Mungu atuondolee moyo wa ubinafsi na ule wa kuwatamkia wenzetu mabaya pale wanapotuudhi

Mungu atuondolee moyo wa ubinafsi na ule wa kuwatamkia wenzetu mabaya pale wanapotuudhi

Hipo hivi mwanaume kabla hajaoa mafanikio ya maisha hutegemeana na yeye na juhudi zake ila mwanaume akaoa na akafunga ndoa basi mwanaume huyo humkabidhi mafanikio yake huyo mkewe yani mafanikio ya huyo mwanaume yatategemeana na dhamira ya mkewe ndio maana usishangae pale mwanamke anapokuwa na uwezo juu ya maisha ya mume wake

Kiufupi mwanaume akioa hupoteza uhuru binafsi juu muktadha wa maisha yake

Mwanaume ni kichwa cha familia

Mke ni mlinzi na msaidizi
 
Hakuna laana kabisa, kungekuwa na laana mleta uzi angekuwa ameshalaaniwa siku nyingi sana.

Mimi nabarikiwa kila kuchwao sababu nimekua furaha ya wanaonihusu

Pole Yoda kwa kuwa laana kwa nyumba yako
 
Amen.

Ingawa ndiyo maana mpaka Leo hii sitaki mwanamke maana kuna mwanamke alinitamkia laana ya kufukuzwa kazi na kweli nikaachishwa kazi wakati huko ndiko nilikuwa napata riziki.

Mwisho wa siku baada ya maisha kuwa magumu akawa analalamika wakati yeye ndiyo alinitia gundu ya kufukuzwa kazi eti kisa nachelewa kurufi home na kwenda kazini siku za weekend.

Nilichokifanya nilitafuta kazi nyingine kimya kimya nikawa hata nikipata mshahara simwambii nikawa kila siku ni kulalamika kinafiki kuwa sina kazi hivyo nakosa hela. Mwisho wa siku akakimbia mwenyewe.
🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom