Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Akiongea kwa uchungu kwenye kipindi cha Da Weekend Chat Show cha Clouds TV jana, Chidi ambaye mwili wake umepungua kwa kiasi kikubwa, amesema bado uwezo kimuziki anao lakini wale aliowaita wadau walioushikilia muziki wamemtupa.
Amesema wakati wa kilele chake, alikuwa akifanya show kila siku katika wiki, lakini kwa sasa mambo yamebadilika kabisa.
“Matatizo yangu na stress zangu ambazo niko nazo zinanisababishia mwili wangu unapungua kwasababu siko okay, siko poa, siko sawa yaani,” alisema.
Katika hatua nyingine Chidi alisema pamoja na afya yake kuzorota, hivi karibuni alipiga show kwa masaa mawili hadi mama yake akalia.
“Mama yangu akaniambia mwanangu unafanya show two hours, show kali watu wanapenda unachokifanya lakini sioni mwamko wa watu kutokea kukusaidia, kwahiyo tufanye mpango watu wakusaidie’ na mimi namuambia nataka watu wanisaidie, natamani kusaidiwa, natamani kupata mafanikio anayopata Diamond,” alisisitiza.
View attachment 330955
aliyoimba kuhusu ufisadi wa lowasa wala hayahusiani na sasa alivyo!Na yanayomkuta leo yote ni halali!! Au Siyo? SHilingi ina pande mbili mkuu.
Dogo janja nae anakula Unga?kwasasa chidi benz hamkuti dogo janja kwa afya,asaidiwe na nani badala ya kujisaidia mwenyewe kwanza kuacha upuuzi.
niliwahi kuwa mvutaji mzuri wa sigara,nikapata kansa ya mapafu nikatibiwa nikapona.daktari siku ananiaga alisisitiza kunywa pombe moshi achana nao.mpaka leo niko poa kwani kweli sijagusa.
Nilikua namkubali sana chid kwa rap zake kwakweli angeendelea angefika mbali sana.nafkiri Nay kidogo anafuatia lakini kwa Chid yuleeee Nay bado sana.
N survival of the fittest...!Golden chance never comes twice.. Wakati ukuta, ukishapita utajuta!
Mkuu hivi alikua ni TI au ni CASSIDY???Dah! Siku za Dar es salaam stand up haziwezi kurudi tena, huwa kuna nafasi moja Tu huwa inatokea, Chid yule anafanya show moja ya Kilimanjaro award then T.I Kama msanii mkubwa toka Marekani anaalikwa kwenye utoaji tuzo ule, wakati unafanya show ya nguvu kwa ngoma zako kali Naitwa nani! Babe ft Ray C, T.I ananukuliwa akiwauliza wenyeji wake alokaa nao.... "Huyu Ni nani?"...anaambiwa huyo Ni mwana Hip Hop anayekimbiza bongo, Na baadaye unashinda tuzo, T.I mwenyewe anakupatia tuzo, Na uhakika uliambiwa jinsi T.I alivyouliza kuhusu wewe, Leo kina Diamond wakipata nafasi Kama hizo wanazitumia hapo hapo, Ni vipi ungefanya ngoma Na T.I wakati ule, bila shaka ungekua mbali, all in all madawa yamekupoteza, sidhani Kama utapata msaada kwenye muziki wako tena, Sana Sana makosa yako wacha yatumike Kama funzo kwa vijana wengine, Na wenyewe wasipojifunza kwako! Wacha yawakute Tu, hatuna namna....sorry Chid Benz, fulsa huwa Ni Mara moja Tu!
Sio HIV mkuu mi unga tuu, mbona hata Paul Gascoigne Gazza yy pombe tu zimemfanya hivi hivi kawa kama zombie??akina Lineker wamemsaidia hadi wamechoka wameamua kuacha meli izame tuu.Hapana huyu atakuwa na HIV n addicted n unga tu mmmmh so kwa kukonda huko jaman
Hapana yana formula ambayo hupaswi kwenda nayo kinyume ni formula ya mizania ya haki hasa kwa wale wanaoonewa na wenye nguvuama kweli maisha hayana formula
Nishawaona watu wengi waliyowacheka watu ambao walikuwa wamejingiza ktk utumiaji wa madawa ambao na wako wakajikuta wameingia ktk utumiaji huko huo....kuna sababu nyingi ambazo humfanya mtu kujingiza ktk utumiaji wa madawa hayo...Safi sana mkuu, ndiyo maneno ya utu uzima. Sio kuonekana we mjanja wakati mwenzako ana shida.