Mungu Atakuinulia Watu Wa Kukataa Ubaya Unaotaka Kutendewa

Mungu Atakuinulia Watu Wa Kukataa Ubaya Unaotaka Kutendewa

Samson Ernest

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2014
Posts
1,237
Reaction score
1,744
Yer 26:16 SUV
[16] Ndipo wakuu na watu wote wakawaambia makuhani, na manabii, wakisema, Mtu huyu hastahili kuuawa; kwa maana amesema nasi katika jina la BWANA Mungu wetu.

Hapa tunaona nabii Yeremia alipokuwa kwenye hatari ya tishio la kuuawa kwa sababu alitoa ujumbe mgumu kwa watenda mabaya, uliokuwa umebeba hukumu dhidi ya Yerusalemu na Hekalu.

Jambo la kushangaza hapa, nabii Yeremia alipata watetezi, Mungu aliinua viongozi katikati ya wale waliokaa kikao cha kutaka kumuua, walimtetea sana Yeremia asiuwawe kwa sababu alitoa ujumbe wa BWANA na sio wa kwake.

Wakasema, "Mtu huyu hastahili kuuawa; kwa maana amesema nasi katika jina la BWANA Mungu wetu."

Pamoja na ujumbe huu ulikuwa mgumu, ulikuwa ni wa kweli, sio wa kweli tu, ulitoka kwa Mungu moja kwa moja, kwa maana nyingine walitaka kumuua mjumbe wa Mungu. Kesi yao ilikuwa na Mungu na sio Yeremia tena, ndio maana tukaona viongozi wachache hawakutaka kujiingiza kwenye hatia isiyo na msingi wowote.

Katika utumishi wetu tunaweza kukutana na hali kama ya nabii Yeremia, hatupaswi kufukia ujasiri wetu na kushindwa kuzungumza kweli ya Mungu, hata kama kuna tishio la kifo mbele yetu.

Mdo 5:29 SUV
[29] Petro na mitume wakajibu, wakisema, Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu.

Sisi tumeitwa kuwa mashahidi wa kweli wa MUNGU, hatupaswi kutetereka kusema kile neno la Mungu au Roho Mtakatifu anatusukuma kusema juu ya kanisa, au taifa. Hata kama tunachosema kinapingana na jamii au mamlaka.

Tumeona wapo viongozi walijitokeza kumtetea Yeremia, hawa watu inaonekana walikuwa na hofu ya Mungu, au waliingiwa na hofu ya Mungu, kwa sababu waligundua haraka ujumbe ule ulikuwa unatoka kwa Mungu moja kwa moja na Yeremia alikuwa mjumbe tu.

Hata kwako itafika hivyo, hata kama wapo hawataelewa kile wenzao wanawaonya juu ya kile wanataka kufanya, uwe na uhakika Mungu atakuinulia watetezi wake. Mungu hawezi kunyamaza kimya juu ya watumishi wake wanaojitoa kwa ajili ya utumishi wake.

Mungu humpa ulinzi mtumishi wake yeyote aliye mwaminifu kwake, na ujumbe wa ki-Mungu haupimwi kupitia umaarufu wa mtu, au upole wake. Yule mtu mwaminifu mbele za Mungu na anayeishi kwa mapenzi yake, hutumiwa na Mungu.

Tumeona jambo kubwa sana kwa Yeremia, kutishiwa kwake kuuawa, Mungu alimwinulia watu wa kumtetea, maana waliitambua kweli ya Mungu kupitia kinywa cha nabii Yeremia.

Hatupaswi kuogopa, Yesu alishaweka sawa hili kwa kusema;

Mt 10:28 SUV
[28] Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika jehanum.

Yesu alimaliza kabisa na kuwaambia wanafunzi wake wasimwogope mtu anayeua mwili, bali wamwogope yule anayeua vyote, yaani mwili na roho. Maana yake lipo tumaini kwa wale waliokufa katika kuitetea haki au kweli ya Mungu.

Kuwa mwaminifu mbele za Mungu, ulinzi wa MUNGU utaambatana na wewe, atakuinulia watu kuwa ulinzi wako, utashangaa wanasimama na wewe na kukataa au kupinga ule ubaya unaopangwa kufanywa juu yako.

Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana
Samson Ernest
 
Back
Top Bottom