Mungu Muumbaji ndio msaada wa hakika tupopatwa na shida za maisha

Mungu Muumbaji ndio msaada wa hakika tupopatwa na shida za maisha

Msolo

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2008
Posts
3,832
Reaction score
5,309
Fikiria Mungu kama mtengenezaji (manufacturer) wa kifaa cha kipekee sana, kifaa ambacho hakina duplicate, hakina serial number nyingine, na hakina manual inayoweza kuelezea kila undani. Hicho kifaa ni mwanadamu.

Kila mtengenezaji wa kifaa anajua muundo wa ndani, waya gani unaenda wapi, program gani inakiendesha, na sehemu gani ikiharibika inahitaji kufanywa nini.

Sasa, kifaa hiki (sisi binadamu) kikianza kuleta shida(malfunction) iwe ni kiafya, kiakili, kihisia, hata kiroho, mtu pekee anayejua kwa hakika nini cha kufanya ni yule aliyekitengeneza.

Madaktari wanaweza kusaidia, dawa zinaweza kutuliza, ushauri unaweza kutia nguvu, lakini repair ya kweli ya ndani kabisa inajulikana na Muumba tu.(The Creator)
Yeye ndiye ana access ya mchoro halisi(original blueprint)

Ndiyo maana tunapopata shida ya mwili, akili au roho, kuna mantiki sana kusema tunarudi kwa Mungu kama mtengenezaji wetu.

Si kwa sababu hatuthamini msaada wa kibinadamu, bali kwa sababu tunajua chanzo cha uhai wetu kinatoka kwake, na ufumbuzi wa kina uko kwake.

“Kwa maana wewe uliunda viungo vyangu; uliniunda tumboni mwa mama yangu.” Zaburi 139:13
 
Back
Top Bottom