Samson Ernest
JF-Expert Member
- Aug 28, 2014
- 1,237
- 1,744
Yer 23:23 SUV
[23] Mimi ni Mungu aliye karibu, asema BWANA, mimi si Mungu aliye mbali.
Zamani katika agano la kale Mungu alionekana yupo juu mbinguni, na mara nyingi alizungumza na watu wake kupitia kwa manabii.
Jambo hili linaweza likawa ndani ya baadhi ya watu, wanaweza kufikiri Mungu yupo mbali sana, maombi yao wanayoomba hayawezi kusikiwa.
Tunapaswa kuelewa Mungu wetu yupo karibu mno kupitia Yesu Kristo, huyu Yesu ni Neno, na huyu Neno alifanyika mwili akakaa kwetu.
Yn 1:14 SUV
[14] Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.
Tunaona baada ya Yesu kuondoka hapa duniani, yupo msaidizi mwingine alikuja kwetu, ambaye ni Roho Mtakatifu, msaidizi huyu akiingia ndani ya mtu anakaa au anaishi ndani yake.
Yn 14:16-17 SUV
[16] Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; [17] ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.
Nini napenda uone hapa, tumepewa uthibitisho na andiko hili kuwa Mungu wetu yupo karibu nasi, sio kimwili tu, hata kiroho yupo nasi kwa ukaribu mno..
Usije ukapita kwenye changamoto au shida fulani ukajiona upo peke yako, kibinadamu unaweza kuachwa peke yako, ila kwa Mungu hawezi kukuacha peke yako.
Efe 2:13 SUV
[13] Lakini sasa, katika Kristo Yesu, ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa karibu kwa damu yake Kristo.
Mungu hayupo karibu nasi kimwili tu uelewe hili, yupo karibu nasi kiupendo, kihuruma, na kiuhusiano, sifa ambayo mwanadamu hawezi kuwa nayo. Binadamu anachoka, upendo wake unaweza kuharibiwa wakati wowote.
Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana