"Mungu anaangalia roho haangalii mavazi" ni kauli inayohamasisha mmomonyoko wa maadili. Wakristo tuwe na msimamo juu ya mavazi kanisani

Nipo hapa kupaza sauti juu ya mmomonyoko wa maadili,

Mambo ya mtaani yaishie mitaani, yanapoanza kuzoeleshwa makanisani si sawa, makanisani inabidi kuwe sehemu ya mfano wa kuigwa linapokuja suala la maadili.
Si ulishatuambia sa mbona unafungua nyuzi zimefanana kila siku? Upo sawa?
 
Huu utamaduni umekuwa ni cancer kwa ukristo maana baadhi ya waumini waliozoea kuvaa hovyo wakienda kuanzisha makanisa yao wanachafua ukristo, Mtu kama Masanja anavaa kata k / Mlegezo / Suruali chini ya ma*****
Tena huyu ni mfano mbaya kwa wachungaji vijana, anajifanya ni wa kisasa, kanisa lake ni jipya amekuwa akizoazoa, tena kwa kauli zake anasema anapokea waliotengwa na kufukuzwa kwenye makanisa yao anawakaribisha kanisani kwake. Hatukatai akiwapenda na kuwapokea wenye dhambi, ila awafundishe kuacha dhambi na kuishi maisha matakatifu ya wokovu. Mienendo yao na sifa zao ziwe njema, wavae mavazi yenye staha kwa ukristo. Dhana kwamba Mungu anaangalia roho haangalii mavazi ni dhana ya upotoshaji maisha ya kikristo. Mavazi ni kielelezo cha tabia ya mtu na haiba yake
 
Ni kanisa gani hilo mkuu, maana baadhi ya makanisa makubwa pale nje utakuta babgo kuubwa kuhusu mavazi yanayotakiwa kuvaliwa. Ukivaa vibaya unarudishwa.

Lakini bado wakristo wengi wanavaa hovyo sana kwenye nyumba za ibada.
Bora avae suruali ila sio kimini, huko nyuma mgongo wote upo wazi, mtindi ameuboost unaonekana waziwazi.

Kikubwa kama mwanaume nenda na kilichokupeleka huko kanisani, ukiwa na mawazo ya ngono hata kucha utatamani.
 
nimeliahuhudia hili kwenye makanisa makubwa ya hawa wazee wa mafutaa ya upako
hawa wazee wa mafuta ya upako hawakemei dhambi wala hana mahubiri ya kutubisha wenye dhambi, wao ni sadaka na uuzaji wa hayo mafuta na maji ya upako wao tu, mara keki, mara udongo na upuuzi mwingine mwingi, hawashughuliki na dhambi. Wazee wa upako wamepotoka na Mungu hayuko nao amewaacha wajifanyie mambo kwa kutumia akili zao
 
Mifano ya haraka ni hii, naamini hata kkt wameweka bango ila waumini washazoea sababu ishazoeleka hakuna wa kuwakaripia

 
Huko ni kwa kukimbia, wanawake wengi ni kazi rahisi sana kuwadanganya kwa imani wamewazoa wengi sana
 
Kumbe hoja siyo nguo, bali ni ukosefu wa maadili na matamanio
Mazingira uleta matamanio, mwanamke mmoja mwenye makalio uchi anaweza fanya uzinzi na hata wanaume 300 kwa siku moja uzinzi ni dhamira na sio kitendo ni hitimisho.
Kabla ujazini na mtu ni lazima akushawishi kupitia matamanio. Mavazi uzungumza kuhusu tabia ya mtu.
 
Hao ni wafanyabiashara,upako wa kuangusha watu KWA kukata teke hewani unauzwa milioni 4 kwa waganga, upako wa keki, maji, mafuta, vitambaa, chumvi unauzwa milioni 40 kwa waganga.
 
Huko ni kwa kukimbia, wanawake wengi ni kazi rahisi sana kuwadanganya kwa imani wamewazoa wengi sana
wanawake wanawaamini sana hawa wazee wa upako, wakipulizwa pfuuu wanadondoka chini na kuanza kufurukuta
 
Wakongwe wa zamani huwa hatusifu wala kuabudu tunawakodolea macho tu. Utaabudu vipi wakati ushatolewa kwenye uwepo wa Mungu
Nilifikiri ni mimi tu yani hakuna upako wowote napata kutaka kwa hawa praise team. Huwa naangalia matako, nyonyo, hips na miguu pekee jumlisha mitindo ya nywele.

Kiukweli makanisa mengi kwa sasa ni mabanda ya makahaba na vijana wahuni wahuni tu katika kivuli cha wamtumikiao Mungu

Na ndio maana huwa napata mashaka na huyo Mungu wanaemhubiri kila siku
 
Kwanza kabisa, thibitisha huyo Mungu yupo kweli.
 
Picha zinaonyesha wasichana wapo mazingira ya bar ama mahotelini.
 
wachungaji wazee wa siku nyingi enzi za injili kali ni wahafidhina hawataki mbwembwe za mavazi na mitindo mbele ya madhabahu huwa wanatimua wadada wanaovaa kikahaba ndio wanaenda kwa hao wachungaji vijana wanawapokea na kuabudu nao hivyohivyo walivyo
 
Mie napenda wadada wanavyo boost matiti
 
Unakuta mchungaji mwenyewe ni kijana msela tu, yeye mwenyewe kavaa kisela yuko madhabahuni, praise team yake nayo imevaa nguo tata, nyimbo na pambio zinabadilishwa twini, mara sebene, mara singeli na sasa mara amapiano, hapo sasa kwa muumini wa kale aliyekulia kwenye maadili ya kikristo atawezaje kuabudu katika hali ya vurugu na fujo hizo? Wakongwe tukiingia makanisa haya huwa tunatulia tu na kutazama vijana wakichakarika katika ibada yao
 
Tuseme ukweli tu, ila hizi picha si za hao waenda kanisani. Huwezi kwenda kanisani umevaa chupi, uvaaji mbovu upo lakini si huu kwenye picha hizi
 
Kwanza tukubaliane,suala la mavazi kulingana na Agano jipya ni kweli sio ishu. Kama palikuwa na restrictions za mavazi basi ziliisha wakati wa agano lile la awali tena ambalo lilikuwa kati ya Mungu na Waisrael. Sasa kwa kutambua hilo kama jamii inapaswa kujiuliza ni namna gani inatafsiri mavazi yasiyo na staha.

Lakini pamoja na hayo makanisa sio sehemu ya kuwatenga watu wanaoonekana kwenda kinyume na maadili,badala yake ni mahali ambapo watu wa namna hiyo wanakwenda ili kujifunza na mwisho waachane na tabia ambazo zinawapelekea wao kuvaa mavazi yasiyo na staha. Kimsingi hata Yesu hakuja kwa ajili ya walio wema bali kwa ajili ya wenye dhambi.

All in all mavazi hayaelezi hali ya usafi wa moyo wa mtu,ingawa mara nyingi wanaovaa mavazi ya hovyo moyoni wanakuwaga na lengo lao ambalo linakwenda kinyume na mapenzi ya Mungu. Kikubwa waaalimu waendelee kujitahidi kuwafundisha watu neno la Mungu,watu wamjue Mungu na hayo yote tunayoona ni ya kukwaza yatakoma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…