Mungu hatutolala hatutochoka kukuita mpaka utakapo jibu

Mungu hatutolala hatutochoka kukuita mpaka utakapo jibu

TumainiEl

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
6,782
Reaction score
12,716
Mungu uliopo juu Mungu muumba wa vyote vinaonekana mpaka visivyo onekana. Wewe ni Mungu tusema Asante kwa kila Zawadi umetupa Taifa zuri Tanzania. Mungu wa Tanzania ni wanyonge na wachache umewapa kutuongoza wamekuwa na tamaa na kiu yakulitafuna hili Taifa kwa uchu wa mchwa walio na njaa Kali. Mungu kama Wazee wa kwanza wa Taifa wangekuwa na tamaa na uchu walio nao hawa vijana wa sasa hakika Taifa hili lingekuwa Mali ya mkoloni asubuh sana.

Mungu pita kwenye Mawizara ona yanayo fanyika na usiache mchwa hawa wakamaliza kula kabla hujapata dawa yakumaliza mchwa hawa. Mungu unawajuwa wazalendo katika Taifa hili na kamwe usiwaache roho zao zikamezwa na mapanzi.

Mungu hata kama Kuna mtu mmoja katika Taifa hili anania njema na Watanzazia Mungu hata kama ni dereva bodaboda umtoe huko kwenye bodaboda ukampandishe kwenye kiti chako pale ikulu katika wakati wako. Kama ulivyo mpandisha mchunga kondoo Daudi mpaka kuwa mfalme. Kama ulivyo mfanya Yusuph house boy tena kuitwa kwa kusingiziwa mbakaji Mungu wanyanyue vijana jasiri ktk mifumo na roho za Taifa la Tanzania.

Mungu waroho wapasikie ikulu kama wanavyoisikia mbingu ambayo hawajawi kuiona.

Mungu anaglia mawaziri wale, wazee wale na wanachama wale Walifurahi na walisema Mungu mkubwa baada Ya Rais wa Awamo ya Tano kufariki Dunia. Mungu kama wewe upo na unataka ikawe fundisho kwa kizazi hiki na kijacho basi kawape darasa ambalo kila mtanzania atakapo sikia majina yao atasema ipo adhabu Kali kwa wasaliti sio kutoka kwa wanadam ila kwako mwenyewe.

Mungu nasimama na Jamuhuri hii ya watu wa Tanzania nakusema viangaze vyombo vya usalama katika jicho la tofauti. Uwasi usifanikiwe ktk Taifa hili kila anaye panga uwasi akakutane na upanga wa Mbinguni na wajeshi lako tiifu la vijana hodari wa Jamuhuri ya watu wa Tanzania. Mungu ilinde serikali hii na ile inakuja Watete Baba. Tumekosa sana utuhurumie.

Mungu usiache waovu wakaisumbua Jamuhuri yetu pale jeshi na vyombo vya ulinzi vitashindwa Wewe ukasimame nakutulinda.

Baba hatutolala wala hatutofumba macho hata watoto wako tutakapo ona Nuru yako na hali yako ikitawa Taifa hili Teule katika Africa.

Amen.
 
Na kweli yezebeli kachanganyikiwa kabisa!

Hajui ateue nani akae wapi na afanye nini!!!
Kuna Mmama mmoja mtu mzima anasema hii teua tengua ya chini ya siku moja kuelekea siku kuapisha ni mbinu ya kutaka Attention au kiki na hilo jambo la teua/tengua sio mara ya kwanza kufanyika. Wanawake ndio wanajua hiyo michezo ya kutafuta attention. Hakuna cha system wala ni nini, ni kutaka attention tu na Kiki 😂
 
Back
Top Bottom