Wakusolve
JF-Expert Member
- Jul 30, 2020
- 561
- 997
Warumi 8:31
Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu?
Katika bibilia tunaona kwamba Mungu akiwa upande wako akuna kitu kitakacho kudhuru kwenye maisha yako.
Mungu akiwa upande wako maadui wanaweza tumia njia zote kuweza kukumaliza lakini wakashindwa na Mungu kutumia njia hiyo kuonesha nguvu zake.
Paulo na sila walitupwa gerezani sababu ya kuhubiri injiri na kwenda kinyume na mafundisho ya makuhani na mafarisayo ambao wao awamini katika Yesu kristo ,
Lakini wakiwa gerezani malaika wa bwana wakaweza kuwaokoa mbele ya ulinzi mkali.
Daniel alitupwa ndani ya shimo la simba sababu ya kumtumikia Mungu lakini malaika wa bwana waliweza kumlinda na kutoka salama,
Meshack, shadrack na Abelinego walikataa kuabudu sanamu ya dhahabu ya mfalme wa babeli nebukadreza na kusema wana muabudu Mungu wa mbinguni pekee
Mwisho wakatupwa kwenye tanuri la moto lakini malaika wa bwana aliwalinda na kutoka salama na utukufu wa Mungu ukaonekana kwa mfalme wa babeli.
Katika maisha yako, Mungu akiwa na wewe akuna mtu au adui anaweza kukushinda, unapitia changamoto za watu kukufanyia ubaya , usiuzunike, usilipize kisasi,
Mungu anaona shida zako ukifika wakati sahihi Mungu atatumia hizo changamoto kuonesha utukufu wake kwenye maisha yako kwa kukuinua mbele za maadui zako.
Unapitia changamoto ngumu za kimaisha usiogope Mungu anaona kilio chako, anaona maombi yako ukifika wakati sahihi anaweza badilisha maumivu yako na kuwa furaha kwenye maisha yako.
Mungu anaweza tumia siku moja kubadilisha kila kitu kwenye maisha yako,
Mungu alibadilisha siku moja ya Yusuph ambayo alikuwa sio kitu, kupitia kusalitiwa, kuuzwa utumwani na mfungwa
baada ya kuweza kutafsiri ndoto tu hii ikapelekea kuwa waziri mkuu wa Misri na mtu muhimu wa utawala wa mfalme farao
Hivyo kuwa mvumilivu na imani kwa kile unachopitia hiwe changamoto ya fedha, mahusiano, afya, nk kwamba utashinda, endelea kumuomba na kumtegemea Mungu atajibu maombi yako.