Nina muda mrefu sijapanda daladala. Leo nimepqnda nilichokiona umo khaaa! Daladala imejaa hakuna sehemu ya kueka mguu. Kuna wale wanaonukia pafyumu za sh 200 zinaumiza pua na kichwa mtu unaweza ukazimia kwa harufu, halafu kuna wale wanaonuka jasho. Harufu hizi zinachanganyika kunatokea harufu ambayo haielezeki kama afya yako mgogoro unajikuta upo hospitali. Mungu awasaidie wapanda daladala wana hali ngumu sana.