Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 1,831
- 5,489
Tuendelee kufundishana.
Wakati mwingine ninaumia ninapoona watu wanaomba na hawapokei kama wanavyotakiwa kupokea, si kwamba Mungu hajakusikia, amekusikia, na atakujibu, ila kuna vitu ambavyo nawe unatakiwa kufanya.
Kuna dhambi ambayo Mungu anaichukia sana. Ngoja nitumie Mungu manake mtanielewa japokuwa Yeye hajali kuhusu maandishi, yeye hajali kuhusu mwili wako, mavazi yako, anachokijali ni roho yako tu.
Ndiyo!
Mungu anajali roho na si mwili wako.
Utakapokufa, mwili utauacha hapahapa duniani, ataichukua roho aliyokupa, so mtaziosha maiti, ziwe safiii kama theluji, ila kama roho hazikuwa safi, mnafanya kazi bure.
Dhambi ambayo Mungu haipendi kabisa ni wewe kumuabudu Mungu mwingine tofauti na yeye. Ndiyo! Kuna watu tunaabudu miungu mingine na hatumuabudu Mungu aliye juu.
Kama unaamini kwenye mambo ya ibada, unapofika muda wa ibada, unatakiwa kwenda huko, huendi, muda wa ibada upo dukani kwako unaendelea na biashara, this means kwamba hiyo biashara ndiyo mungu wako.
Muda wa ibada unapofika, badala ya kwenda kufanya ibada umejifungia bandani unaangalia mpira, hii inamaanisha huo mpira ndiyo Mungu wako. Sijui unanielewa!
Muda wa kumwabudu Mungu, nenda kamwabudu, achana na mambo mengine, Mungu ana muda wake, huo muda umefika, umeamua kumpa mungu mwingine. Sijajua kama mnanielewa.
Hili ni chukizo kubwa sana kwa Mungu, tunaiabudu miungu mingine pasipo kutarajia, mwisho wa siku unamuomba Mungu akubariki, akusaidie lakini maombi yako yanagonga mwamba. Unaendelea kuteseka, magonjwa na madeni yanakuandama, suala ni moja tu, umeiabudu miungu mingine bila kujua.
Sijajua kama mnanipata.
Kwa watu kama sisi ambao hatuamini masuala ya kwenda kanisani ama msikitini ndiyo kuzungumza na Mungu, huwa tunafanya yale ambayo Mungu ametaka tuyafanye. Nitasaidia mayatima, nitalisha wajane, nitampenda kila mtu na kubwa zaidi, nitamshukuru Mungu kwa mambo yake makubwa.
Kwenye suala la kumshukuru Mungu tumeligeuza na kuwa la kawaida sana. Yaani unaamka asubuhi, unamwambia Mungu Asante, lakini je, hiyo Asante imetoka moyoni? Kuna aina mbili za asante kwa Mungu, kuna ile kutoka moyoni na ya mazoea.
Leo mpenzi wako anakwambia I miss you, wewe hujammisi lakini unaandika I miss you too, haya ndiyo mazoea ambayo sasa unatakiwa kuyaacha, unapomshukuru Mungu, hakikisha unaitoa ile moyoni mwako kabisa.
Faida za kumshukuru Mungu.
Unapoumwa kichwa, unakunywa dawa, baadaye unapona unamshukuru Mungu, unamshukuru kimazoea lakini hebu pata ajali, ulazwe hospitalini, madaktari waseme imeshindikana halafu ghafla tu, ukaomba ukapona, shukrani utakayoitoa hapo ni kutoka moyoni kabisa.
Umeshinda njaa, huna pesa, watoto hawana ada, mambo yako yanakwenda hovyo, ukamuomba Mungu, ukamuamini halafu akarekebisha kila kitu, ndugu yangu utakavyomshukuru Mungu ni tofauti kabisa.
Tunamshukuru Mungu kila siku, je, tunamshukuru kutoka moyoni? Tunamuomba Mungu atupe, lakini je, sisi tunatoa?
Ombaomba na watu wenye matatizo unaowaona mitaani, wengine si binadamu kabisa, wengine huwa malaika, waliojivika mwili wa binadamu na kuja kukuomba. Umemuomba Mungu jambo kubwa sana, tena kubwa ambalo hajawahi kumfanyia yeyote kwenye ukoo wako, ni kweli Mungu anatamani akufanyie, lakini anaanza kukujaribu, anakuletea ombaomba mwenye shida, yatima ama mjane, je, utaweza kumsaidia? Utaweza kutumia senti ya mwisho kwao?
Wakati mwingine nakuwa sina pesa kama binadamu wengine. Hapohapo unapigiwa simu na kuambiwa dogo ada inahitajika, hela ya ada unayo, lakini badala ya kumpeleka mtoto shule, unaitumia kwenda kulisha mayatima na ombaomba, unadhani huyu Mungu ataniangalia kwa jicho gani? Unadhani ataninyima nikimuomba chochote?
Unakaa na kumshukuru Mungu kila siku, lakini hiyo shukrani inatoka moyoni mwako ama kimazoea tu? Mungu haimfikii kama inatoka kimazoea, utashangaa unamshukuru Mungu kila siku lakini unaandamwa na matatizo kibao.
Mfukoni una 50,000/= halafu ghafla unatakiwa kusaidia watu, unaamua kutoa elfu mbili, hapohapo unataka Mungu akufanyie mambo makubwa kwenye maisha yako, je, mambo hayo yanalingana na shilingi 2000 yako?
Ndoto yangu ni kujenga jumba la milioni 150 hapo baadaye, ili nipate hiki kitu ni lazima nijitoe sana kwa watu, nipoteze muda wangu, wakati nikipeleka chakula, mvua inanilowesha, nafika nimelowa chapachapa, wakati mwingine unafika umepigwa sana na jua, jasho kama maji, ila unafanya hayo yote kwa sababu unahitaji Mungu akupe vile vitu vikubwa.
Vitu ninavyovitaka ni lazima nitoke jasho kwa ajili ya wahitaji, vitu ninavyovitaka ni lazima nilowanishwe na maji ya mvua chapachapa kwa kuwa ninataka vitu vikubwa mno. Kabla ya Mungu kunipa vitu hivyo lazima anipitishe kwenye vitu mbalimbali, anataka aone je utafanya?
Upo home siku nzima, hakuna mvua, unapotaka kwenda kuwalisha watu tu, mvua hiyo inaanza kunyesha, tena kubwa, Mungu anataka kuona utafanya?
Unataka Mungu akupe utajiri, biashara zako ziingize mpaka milioni 10 kwa mwezi, je, unaweza kutoa hata senti yako ya mwisho kwa ajili ya watu wengine kwenye kuwasaidia?
Mungu anaangalia moyo wako. Ukiwa na elfu hamsini, ukamtolea Mungu elfu mbili, BRO! YOU ARE WASTING YOUR TIME (UNAPOTEZA MUDA WAKO).
Sema tu, mimi nataka kwenye kila mshahara wangu, nichukue asilimia kumi nitoe kwa ajili ya wenye uhitaji. Unapokea laki moja kama mshahara, unamtolea Mungu elfu tatu halafu unataka Mungu aonekane kwenye maisha yako, unapoteza muda wako.
Naujua utamu wa kubarikiwa, nimeonjeshwa sana na Mungu na ndiyo maana ninakuandikia haya ili siku moja na wewe upate vile ninavyovipata. Sijisifu ila ninakwambia ukweli kuhusu huyu Mungu.
Mungu yupo, anafanya kazi sana, ila kufanya kazi kwake anafanya na watu wanaojitoa kwa ajili ya wengine, anafanya kazi na watu ambao wanamshukuru kwa kila jambo.
Mimi nakufundisha vitu ambavyo nilifundishwa na mshua kuhusu Mungu. Yule mzee Mungu amlaze mahali pema peponi.
Chukua karatasi, andika mambo ambayo unataka kumshukuru Mungu. Kuna hili na lile uliwahi kumuomba, na hatimaye akakupa, hebu liandika.
Andika yote ambayo uliyataka na ukayapata, itakapofika majira ya saa tisa usiku, hata kama umelala, amka, yasome, halafu mwambie Mungu kutoka moyoni, nashukuru kwa hili, nashukuru kwa lile. Mwambie nashukuru kwa kunipa hiki, nashukuru kwa kuniokoa pale.
Kwa nini saa tisa usiku?
Ndiyo muda mzuri ambao akili yako, moyo na roho yako vinakuwa vimetulia. Na ndiyo maana hata meditation zinafanyika usiku mnene.
Unapita karibu na msikitini, unaona wameweka chombo cha sadaka, halafu unaingiza mkono mfukoni, unaweka mia tano huku mfukoni ukiwa na elfu kumi, na baada ya hapo unakwenda kumuomba Mungu kitu cha shilingi milioni 50.
Huna mtoto, magonjwa yanakuandamana, hauna ajira, kila kitu kipo hovyo, shukrani pekee ambayo utaitoa kwa ajili ya watu wenye uhitaji ni mia tano.
Yaani inamaanisha wewe kupata mtoto gharama yake ni 500, wewe kupata kazi, gharama yake ni 500, wewe kutusua maishani mwako, gharama yake ni 500.
Ndugu yangu! Mungu pekee atakayekujibu hapo ni Mungu wa makaratasi. Na siku ukiona umefanya hayo, akakujibu, njoo uniambie nimekaa paleeeeeeeee.
Hizi pesa usizitoe kama sadaka, siku hizi hizo sadaka watu wanakwenda mpaka kuhonga. Hizi nenda kwa watu wenye uhitaji, wafanyie kitu, nakuhakikishia Mungu ataonekana kwenye maisha yako hatua kwa hatua.
Kama unamuomba Mungu sana akufanyie kitu fulani na hajajibu, jaribu kubadilisha gia angani, fanya niliyokwambia.
Mungu wa yule anachelewa kujibu, ila Mungu wangu anawahi kujibu. Inawezekana tuna miungu tofauti. Wangu anawahi, wako anachelewa.

- Moyo wako utakuwa na amani, furaha na tumaini jipya.
- Utagundua kwamba kila kitu unachokifanikisha kwenye maisha yako si kwa nguvu zako.
- Utashangaa hata yale ambayo ulisema huyaweza, sasa hivi unayaweza.