Muonekano mpya wa Chidi Benz baada ya kutumia unga

mmmh,kwa mpukutiko huo haiwezi kuwa ngada pekee,nadhani na papuchi zimechagiza mpukutiko wake,aweke wazi anataka tumsaidiaje wanaume tuingie kwenye media tu-raise funds
Wastage of funds n time ...alikamatwa airport live na madawa akakiri kuwa ni yake lakini ikafanyika namna hakupelekwa chuo cha mafunzo kwakuwa tu ni Chid Benz...kumbuka kuna watu wanaozea jela kwa kesi za kusingiziwa....
Upendo sawa uwepo lakini na hekima pia
 

sure mkuu,hawa binadam wengine wameletwa duniani kwa makusudi ili wawe mfano kwa wengine,tuache maandiko yaendelee kutimia ili mungu aendelee kutukuzwa,baadae tutasema......roho ya bwana imwangazie......na mwanga wa milele.......,apumzike kwa amani,hapo mkuu ujue ndio kwisha habari yake hyo
 
Haya shime Watanzania, wapo watu wenye uwezo tofauti hivyo tuungane kumsaidia maadamu ameomba msaada kwa mdomo wake.
Iwe kwa kumpeleka soba, kumpatia dawa maalum kama Ray c au kwa namna yeyote ile ila tusikubali kumpoteza mtu huyu mwenye kipaji cha pekee na hakuna wa kumlinganisha nae.
 
Tusimshirikishe MUNGU tusiemwona kwenye Mambo ya chuki za kipuuzi.Chidi ni binadamu mwenzetu na anastahili nafasi ya pili.Kama kuna wadau mko Karibu nae msimtupe.Na kama hata ni hela ya rehab inahitajika mpango ufanyike humu jukwaani tumchangie..Namtakia afya na maisha marefu Chid Benz.
 
Acha uongo T.I kwy kili awards
 
Mtu mzima na mwenye akili timamu hujifunzi kwa kupitia makosa yawenzake! Na mtu mjinga hujifunza kutokana na makosa yake mwenyewe!

Kwa mtazamo wa kawaida na maswali rahisi ya kujiuliza na kumuuloza yeye mwenyewe chidi benzi ni kama yafuatayo;

1. Kati yake yeye na daz baba nani alianza kutumia hayo madawa?

2. Hakuona mifano ya watu waliomtangulia na kuona madhara ya hayo madawa!

3. Hakusikia wala kuona athari zitokanazo na madawa ya kulevya?

Nimeuliza hivyo kwa kuwa alikuwa ana mifano ya watu walio mbele yake na aliona madhara ya hivyo vitu!!

Je tukisema alikuwa anfanya makusudi na watu wasitake kumsaidia ataona watu ni wabaya ama nini?

Kuomba msaada haitosaidia endapo bado ataendelea kuwa mtumiaji wa hivyo vitu!

Jamani vijana wenzetu kuiga vitu visivyo vya msingi vitatubaribia maisha yetu sisi pamoja na vizazi vyetu!

Ahsante!
 
chidi ni bonge la msanii ila hayo mapoda yamempoteza njia totally,, sasa chuma yake! ila binafsi i wish apate huo msaada ainuke tena asee
 
Nakumbuka wakati Chid akiwa kwny "peak" alikua na mashaniki na wapambe wengi. Alipata mafanikio mazuri kimuziki. Nakumbuka alikua na kipindi EATV kikizungumzia maisha yake nje ya muziki.

Kilikua ni kipindi kizuri ambacho kingempa opportunity ya kufanya biashara na wadau mbalimbali kama angeweza kutumia fursa hiyo vizuri. Kupitia kipindi hicho Chid angeweza kuingia mikataba ya matangazo na makampuni mbalimbali na akaongeza kipato.

Lakini nasikia Chid alishindwa kumaintain kutokana na kutumia sn madawa ya kulevya hali iliyopelekea kunyang'anywa hiyo "air time". Lakini kama Chid angekua na nidhamu ya kazi leo angekua level za kina Diamond.

Ila kwa sasa ni mgonjwa, kadhoofika mno ma anahitaji msaada kwa wasamaria wema.

Lakini maisha yanatupa funzo kubwa kuwa hujafa hujaumbika. Ukiwa na nafasi leo itumie vzr na usimdharau yule asiyekuwa nayo. Historia ya Chid inatupa mengi ya kujifunza.

‪#‎September_20_mwaka_2015‬
Chid alitoa wimbo wimbo wake unaoitwa "matusi kwa Lowassa na Chadema". Wimbo huu una matusi mazito ya nguoni kumhusu mgombea Urais wa UKAWA Edward Lowassa na CHADEMA kwa ujumla.

Wimbo huu ulikua uploaded kwenye Youtube tar 25 September 2015 na Wema Sepetu. (Ingia Youtube andika Matusi kwa Lowassa na Chadema utaupata). Sehemu ya Maneno kwenye wimbo huo Chid anasema "ukiwa mwizi uraiani huwezi kuacha wizi ukienda ikulu, ukiwa mgonjwa uraiani huwezi kupona ukienda Ikulu"

Hapa Chid alikua akiendeleza ile propaganda ya CCM kwamba UKAWA wana mgombea mgonjwa. Sasa najaribu kumuangalia Lowassa alivyo sasa hivi na Chid alivyo sasa hivi najiuliza nani mgonjwa kati yao?

Je Chid alimtukana Lowassa kwa utashi wake? Kama sio utashi wake alitumwa na nani? Ka ujira gani? Mbona huyo aliyemtuma akaponde afya ya Lowassa hakumsaidia Chid kuimarisha afya yake kwanza?

‪#‎March_22_mwaka_2013‬,
Chid wakati huo akiwa na nguvu nyingi na afya nzuri alimpiga msanii mwenzake Marehemu "Ngwair" katika ukumbi wa "Ammbassador Luongue" uliopo kwny jengo la Benjamin Mkapa Tower jijini Dar. Sina hakika kama Chid aliweza kumuomba Ngwair msamaha kabla ya kifo chake.

‪#‎June_20_mwaka_2012‬
Chid Benz akiwa bado na afya nzuri alimtukana msanii mwenzie Profesa Jay na kutaka kumpiga ktk ukumbi wa Dar-West Park Tabata, kabla hawajaamuliwa na mashabiki.

Sababu ya kufanya hivyo Chid alidai ni Prof.Jay kusema ktk kipindi cha "Mkasi" kuwa yeye ndio alimuibua Chid na alimuombea ruhusa kwa mama yake ili amruhusu Chid kufanya muziki.

Sina hakika kama Prof.Jay alisema Manento hayo au Labda Chid alikua anatafuta tu sababu ya kufanya fujo maana alishazoea fujo.

Lakini hata kama Jady hakusema, je ukweli ni upi? Ukweli ni kwamba Prof.Jay ndiye aliyemuibua Chid. Hata jina "Chid Benz" alipewa na Prof.Jay.

Wakati anaanza muziki alikua anajiita "Benzino" jina la msanii wa Marekani. Professor Jay akamshauri atafute identity yake. Baadae akajiita "Chidi" kama kifupisho cha jina lake Rashid Abdala Makwiro.

Professor Jay akamsaidia kuunganisha jina "Chid" ambalo ni kifupi cha "Rashid" na jina "Benz" ambalo ni kifupi cha "Benzino", hivyo akapata "brand name" yake "Chid Benz" ambayo anaitumia hadi leo.

Najaribu kujiuliz hivi Chid angeambiwa anaweza kuwa ktk hali hii aliyonayo leo halafu yule aliyetaka kumpiga akawa Mbunge angeamini? Anyway maisha ni safari yenye mafunzo mengi njiani.

‪#‎May_05_mwaka_2013‬
Chidi alijaribu kumfanyia fujo msanii mwenzie wa BongoFleva "KalaPina" kwa kuvamia steji katika ukumbi wa Maisha Club Msasani. Lakini Kalapina alimdhibiti na Chid akaishia kupigwa yeye. Kala Pina alimwambia "usidhani mimi ni Ngwair"

‪#‎January_05_mwaka_2015‬
Chidi alijaribu kumpiga mwandishi wa habari kwa madai kuwa alimripoti vibaya alipokamatwa na madawa ya kulevya. Inadaiwa alimtwanga mwandishi huyo kabla "Babu Tale" kuingilia kati na kumuokoa.

Ripoti ya matukio ya Chid ni ndefu sana na pengine tunaweza kuelezea orodha ya matukio yake ya utukutu bila kumaliza maana ni ndefu sana.

Lakini kwanini Chid alikua mtukutu kwa kiwango hiki? Je ni sababu ya nguvu alizokua nazo? Je ni kiburi, ubabe, majivuno, fedha au wapambe? Je hakuwahi kufikiri kuwa siku moja anaweza kudhoofu na akashindwa kumpiga hata mtoto mdogo licha ya watu wazima aliokuwa akiwapiga?.

Chid amedhoofika kabisa kiafya kwa kile kinachodaiwa ni athari za madawa ya kulevya. Chid amechoka sana. Madawa yamemmaliza kabisa.
 

Attachments

  • chid.jpg
    19 KB · Views: 150
Tumuombee mola amsaidie kuondoka katika hali aliyonayo. Ila ni funzo kwa wasanii wengi kuacha maisha ya kuiga bila kuweka fikra za maisha yatakavyokuwa baadae.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…