Nakimbizwa
Senior Member
- Jun 19, 2023
- 154
- 302
Wasalaam allaykum na Bwana Yesu asifiwe ndugu zangu watanzania wenzangu wa dini zote. Twende moja kwa moja kwenye mada.
Dini zote mbili za Tanzania wanaamini kuwa Mungu ni mmoja.
Hii ni kweli kwasababu tunatakiwa tujue hizi sheria za ulimwengu kuwa
1. kila kitu kwenye huu ulimwengu ni kitu kimoja. Na pia
2. Kila kitu kwenye huu ulimwengu kipo interconnected na chenzake.
Mosi, Kila kitu kwenye huu ulimwenguni kitu kimoja, kwasababu:
Tukimenya maganda ya kila kitu, tukachungulia ndani kuangalia kimetengenezwa na nini yani atoms, molecules, neutrons, electrons, mpaka kwenye field ya kila kitu, tunagundua kuwa kila kitu (kuanzia nyota, milima, watu na maembe) kwenye huu ulimwengu kimetengenezwa kwa kutumia material zile zile. Sasa kama kila kitu kime tengenezwa kwa kutumia material zile zile, huu ulimwengu basi kumbe sio mkusanyiko wa vitu mbali mbali vyenye sifa tofauti. Bali ulimwengu Wote ni kitu kimoja kinachojimanifest katika mifumo/maumbo tofauti tofauti.
Albert Einstein kupitia theory ya relativity alituonyesha kuwa energy na mass ni kitu kile kile. Kuwa ukicompress energy unapata mass, na ukiexpand mass unapata energy. Time na space pia zote ni pande mbili za shilingi moja. Zote zimeunganika kwenye matter and energy. Kwahyo ulimwengu wote kisayansi, ni kitu kimoja.
Kwa msingi huo binadamu wote, au wewe hapo unayesoma, unayejijua kuwa wewe ni wewe, wewe pia sio sehemu ya ulimwengu, wala wewe haukuja ulimwenguni.
Wewe sio sehemu (part) ya ulimwengu kwa sababu ulimwengu hauna sehemu (parts). Ulimwengu Wote ni kitu kimoja. Ni sawa na namba saba, Je, namba saba ina sehemu ngapi? Tunatofautisha vitu ulimwenguni sio kwasababu viko tofauti lakini ni kwasababu ya ufi yu wetu wa uelewa na pia kwaajili ya lugha na mawasiliano.
Kwa hiyo, ulimwengu wote ni kitu kimoja. Na sisi sio sehemu ya ulimwengu, bali sisi ni ulimwengu. Na kila kitu ni kitu kimoja, ndiyo maana watu wadini mbalimbali, huita kitu hiki kwa majina tofauti tofauti. Wengine huita Mungu, wengine huita brahman, wengine huita dao, lakini vyote ni kitu kimoja.
Mungu ni omnipotent, omniscient omnipresent, yani yupo kila mahali, anaweza kila kitu na Anajua kila kitu. Hili linawezekana kwasababu yeye ni kila kitu. Bila yeye kuwa kila kitu hawezi kuwa kila mahali au kujua kila kitu au kuweza kila kitu.
Maana kwamfano kama mguu wangu sio sehemu yake basi hayuko mguuni mwangu.
Tunaposema mapenzi yake yatimizwe hapa duniani kama mbinguni. Ni kwamba kila siku mapenzi yake lazima yatimizwe maana kila kitu kinafanya mapenzi yake maana yeye ni kila kitu au kiusahihi tuseme yeye ni kitu kimoja kama tulivyoona.
Pili, Kila kitu kipo interconnected na kinategemeana kwasababu vyote ni kitu kimoja.
Bila jua hakuna sayari, bila sayari na jua hakuna maisha duniani.
Bila maji na oxygen duniani kusingekuwa na maisha.
Bila maisha aina nyengine kama mimea, wanyama wengine hata sisi binadamu tusingekuwepo.
Bila uwepo wa binadamu wenzako hata wewe pia usingekuwepo, maana uwepo wako hapa duniani unategemeana na uwepo wa binadamu wenzako wengine kama boss wako, wateja zako, ndugu zako, majirani zako, walimu wako, viongozi wako, askari/trafiki anayekuongoza barabarani, wakulima wanaokulimia, wasafirishaji wanaokusafirisha wewe na mahitaji yako nk. Na kadhalika.
Bila nyuki hakuna maua na bila maua hakuna nyuki, hivyo nyuki na ua sio vitu viwili tofauti bali ni sehemu ya kitu kimoja, au kiumakini zaidi tunaweza kusema nyuki na ua ni kitu kimoja.
Kama ambavyo hydrogen na oxygen vikiungana hutenegeneza maji ya kwenye chupa tunayokunywa, mvuke unaoleta mvua, bahari inayotunza viumbe mbalimbali na hata maji yanayochukua 70% ya miili yetu.
Vivyo hivyo Wewe na mimi na watu wote duniani na vitu vyote ulimwenguni ni kitu kimoja kwasababu vyote vina sifa moja. Vimetokea sehemu moja, vipo sehemu moja, ni kitu kimoja.
Kuhusu jina la hiko kitu, kiukweli hakina jina maana kuna tofauti kati ya jina la kitu na kitu chenyewe kiuhalisia.
Majina ni uwakilishi tu wa vitu katika symbols au lugha zetu homo sapiens ili tuwasiliane, lakini uhusiano wa jina la kitu na kitu chenye hilo jina ni kama Ramani ya nyumba na nyumba yenyewe, au kama menu ya chakula na chakula chenyewe, au kama pesa na utajiri wenyewe.
Huwezi kuishi kwenye ramani au kula menu ya chakula au kutumia pesa za makaratasi ukipotea mwenyewe jangwani.
Lakini kwasababu tu za kurahisisha kuwasiliana binadamu wamekipa hiki kitu kimoja jina, wengine wameita Mungu wengine Brahman, wengine Tao nk. Lakini yote kwa yote Mungu ni mmoja.
Alamsiki.