Mungu mkubwa, hatimaye nimepata kazi ya kuchoma chipsi

Mungu mkubwa, hatimaye nimepata kazi ya kuchoma chipsi

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Leo nimepata kazi Kama utani nilienda kunywa pombe kwenye grocery fulani mtaani jamaa mwenye grocery Ni mwanajeshi mstaafu alikuwa na yeye amelewa akasema haiwezekani grocery ikose chips tunafanyaje me nikaropoka boss me nipo kijana wako kwanini uteseke akasema Safi Sana subiri nikachukue hela ukanunue viazi na nyama kwa ajili ya mishikaki.

Kazi umeshapata nimefurahi kinoma hasa kwenye mishikaki hapo nitajiongeza mpaka nitoke shavu asee hajaniambia shingapi atanilipa ila kikubwa jueni tu kazi nimepata baada ya kukaa kitaa kwa kuunga unga Sasa hv nta enjoy halafu mazingira ya kazi mazuri maana nikifika tu asubuhi natoa Kwanza wenge na kinusu.

JPEG_20210711_133325_3816169436870106737.jpg
 
Hongera ndugu, mwenzako hadi muda huu bado nimelala, nikiamka nianze kuilalamikia serikali.

Sent using Jamii Forums mobile app

Albert Einstein aliwahi kusema siku teknolojia ikipamba moto duniani,wajinga wataongezeka.Wakati ukiilalamikia serikali ungetumia changamoto kuibadili iwe fursa.Amini hili chakula cha bure hulemaza akili.jitahidi usipishane na akili zako vinginevyo utasota.ukiendelea kuilalamikia serikali kila siku muda nao unaenda.[emoji120][emoji120]
 
Hongera sana mkuu. Lakini saa usifikirie kujenga shavu sasa hivi zungumzeni kuhusu ujira wako maana wazee hao hawachelewi kukulipa kula
 
Hongera mkuu, nasikia hakuna mtu mwenye confidence kama mkaanga chipsi yaani unawezakuta amezungukwa na nyomi la watu wananjaa kali halafu ndio anamenya viazi anawaambia dakika sifuri tu nakuletea chipsi yai, akigeuka huku dakika moja tu inatoka sasa hivi na ukwaju, kufumba na kufumbua kawaweka watu nusu saa nzima🤣
 
Back
Top Bottom