Mungu katengenezwa na nani?

Mungu katengenezwa na nani?

Hakuna proof yoyote ya uwepo wa Mungu.
 
Sikubaliani na wewe hapa. Huwezi kufanya hitimisho kwa a such very simple reasoning
Simple reasoning ipi imetoa hitimisho lipi?

Na umenisoma wapi na wapi mpaka kujua reasoning yangu ni simple?

Nimeandika kwa habari zaidi soma hivyo vitabu viwili.

Umevisoma?
 
Ushasema hakuna mungu,sasa je,msimamo wako ni upi baada ya kutokuwepo mungu ama ukweli ni upi?

Ukweli siku zote huwa upo tu,sasa tukisema kwamba wazo la kuwa kuna mungu linapotosha ukweli..ndipo napouliza ukweli ni upi ambao unapotoshwa na wenye kusema kuna mungu?

Maana kusema tu hakuna mungu haitoshi.
Ukweli ni kwamba kuna mengi hatujui.

Tuyatafutie majibu kwa uchunguzi.
 
Kwani hata sayansi ilianza kuandikwa na muislamu wa kiarabu anaeitwa Ibn-Alhaitham mwaka 1021. Ukitaka kujua mengi kuhusu hili ingia google halafu andika kitabu chake kiitwacho:" Book of Optics"
Sayansi ni nini?

Unafahamu mwaka 1021 ni juzi tu hapo na watu walikuwa washaamka miaka 2500 kabla ya kuzaliwa Kristo?
 
Ukweli ni kwamba kuna mengi hatujui.

Tuyatafutie majibu kwa uchunguzi.
Suala si kujua mengi.

Je,wewe binafsi ni uchunguzi gani hadi sasa umefanya kujua ukweli ambao ndiyo ulipaswa uelezwe badala ya kuelezwa kuwa kuna mungu? au labda umeshawahi kuchunguza kuwa pengine huyo mungu yupo ila watu wamekosea kumuelezea?

maana kama hujui unachokitafuta huwezi kukiona.
 
Ukweli uliopaswa kuelezwa ni hakuna Mungu.Mungu at the outset being mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote.

Nimegundua kwamba unaweza kujua ukweli na uongo wa masuala mengi kwa elimination method, na kwamba hata usipopata jibu kamili la swali leo, unaweza kujongea (converge) kwenye jibu sahihi kama unaondoa uongo kwenye mlinganyo wako na unachambua ukweli.

Huu niugunduzi mkubwa sana kwa sababu unakusaidia kupunguza mambo ya kuangalia ili kupata jibu lako kamili.

Kwa mfano, natafuta square root ya namba 2.

Sijui namna ya kupata jibu la square root ya 2 moja kwa moja.

Lakini najua kwamba square root ya 2 haiwezi kuwa kubwa zaidi ya 2.

Kwa hiyo mpaka hapo, bila hata ya kujua square root ya 2 ni nini, najua kwamba namba yoyote iliyo kubwa kuliko 2 haiwezi kuwa jibu sahihi.

Pia nikijua kwamba kila positive number ina positive na negative square root, najua kuna majibu mawili, moja positive na moja negative.

Pia najua kwamba 1 x1 = 1, kwa hiyo jibu langu litakuwa -+ namba fulani ambayo ipokati ya 1 na 2.

Kwa hiyo katika namba zote nime narrow down uchunguzi wangu kuuweka katika namba iliyo -+ kati ya 1 na 2 exclusive

Kwa elimination method hii hii nimeshaona Mungu wenu hayupo kwa sababu anaanguka nje ya test ya logical consistency.

Hii njia ya convergence inaweza kutumika kwenye mengi sana.

Na imeonyesha kwamba Mungu hayupo.
 
Kuratibiwa maana yake nini?

It is possible for complexity to arise from simplicity, computer algorithms and mathematical facts show that.

In fact, perfect equilibrium is always attached to nothingness.

So, if there is a perfect God, that God must be nothingness, because that is the epitome of perfection.

Anything that deviates from nothingness, deviates from perfection.

That is another way of saying and showing God does not exist.

Because he is too perfect to exist.

We are lucky to be imperfect.

Our imperfection is what allow us to exist.

For more see "Why Does The World Exist?" by Jim Holt

An even more interesting book is "A Universe from Nothing" by Lawrence M. Krauss

I enjoyed both immensely, the later more so.

Sio kila siku Quran na Biblia tu.

51BjAc2STiL._SX332_BO1,204,203,200_.jpg

220px-AUFN_LawrenceKrauss.jpeg
Nahitaji hivi vitabu mkuu, navipataje?
 
KENZY
Kwanza ninaposema kafiri simaanishi ni adui yangu mimi ila namaanisha ni mtu anaenda kinyume na maamrisho ya mungu.
Kwa hiyo mimi ninaamini wazi wakiristo ni makafiri.

Pili mungu hampi mtu adhabu mpaka amuulize suala hili jee hawakukujia minabii na mitume kukuonya ili utake msamaha kwangu na nikusamehe.Kwa hiyo mungu ana muadhibu mtu kwa kujifanya kwake anajua sana zaidi kuliko huyo mungu.

hlf kuna haja gani ya kumbakiza shetani wanapoishi wapendwa wako huku ukijiita wewe ni mfalme wa amani ama wewe ni tumaini la wanyonge..?
Mimi naamini hivi mungu ni tumaini la wanaomuamini na si tumaini la wanyonge wasiomuamini,halafu pia mungu mwenyewe anasema hivi kila jambo jema linatokana yeye na jambo baya linatokana na nafsi ya mtu mwenyewe kwa maana hiyo mola wangu mimi ni mwema na hana mabaya.

Ahadi ya mungu ni ya kweli hivyo aliposema kila Kiumbe atamuonesha nija njema ili mwenyewe aifuate kwa hiari pasi na kulazimishwa basi atatimiza hivyo hivyo milele. Hivyo mungu hakuwa na haja ya kuvunja ahadi ya kumteketeza shetani bali alimuacha kwa sababu yeye amechagua njia yake anayotaka. hivyo atapata hukumu ya hicho alichokifuata na yule atakae mfuata shetani nae atakuwa katika njia hiyo hiyo .

na kwa mapenzi yake mungu hakumuacha mja wake bali alimletea mitume na kitabu ili kuwaongoza kwake kazi ya mitume si kulazimisha ni kutahadharisha watakaofuata ndio wamefuata na wasiofuata basi ndio wamechagua hivyo.

hapo kwenye nyekundu: 1. kuhusu mungu kutumia reference ya manabii na mitume kuhukumu watu, inaonesha jinsi gani huyo Mungu amekosa sifa ya haki, upendo na usawa. Hivi nikuulize tu je wewe hao mitume na manabii ulishawahi kuwaona? Sasa huyo mungu atawahukumu vipi watu kwa kufuata stori alizozikuta ilihari anajua binadamu hajakamilika? Lazima binadamu atatumia utashi wake binafsi.

2. Mungu angekuwa ana muonesha mtu katika njia njema basi angemuangamiza huyo shetani. Sasa imekuaje amruhusu shetani amtawale binadamu wakati anajua kuwa kabisa kuwa binadamu hakukamilika?
3. Kwanini huyo Mungu amuumbe kiumbe dhaifu halafu mwisho wa siku akamtie kwenye moto wakati yeye ndio aliyempangia awe hivyo?
4. Kwanini huyo Mungu anawaacha watu wanaishi katika mateso, chuki, dhuluma, bila yeye kuwalinda?
4. Kwanini huyo mungu amekosa njia sahihi ya kuwafanya watu wamjue yeye wakati yeye anajisifu kuwa ana uwezo, haki, na upendo sasa kwanini dini zisambazwe kwa uonevu wa vita, biashara ya utumwa, harakati na vita za kugombea dola?
5. Mungu ana umbile gani? Kama ana umbile basi nae kaumbwa. Kama hana umbo lolote basi huyo mungu hayupo
 
Ukweli uliopaswa kuelezwa ni hakuna Mungu.Mungu at the outset being mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote.

Nimegundua kwamba unaweza kujua ukweli na uongo wa masuala mengi kwa elimination method, na kwamba hata usipopata jibu kamili la swali leo, unaweza kujongea (converge) kwenye jibu sahihi kama unaondoa uongo kwenye mlinganyo wako na unachambua ukweli.

Huu niugunduzi mkubwa sana kwa sababu unakusaidia kupunguza mambo ya kuangalia ili kupata jibu lako kamili.

Kwa mfano, natafuta square root ya namba 2.

Sijui namna ya kupata jibu la square root ya 2 moja kwa moja.

Lakini najua kwamba square root ya 2 haiwezi kuwa kubwa zaidi ya 2.

Kwa hiyo mpaka hapo, bila hata ya kujua square root ya 2 ni nini, najua kwamba namba yoyote iliyo kubwa kuliko 2 haiwezi kuwa jibu sahihi.

Pia nikijua kwamba kila positive number ina positive na negative square root, najua kuna majibu mawili, moja positive na moja negative.

Pia najua kwamba 1 x1 = 1, kwa hiyo jibu langu litakuwa -+ namba fulani ambayo ipokati ya 1 na 2.

Kwa hiyo katika namba zote nime narrow down uchunguzi wangu kuuweka katika namba iliyo -+ kati ya 1 na 2 exclusive

Kwa elimination method hii hii nimeshaona Mungu wenu hayupo kwa sababu anaanguka nje ya test ya logical consistency.

Hii njia ya convergence inaweza kutumika kwenye mengi sana.

Na imeonyesha kwamba Mungu hayupo.
Tafuta ukweli ndugu kwa jinsi maelezo yako yanaonesha umekomea hapo hapo kuwa hakuna mungu,na unatumia muda na nguvu katika kuzidi kujihimalisha hapo hapo tu kuwa hakuna mungu na si vinginevyo.

Na ndiyo maana watu huona kusema kwenu hakuna mungu ni kama imani kwenu ambayo mnaitetea humu.
 
Ningeweza kukuambia kuhusu Heisenberg's Uncertainty Principle, quantum entanglement, wave particle duality, tiny breaks in space-time causality at the quantum scale, black hole decay, the heat death of the universe, relativistic time dilation etc.

Lakini ni habari ndefu na nyingine ziko too theoretical zinahitaji a collider that is the size of the solar system to explore experimentally.

Ninachokwambia hapa si mwisho wa ninachojua.

Ni mwisho wa ninachoweza kukitetea bilakuandika mambo ambayo yatazua mjadala utakaokuwa umezidi kimo 99.9% ya audience.

Na nina shaka kama utakuwa na maana.

Na browser inaweza kushindwa ku support formulaes za mjadala.

Kuna mijadala mingine inahitaji hesabu za Roger Penrose za kutoka "The Road To Reality: A Complete Guide To The Laws of The Universe".

Wataumia watu vichwa bure hapa.

320px-The_Road_to_Reality.jpg
 
KENZY
Kwanza ninaposema kafiri simaanishi ni adui yangu mimi ila namaanisha ni mtu anaenda kinyume na maamrisho ya mungu.
Kwa hiyo mimi ninaamini wazi wakiristo ni makafiri.

Pili mungu hampi mtu adhabu mpaka amuulize suala hili jee hawakukujia minabii na mitume kukuonya ili utake msamaha kwangu na nikusamehe.Kwa hiyo mungu ana muadhibu mtu kwa kujifanya kwake anajua sana zaidi kuliko huyo mungu.

hlf kuna haja gani ya kumbakiza shetani wanapoishi wapendwa wako huku ukijiita wewe ni mfalme wa amani ama wewe ni tumaini la wanyonge..?
Mimi naamini hivi mungu ni tumaini la wanaomuamini na si tumaini la wanyonge wasiomuamini,halafu pia mungu mwenyewe anasema hivi kila jambo jema linatokana yeye na jambo baya linatokana na nafsi ya mtu mwenyewe kwa maana hiyo mola wangu mimi ni mwema na hana mabaya.

Ahadi ya mungu ni ya kweli hivyo aliposema kila Kiumbe atamuonesha nija njema ili mwenyewe aifuate kwa hiari pasi na kulazimishwa basi atatimiza hivyo hivyo milele. Hivyo mungu hakuwa na haja ya kuvunja ahadi ya kumteketeza shetani bali alimuacha kwa sababu yeye amechagua njia yake anayotaka. hivyo atapata hukumu ya hicho alichokifuata na yule atakae mfuata shetani nae atakuwa katika njia hiyo hiyo .

na kwa mapenzi yake mungu hakumuacha mja wake bali alimletea mitume na kitabu ili kuwaongoza kwake kazi ya mitume si kulazimisha ni kutahadharisha watakaofuata ndio wamefuata na wasiofuata basi ndio wamechagua hivyo.

Una fantasy nyingi mjomba ,Duh.

Well ,umeuliza kama kuna andiko lolote linalo zungumzia Allah anaeneza chuki.

Nini maana ya chuki?

Je nikikupa ayah zaidi ya 20 ndani ya Quran zinazozungumzia chuki na violence among people ,Utaukana uislam ?

Pia,umesema Mungu hakuadhibu kama amekuletea mitume,Umeongea vizuri Mjomba ,

wewe umeletewa mtume gani? Kuna mtume yeyote ambae umeletewa wewe ?

Usiniambie kuwa Muhammad ni mtume wako.

Unaielewa Quran Mubashara ikisomwa au wewe ni miongoni mwa wale ambao wamekariri lakini hawajui walichokariri kina maanisha nini .?

Halafu definition yako ya Kafiri sio sahihi.Unatakiwa kujifunza zaidi mjomba bila Fantasy .
 
Una fantasy nyingi mjomba ,Duh.

Well ,umeuliza kama kuna andiko lolote linalo zungumzia Allah anaeneza chuki.

Nini maana ya chuki?

Je nikikupa ayah zaidi ya 20 ndani ya Quran zinazozungumzia chuki na violence among people ,Utaukana uislam ?

Pia,umesema Mungu hakuadhibu kama amekuletea mitume,Umeongea vizuri Mjomba ,

wewe umeletewa mtume gani? Kuna mtume yeyote ambae umeletewa wewe ?Usiniambie kuwa Muhammad ni mtume wako.

Unaielewa Quran Mubashara ikisomwa au wewe ni miongoni mwa wale ambao wamekariri lakini hawajui walichokariri kina maanisha nini .?

Halafu definition yako ya Kafiri sio sahihi.Unatakiwa kujifunza zaidi mjomba bila Fantasy .

Kwanza ningelipenda ufahamu , mola wangu ameniepusha mbali na ujinga. Hivyo mimi sio atheist.

Kwa imani ninaamini hivi Mungu hawapendi makafiri na anawapenda wale wote wanaofuata amri zake.
Hiyvo kama hizo aya mpaka zizungumziye chuki kwa wanaokwenda kinyume na yeye mungu.
Halafu mungu anasema katika quran
"((Wala msisengenyane nyinyi kwa nyinyi. Je! Yupo katika nyinyi anayependa kuila nyama ya nduguye aliyekufa? Mnalichukia hilo! Na mcheni Allaah. Hakika Allaah ni Mwenye kupokea toba, Mwenye kurehemu)) [Al-Hujuraat: 12]"

"((Wala msitukanane kwa kabila wala msiitane kwa majina ya kejeli. Ni uovu kutumia jina baya baada ya kwisha amini. Na wasiotubu, hao ndio wenye kudhulumu)) [Al-Hujuraat: 11]"

Hivo kwa Muislamu ni haramu kumchukia mwislamu mwenziwe.

2.wewe umeletewa mtume gani? Kuna mtume yeyote ambae umeletewa wewe ?Usiniambie kuwa Muhammad ni mtume wako.

Kwa vile mimi ni muislamu na kitabu changu ni quran basi nitaamini yaliomo humo wala sitopinga kwa vile Allah amesema Muhammad ni mtume wake basi mimi na mafuata huyo kwasabu Allah ametaka tumfuate.

Mungu anasema kwenye quran.

"Muhammad ni mtume wa mwenyezi mungu.Na walio pamoja nae ni wenye nyoyo thabit mbele ya makafiri na wenye kuhurumiana wao kwa wao.Utawaona wakiinama kwa kurukuu na kusujudu kwa pamoja,wakitafuta fadhila za mwenyezi mungu na radhi yake.Alama zao zi katika nyuso zao kwa athari ya kusujudu.Huu ndio mfanoo wao katika taurat na katika injili.Na mfano wao katika injili kuwa wao ni kama mmea ulioota matawi yake,kisha matawi hayo ukautia nguvu ukasimama sawasawa katika kigogo chake,ukawafurahisha walioupanda ili awakasirishe makafiri kwa ajili yao.Mwenyezi Mungu amewaahidi walioamini na kutenda mema katika wao msamaha na ujira mkubwa".
Quran 48:29.

Itakuwaje ni mkane Muhammad kuwa si mtume?
 
nakushauri kaa jenga familia yako ...Njia za Mungu hazichunguziki sana sana unajitengenezea mazingira ya yeye kuanza kukuchunguza na kukupa majaribu kama Ayubu !!! Tulia Fanya Maisha ...Uliza tu Baba yako mzazi katengenezwa nanani !! Usiende mbali kwa Mungu , wakati hujajua baba yako alitengenezwa nanani !!.
 
Natumai hujasoma vizuri post yangu.Hemu isome full usisome heading tu.
 
Back
Top Bottom