , watu waombe yasitokee --- maana yake aliyoyasema yasipotokea basi maombi yatakua yamefanya kazi kuepushaUnamaanisha nini kuomba kivyao?
OK, nimekupata, mkuu.hao manabii wa uchaguzi wameweka backdoor , watu waombe yasitokee --- maana yake aliyoyasema yasipotokea basi maombi yatakua yamefanya kazi kuepusha
nadhani ndo anavomaanisha mkuu --- kifupi ni openended unabii
Backdoor unaelwa maana yake mkuu?OK, nimekupata, mkuu.
Jambo hilo linahusiana na ile habari ya Nabii Yona na mji wa Ninawi (Yona 3:4-10).
Nabii Yona alienda Ninawi kuhubiri maneno ya Mungu. Akatabiri kwamba “Baada ya siku 40 Ninawi itaangamizwa.”
Watu wa Ninawi wakasikia, wakatubu, wakaacha dhambi zao, na kuanza kuomba na kufunga. Mungu akaona bidii yao na unyenyekevu wao na hakutenda uharibifu aliokuwa ameukusudia.
Huo ni mfano wa wazi wa unabii usiotimia kutokana na maombi ya watu waliopewa unabii. Ninawi haikupatwa na madhara kwa sababu ya maombi na toba ya watu wa mji ule. Hapo hatuwezi kusema nabii yule ni mwongo. Kama wasingetubu na kuomba, ni wazi mabaya yangewapata.
Naomba nifafanue vizuri. Pale mwanzoni nimesema sifa kuu ya nabii wa uongo ni kutotimia kwa unabii aliotoa. Hata hivyo, sifa hiyo inaambatana na sifa nyingine za manabii wa uongo, kama nilivyozieleza katika uzi huu:
Manabii wa "Mchongo" - Njia rahisi ya kuwatambua na kujiepusha nao
Nyakati hizi kuna watu wengi wanaoitwa manabii. Nabii ni mtu anayepokea ufunuo au maono kutoka kwa Mungu na kuyatangaza kwa watu. Kwa maneno mengine Nabii ni mtu anayeongea kwa niaba ya Mungu. Je, kila anayejiita Nabii ni nabii wa kweli? Biblia inatufundisha kwamba siku za mwisho, manabii wengi...www.jamiiforums.com
cc: Mcharo son
Unamaanisha kwamba in case unabii wao usipotimia, tayari wana backdoor (kisingizio au njia ya kukwepa lawama kwamba wao ni manabii wa uongo)?Backdoor unaelwa maana yake mkuu?
Naam, sawa mkuuUnamaanisha kwamba in case unabii wao usipotimia, tayari wana backdoor (kisingizio au njia ya kukwepa lawama kwamba wao ni manabii wa uongo)?
If so, mfano wa Nabii Yona haufiti kwa hao. Nabii Yona alisema wazi kabisa kwamba Ninawi itaangamia. Wanaoweka backdoor wanatoa unabii kisha wanasema: "ombeni sana yasitokee." Yakitokea waliyotabiri, watasema "si mnaona, nilitabiri ukweli." Yasipotokea watasema: "watu waliomba sana, hivyo maombi yao yamezuia..."
Are we together?
kuomba kisiri siri au maombi ya mtu binafsi kwa MunguUnamaanisha nini kuomba kivyao?