Mungu lazima aabudiwe, wakati wa shida au raha

Mungu lazima aabudiwe, wakati wa shida au raha

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2016
Posts
15,923
Reaction score
40,246
Habari wana JF

Kwa wale tunaoamini Mungu, ni lazima tumuabudu bila kujali tuko kwenye wakati au hali gani, yaani shida au raha. Ikumbukwe kwamba maisha ni zawadi kutoka kwa Mungu hivyo basi tumrudishie yeye sifa na utukufu.

Kwa mantiki hiyo, nakubaliana na Mh. Rais, si vyema kufunga misikiti na makanisa kwa hofu ya uhai ambao anautoa huyo anayeenda kuabudiwa kwenye hizo nyumba za ibada. Aidha, taadhari lazima zichukuliwe kama inavyoshauriwa ikiwa ni pamoja na kuvaa barakoa na recommended social distance.

Kama wewe na wenzako mnabisha hili, nendeni polisi mkaombe kibali cha kuandamana
 
"Mungu ni mwema kila wakatiii" ni sawa na kiu ya maji ukihisi unapiga glass mojaa unatulia.....so every second, minute and hour make your own prayer.
 
Kama Mungu ni Roho, na yupo popote pale, kwanini iwe shida kumwabudu huyo Mungu nyumbani kwako na familia yako?

Kumbuka ibada ya kweli huanzia nyumbani na humalizikia nyumbani.
 
Ni wapi Mungu alisema ukitaka kumuabudu ni lazima uende kwenye majengo ya kidini?
Kwa hivyo alipopendezwa kujengewa hekalu na mfalme Suleimani ilikua ni kwajili ya kupigia selfie?
 
Sisi MATAGA tunamwabudu Magufuli na Makonda watoa TEUZI na MAPESA na wajenga MISIKITI.

Mungu hajibu maombi.
 
Back
Top Bottom