Kuna watu niliwahi kuwambia Mungu na Shetani ni marafiki sana. Wakaniona kama nakufuru.Mtu akiteseka wanasema ni mapenzi ya Mungu, Ina maana ana uhusiano na shetani. Mimi ninaona Mungu na shetani ni vitu viwili vinavyofanya kazi pamoja. Ni sawa na mwanga na Giza. Wakati wa mchana mimea inatumia jua kutengeneza ule ukijani wake na usiku mimea inatoa hewa kwa binadamu.
Sisi ndio tunawagombanisha ila wao wanaelewana vizuri.
Rejea tukioa la Ayoub. Pia wakati Babeli inaenda kuvamia Wayahudi ktk kitabu cha Yeremia Mungu akasema nilimtumia Mtumishi wangu Nebukadineza awatie mikononi mwake........
Inawezekana vipi Shetani apigane vita Mbinguni dhidi ya Mungu?
Na bado akafanikiwa kushawishi 1/3 ya malaika zake?
Inawezekana vipi Shetani aliye na nguvu kiasi hiki aletwe duniani kupamna na sisi viumbe dhaifu tulioumbwa na udongo na utegemee ushindi??
Why Mungu asingemalizana na shetani kabisa? Sasa mlolongo wa matukio ukaanza mara namtuma Yesu aje kuwakomboa, mara chinjeni kafara toeni sadaka ziwasafishe dhambi.....huu mzunguko wa nini wakati anatakiwa kufyekelea mbali shetani?
Duniani tunakadiriwa kuwa 7bn. Watakaoenda mbinguni hawafiki 1mIlioni.
Iweje 6bn inapotea hivi hivi sababu ya shetani mmoja?