Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Kama yasemwayo kuhusu mabeberu kutaka kusaidia kufanikisha mabadiliko yana ukweli wowote,binafsi naunga mkono kwasababu zifuatazo:
Wizi,rushwa ufisadi na kulindana
Kikundi hiki cha watu ndio kimetawala hii nchi tangu uhuru na baadhi yao wana tuhuma nyingi za wizi,ufisadi na ubadhirifu wa kutisha mambo yaliyopelekea Taifa hili na watu wake kuwa masikini huku wao na familia zao wakiineemeka na kibaya zaidi wanalindana.
Ukijiopndoa katika kikundi hiki, ndio watajidai kukuishughulikia ila ukiwa ndani hawakugusi na wanakulinda kwa gharama yoyote ile(unafiki)!
Wengi katika kikundi hiki wanastahili kuwa jela au mahabusu ila wako uraiani na wengine bado wako madarakani.
Kwasababu hizo,nitaunga mkono juhudi zozote halali za kukiondoa kikundi hiki cha watu wachache ili Taifa lisonge mbele na wao kama watuhumiwa wafikishwe katika vyombo vya sheria.
Mauji,ukatili na mateso kwa wapinzani wao
Tangu uhuru,kikundi hiki kinatuhumiwa kwa mauji,unyanyasaji,utesaji na sasa hata utekaji wa watu wasiowaunga mkono(wanaowakosoa).
Mambo haya ni miongoni mwa mambo yanayonifanya nikichukie kikundi hiki tangu nilipokuwa mtu mzima mpaka leo hii na bahati mbaya kikundi kilichopo sasa ndio kinatuhumiwa kuendeleza ufedhuli huu kwa kiwango cha juu sana.
Katika mazingira haya,awe beberu,awe shetani,nitamuunga mkono kama azima yake ni kufutilia mbali kikundi hiki kitoke ofisini waingie wengine watakaoheshimu utu wa watu wengine
Dhuluma katika chaguzi na kupora haki za wengine
Kwa miaka mingi kikundi hiki cha watu kinachopokezana kijiti cha uongozi kimetuhumiwa kupora haki za wananchi kuchagua na kuweka madarakani viongozi wanaowataka kwa kutumia mabavu na mbinu nyingine chafu.
Kikundi kilichpo sasa ndio kabisa kimepania hata kuua mfumo wa vyama vingi kwa masilahi yao binafsi hivyo leo hii akitokea mtu wa kutusaidia kukiondoa hakika nitamuombea kwa Mungu afanikiwe awe beberu awe shetani.
Wao wachache wanaishi kwa raha huku mamilioni wakiishi katika rundo la umasikini
Kutokana na uongozi wao mbobu kwa miaka mingi na kuliibia Taifa kwa kila hali kama wanavyotumiwa na kutuhumiana wenyewe kwa wenyewe(wanapogeukana),wamesababishi umasikini na mateso kwa watu wengi na hata kwa watoto walioko matumboni na hata ambao hawataraji kuzaliwa leo wala kesho kwani nao wao siku wakizaliwa, watarithi umasikini huu uliosababishwa na kikundu hiki cha watu wachache hivyo kiondoke tu ofisini(tumekichoka).
Hayo ni machache miongoni mwa mengi yanayonifanya nisikipende kikundi hiki cha watu wachache wanaokula mema ya nchi huku walio wengi wakiteseka na hata kufa kwa kukosa huduma za msingi.
Walaniwe wao na vizazi vyao.