dalalitz
JF-Expert Member
- Sep 6, 2013
- 3,423
- 1,987
Anaitwa EMMA KOK, Binti wa miaka 16 tu. Usipoambiwa anayoyapitia Kiafya utadhani ni binti asiekuwa na shida yoyote kimuonekano.
Hatahivyo uhalisia ni kuwa binti huyu anao mzigo mkubwa, changamoto anayoipitia. Inasikitisha, inahuzunisha lakini ukiisoma Historia yake na anayoyafanya pasi na shaka kuna mahali utatabasamu na pengine utabubujikwa na chozi lenye hisia mchanganyiko.
Maradhi yake Emma ni aghalabu kusikia mtu anaugua kama si kuwa hata wewe pengine ama wengi wetu ndio tunajua uwepo wake kupia kwake yeye.
Kifupi Emma 'ame-paralyze' Tumbo lake. Yaani Tumbo halifanyi kazi kama ambavyo ingetarajuwa kwa Mwanadamu yeyote Hai. Huu ni Ulemavu wa kuogofya na hatari. Sasa, anaishije? Mwingine anaweza kuuliza,
Ni kuwa Emma anatumia Mipira maalum kupitisha chakula mwilini mwake (Si kula kupitia mdomo)
Emma ni Mzaliwa wa 'Udachi' pengine ashukuru, Mbinu na Teknolojia za Matibabu kwa wenzetu pengine zinamsaidia na zimemuokoa maana sipati picha angekuwa kazaliwa Nchi zetu 'Bundesliga' sijui ingekuwaje?
Wanasema Mungu hamtupi Mja wake na hata akikunyima hakunyimi vyote. Emma amejaaliwa kipaji kikubwa cha Uimbaji Muziki. Mwaka 2021 aliibuka kuwa mshindi katika mashindano ya vipaji kwa watoto kule Udachi.
Baada ya kupenya tu hapo akajitoa 'sadaka' na kusema atapigana kwa kutumia kipaji chake kutafuta Pesa ili kusaidia tafiti za Kutibu matatizo ya aina anayoyapitia kwa wengine. Kuanzia hapa na akiwa umri wake huo mdogo ameanza kuingiza Pesa na anadai hatochoka kupambana ili ndoto yake hiyo itimie.
Mwaka jana Disemba kafanya 'Cover' ya Nguli wa Ufaransa mwanadada Barbara Pravis wimbo Mkubwa sana unaoitwa 'Voila' alichokifanya humo Emma si tu alidhihirisha kipaji chake pekee,bali aliwaliza watu 'live' na kuanzia hapo ni kama nyota yake inazidi tu kupaa na kujiengea Heshma zaidi angali mdogo.
Emma Kok namuona akiwa mbali sana.
Pitia hapa umuone:
View: https://www.youtube.com/watch?v=KdIhq1tb8Co
Nawasilisha.