February Makamba
JF-Expert Member
- Jan 31, 2020
- 2,151
- 2,983
Sasa, wakuu, hebu leo naomba tuzungumzie ksidogo kuhusu dini.
Regardless ya definition yako ya Mungu au uchaguzi wako wa Mungu yupi wa ukweli, au hata kama huamini Mungu yupo. Bado haipingi uwepo wa dini Dunuani. Dini zinaexist na kila kinachoexist, regardless ni kizuri au kibaya (kwasababu hizo ni subjective phenomena) kina purpose ya kuwepo. Dini kwa definition yangu ya kichwani ni mfumo au misingi ya mahusiano kati ya mwanadamu na Mungu.
Tunapojaribu kuielewa dini, ni muhimu kuzitazama sifa zake, historia yake, na aina mbalimbali za imani na desturi zinazojumuishwa ndani yake. Tukifanya hivyo, tunaweza kuona mtindo/pattern fulani inajitokeza—uelekeo fulani wa mbele au maendeleo katika jinsi wanadamu wanavyohusiana na Mungu.
Tukianza mwanzoni kabisa, na dini za kwanza za kale zilizorekodiwa, tunaona kwamba binadamu wa kale walijikita kwenye kumwabudu/Kumtii/kumtumikia/Kumuogopa Mungu—Mungu ambaye walimwona kama muumba na mtawala wa ulimwengu. Katika dini hizi za kale, kulikuwa na mpangilio wa ngazi kali(hierarchy): binadamu walikuwa ni watumwa wa huyu mungu, na jukumu lao kuu lilikuwa kumwabudu na kumtumikia. Mtazamo huu unaonekana katika dini za zamani za Uyahudi, Uhindu wa awali, na baadaye, Uislamu. (ingawa uislam ulikuja baadaye.
Kwa namna fulani, Uislamu ulihuisha tena aina ya kale ya Uyahudi (agano la kale)—dini ya Daudi,Musa na Sulemani, ambayo ilisisitiza utiifu na unyenyekevu kwa Mungu kama mtawala/Master/Mfalme wetu. Ninapenda kuiita hatua hii “Hatua ya Kwanza ya dini.” Hatua hii ni pale binadamu walipoanza kuchunguza fahamu zao kuijua asili ya ulimwengu, lakini hatua yao ya kwanza ilikuwa kumwabudu na kumuogopa Muumba.
Kisha tunaingia kwenye kile ninachokiita "enzi ya pili ya dini"/second floor, ambayo inawakilishwa na Ukristo na Ubudha. Katika Ukristo, tuna jamaa anaitwa Yesu, anayesema, “Ndiyo, kuna Mungu, mwenye nguvu zote na anayekuwepo kila mahali, aliyeumba kila kitu, lakini pia huyo anatupenda. Sisi sio watumwa wake tu au vibaraka. Sisi ni sehemu pia ya uumbaji wake.” sisi pia ni wa muhimu kwake kama yeye alivyo muhimu kwetu.
Hii ilikuwa mabadiliko makubwa kwa sababu, katika dini za awali, wanadamu hawakuwa kitu mbele ya muumba huyu. Dini nyingi za kale hazikuweka mkazo kwenye maisha ya baadae; zilijikita zaidi kwenye ibada hapa duniani na sasa.
Lakini na Ukristo na Ubudha, wazo jipya likaja—wazo la kupaa juu ya mipaka ya kibinadamu. Ujumbe ulikuwa: kwa sababu muumba anatupenda, tunaweza kuvuka mipaka ya udhaifu wa kibinadamu. Katika Ukristo, hii inamaanisha kwamba tukiamini, tunaweza kuungana na Mungu baada ya kifo. Katika Ubudha, ni kupitia mwanga wa kiroho (enlightenment) tunaweza kushinda mateso. Hatua hii ya pili ya dini inatufanya tuwe na usawa na Mungu kwa namna fulani.
Yesu alisema, “Mimi ni Mungu, na ukiniamini, mimi na Baba yangu tutakuja kuKaa ndani yako.” Kimsingi, alikuwa anasema kwamba kwa kufuata mafundisho yake, tunakuwa wamoja wa kimungu. Wabudha pia huamini Kuwa Mungu/ulimwengu sio mkubwa kuliko wao kwasababu huwezi kusema Bahari ni kubwa kuliko maji maana bila maji hakuna bahari.
Mwisho, hebu tuongelee kuhusu hatua ya tatu ya dini(third floor), ambayo ndimo nilipo mimi. Hii ni hatua ya umiliki wa ulimwengu. Katika hatua hii, hujioni tu kama sehemu ya uumbaji, bali kama bwana wa uumbaji. Watu wachache sana wanafika hatua hii, lakini wale wanaofika, wanatambua kwamba wao si sehemu tu ya ulimwengu—bali wana uwezo wa kuudhibiti. Wanatambua kwamba Mungu si kitu tofauti; bali, Mungu ni chombo kilichopo kwa ajili yako. Wanatambua kuwa Ulimwengu, na kila kitu kilichomo, kimeumbwa kwa ajili ya kukuhudumia. Kipo kwa ajili ya uwepo wako, kila kitu kuanzia existence yako,ukuaji wako, na conscious experience zako zote zimewezeshwa na ulimwengu/Mungu.
Unapofikia kiwango hiki, hauabudu tena Mungu; badala yake, unamtumia Mungu kuuelekeza ulimwengu kama utakavyo. Secret societies kama illuminatis wanajua siri hizi na hwataki watu wengine wazijue. Kwamba ulimwengu/Mungu unaweza kumcommand/kuucomand.
Infact tayari unafanya hivyo. Kwasababu hata kwa kupumua tu unatumia hewa ambayo Mungu alifanya kazi kukutengenezea, hivyo Jua, Dunia, Hewa, MaJi, viumbe, Miti, Wanyama hata binadamu wamewekwa na Mungu/ulimwengu kwa ajili yako. Kila kitu kipo ili kusapoti uwepo wako wewe, maana bila kila kitu hata wewe usingekuwepo.
Kwa hiyo, kwa kusamaraizi; hatua ya kwanza ya dini ni kuwa mtumwa wa Mungu, hatua ya pili ni kuwa sawa na Mungu, na hatua ya tatu ni kummiliki Mungu. Ni wachache wanaofikia kiwango hiki, lakini mara unapofika hatua hii unauona ulimwengu kutoka mtazamo wa juu kabisa, na huwezi kuitumia nguvu hii vibaya maana utakuwa na sense ya guilt kwa kuwa huwezi kumlaumu Mtu/Mungu/Shetani kwasqbabu unajijua wewe ndo muweza wa yote. Lazima utakuwa na huruma kwakuwa una uwezo wa kuleta mabadiliko. Utakuwa umepanda ghorofa la tatu la dini—njoo hapa juu, huku mandhari ni nzuri.