Mungu ndiye shetani(?)

Kuna watu niliwahi kuwambia Mungu na Shetani ni marafiki sana. Wakaniona kama nakufuru.

Sisi ndio tunawagombanisha ila wao wanaelewana vizuri.

Rejea tukioa la Ayoub. Pia wakati Babeli inaenda kuvamia Wayahudi ktk kitabu cha Yeremia Mungu akasema nilimtumia Mtumishi wangu Nebukadineza awatie mikononi mwake........

Inawezekana vipi Shetani apigane vita Mbinguni dhidi ya Mungu?

Na bado akafanikiwa kushawishi 1/3 ya malaika zake?

Inawezekana vipi Shetani aliye na nguvu kiasi hiki aletwe duniani kupamna na sisi viumbe dhaifu tulioumbwa na udongo na utegemee ushindi??

Why Mungu asingemalizana na shetani kabisa? Sasa mlolongo wa matukio ukaanza mara namtuma Yesu aje kuwakomboa, mara chinjeni kafara toeni sadaka ziwasafishe dhambi.....huu mzunguko wa nini wakati anatakiwa kufyekelea mbali shetani?
Duniani tunakadiriwa kuwa 7bn. Watakaoenda mbinguni hawafiki 1mIlioni.

Iweje 6bn inapotea hivi hivi sababu ya shetani mmoja?
 
Nikisoma historia ya ukoloni baran Africa,
Hasa role ya wamisionari na waarabu ktk kutuletea huu ukoloni.

Nakosa kabisa imanj na hizi dini zilizokuja na meli Islamic& Christianity [emoji22]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata ukifa kwa kupigwa risasi,
Watasema Ni mapenzi ya mungu[emoji22]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Palikuwa na darweshi mmoja wa tarika ya uzururaji (kalanda) aliyetembea jangwani Kwa muda wa siku kadhaa, akiwa mwenye njaa na kiu nusura ya kufa alifika Hadi katika mji mmoja na kuanza kuparamia vyakula na maji...wenyeji walipomwona walimkamata na kumpiga sana Kwa sababu ilikuwa ni kipindi cha ramadhani...alipopata ahueni yule darweshi alisema kuwa kwa wakati ule chakula na maji vilikuwa ndio ibada kubwa kwake ila waliompiga walifanya hivyo Kwa sababu maana ya kufunga haikujulikana kwao...

Inawezekana na sisi, fumbo la "Mungu na Shetani" hatulijui au hatutaki kulijua...
 
Una matatizo gani kwanza
 
Zilongwa mbali,, zitendwa mbali, hapa hatuko kujadili Iran, Quran, wala kadhi. Mleta uzi ni mgala mwenzenu na amesoma biblia na kukiona hicho alichokiona, suala la kusema biblia aisomwi kama gazeti usiniambie mimi bali mwambie huyo mgala mwenzio kwa kuwa yeye ndio alieleta uzi,, shida yangu mimi kwako ni kuingiza Quran, iran, kadhi, sijui albadir kwenye uzi ambao hata hivyo vitu havihusika, na ukitaka kujadili hayo fungulia uzi wako kama alivyofanya mleta uzi,, ila kwa leo jadiliana na mgala mwenzio juu ya kile alichokiona kwenye biblia.
 
Hata ukifa kwa kupigwa risasi,
Watasema Ni mapenzi ya mungu[emoji22]

Sent using Jamii Forums mobile app
Elimu yako na uelewa wako juu yako ya Mungu uko limited na sio wewe ni tatizo la watu wengi, mwanadamu kupitia adamu alimkataa Mungu na mfumo wake wa maisha ndo maana wewe na wenzako mnatukana Mungu na hawafanyi chochote sababu Mungu hawez shindana na binadamu ambaye atakufa
 
Huwez mpangia mtu acomment kama unavyotaka wewe na je kama mleta uzi ni muislamu
 
Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake. Yohana 14:23

Maisha yetu yana shughuli nyingi na vizuizi vingi.Ni rahisi sana kushikika katika shughuli, wasiwasi na majukumu hadi tukasahau kile kilicho cha muhimu zaidi.

Kuna hadithi fupi ya kupendeza mwishoni mwa Luka 2 wakati Maria na Yusufu walimpeleka Yesu Yerusalemu kwa pasaka akiwa umri wa miaka 12. Baada ya sherehe walianza safari kurudi nyumbani wakidhani kwamba yuko nao.

Nami najiuliza, ni mara ngapi tunadhani Mungu yuko nasi ilhali tumeenenda katika shughuli zetu wenyewe.

Sasa jambo la kushangaza ni hili; Maria na Yusufu walikuwa wamesafiri siku nzima kutambua kuwa Yesu hakuwa nao na iliwachukua siku tatu kumpata. Siku tatu! Sasa ujumbe hapa ni huu; ni rahisi sana kwetu kuupoteza uwepo spesheli wa Mungu kuliko kuupata tena tunapoupoteza.

Inafaa tuwe waangalifu kusalia katika uwepo wa Mungu. Tunapofanya hivyo, Mungu hupata maskani mioyoni mwetu.

Hii huanza kwa kuwa watiifu kwa neno la Mungu. Njia moja ya kuonyesha ukomavu wa kiroho ni kuachana na tabia ambazo hazimpendezi Mungu, hii huonyesha kwamba unayajali yale anayofikiria.

Hii inamaanisha unakuwa mkarimu kwa watu, unajifundisha kusamehe, unaachana na migogoro na unaishi kwa amani. Tunapojifunza kuwa makini na maneno yaetu, kumshukuru Mungu na kuwainua wengine, tutazidi kuwa katika uwepo wa Mungu siku nzima.

Ombi La Kuanza Siku
Baba, asante kwa kufanya moyo wangu makao yako. Ninahitaji uwepo wako leo. Nisaidie nikuheshimu kwa mawazo na maneno yangu, na kuwa wa Baraka kwa wale walio karibu nami.
 
Badala ujibu hoja za mleta mada unahangaika hangaika tu..
Unasema Biblia haisomwi kama gazeti halafu wewe ulichoandika ni EMPTY SET.
 
Huwez mpangia mtu acomment kama unavyotaka wewe na je kama mleta uzi ni muislamu
Hata kama awe muislam au mkiristo kwa kuwa ameleta hoja kwa vifungu vya mistari ya kitabu kitakatifu ajibiwe kwa hoja za vifungu pia..
Porojo za sijui huwezi mpangia mtu accoment nini inaonyesha kichwa kimebebe uzito gani wa kichwa.
 
Wafia dini kawaida hawajui kujibu hoja, ni huwa wanakuja na tu vitisho twao walivyokaririshwa kutoka kwenye vitabu vya wakoloni....
 
Umekufuru.Adhabu yako ni kufanya toba/tubu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…