Muonekano mpya wa Chidi Benz baada ya kutumia unga

Muonekano mpya wa Chidi Benz baada ya kutumia unga

Jamaa alisha saidiwa sana sema bdo anarudia kutumia haya madude aisee!
tatizo la chid ni mbishi,mbabe alikua hataki kusikia ana ambiwa aache kutumia poda.yani uki point finger kwake kua anatumia unga anakupa kisago....laiti angesikiliza ya walimwengu asingefikia hapo.
 
sasa mdau umeandika title historia fupi ya chid Benz kufungua ndani naona ni series ya mabaya yake tu, ndio historia hiyo?
 
Tuwe na roho ya kibinadamu jamani sasa mtu kaomba msaada asaidiwe na hali yake ndio hivyo kama mnavyomuona kwann mnaanza kumdhihaki?,sio vizur wakuu...huyu jamaa mbali na ngada pia depression inamsumbua ...nilishawahi kupitia hiyo hali kipind nimemaliza chuo alafu nipo tu mtaani napigika Dah! Niliisha vibaya kila mtu niliyekuwa nakutana nae ananiuliza unaumwa nn? ..Kama una msaada wowote msaidieni jamani kuliko mnAvyomfanyia ..leo yupo kesho hayupo.
 
Acheni kukatisha watu tamaa,sio lazima umsaidie wewe,kama Mungu anakusamehe pale unapojuta na kukiri makosa wewe ni nani?
 
Mange Kimambi on Instagram: “Chi chi chi chi Chidi Benz... I respect huyu msanii sana. Ni Mtu wa kujitolea, about 4 years ago nilikuwa na event ya Watoto yatima pale…”


Shida ya serikali hata watanzania waadilifu wakifichua wauza unga, majambazi serikali haitilii maanani mfano ni kwenye hii link hapa chini: Mange Kimambi on Instagram: “Chi chi chi chi Chidi Benz... I respect huyu msanii sana. Ni Mtu wa kujitolea, about 4 years ago nilikuwa na event ya Watoto yatima pale…” wametajwa watu maarufu wanaouza madawa ya kulevya wakiwamo viongozi wakubwa sana wa nchi.Je, inamaana TCRA, Polisi, Takukuru hakuna hata member mmoja hapa Jamiiforum??

Lets take it seriusly...kama mtanzania anathubutu kuwataza mapapa wauza unga kwanini vyombo vya sheria visichukue nafasi yake kuanza kuwachunguza/kiwachukulia hatua za kisheria????

Lets be seriusly people....
 
Chid is no more! Such an arrogant person to openly declare defeat...! something is on the way
 
1458456257479.jpg

Currently Chid Passo
 
Maskini imebaki miwani
Yaah yenyewe ndio haijakonda na inaweza kuwa inamzidi uzito.Kiukweli kama amefika khatua ya kupaza sauti ili asaidiwe pana haja ya wadau kufanya hivyo haya mambo mengine ya ku sema kwanini alitumia?hayawezi kumsaidia yeye na jamii ya watu kama yeye.Ndugu zangu kuna mataifa mengi yenye nguvu na vifaa bora lakini vita hii inawaelemea mpaka wakaamua kutengeneza rehabilitations centre baada ya kuona vita ngumu.Hatu entertain biashara hiyo kwa kusema wasaidiwe ila uraibu ukikupata hakuna namna ni vita ngumu ila kwanza inaanzia ndani ya nafsi yako than wadau watamalizia.
 
Nakumbuka wakati Chid akiwa kwny "peak" alikua na mashaniki na wapambe wengi. Alipata mafanikio mazuri kimuziki. Nakumbuka alikua na kipindi EATV kikizungumzia maisha yake nje ya muziki.

Kilikua ni kipindi kizuri ambacho kingempa opportunity ya kufanya biashara na wadau mbalimbali kama angeweza kutumia fursa hiyo vizuri. Kupitia kipindi hicho Chid angeweza kuingia mikataba ya matangazo na makampuni mbalimbali na akaongeza kipato.

Lakini nasikia Chid alishindwa kumaintain kutokana na kutumia sn madawa ya kulevya hali iliyopelekea kunyang'anywa hiyo "air time". Lakini kama Chid angekua na nidhamu ya kazi leo angekua level za kina Diamond.

Ila kwa sasa ni mgonjwa, kadhoofika mno ma anahitaji msaada kwa wasamaria wema.

Lakini maisha yanatupa funzo kubwa kuwa hujafa hujaumbika. Ukiwa na nafasi leo itumie vzr na usimdharau yule asiyekuwa nayo. Historia ya Chid inatupa mengi ya kujifunza.

‪#‎September_20_mwaka_2015‬
Chid alitoa wimbo wimbo wake unaoitwa "matusi kwa Lowassa na Chadema". Wimbo huu una matusi mazito ya nguoni kumhusu mgombea Urais wa UKAWA Edward Lowassa na CHADEMA kwa ujumla.

Wimbo huu ulikua uploaded kwenye Youtube tar 25 September 2015 na Wema Sepetu. (Ingia Youtube andika Matusi kwa Lowassa na Chadema utaupata). Sehemu ya Maneno kwenye wimbo huo Chid anasema "ukiwa mwizi uraiani huwezi kuacha wizi ukienda ikulu, ukiwa mgonjwa uraiani huwezi kupona ukienda Ikulu"

Hapa Chid alikua akiendeleza ile propaganda ya CCM kwamba UKAWA wana mgombea mgonjwa. Sasa najaribu kumuangalia Lowassa alivyo sasa hivi na Chid alivyo sasa hivi najiuliza nani mgonjwa kati yao?

Je Chid alimtukana Lowassa kwa utashi wake? Kama sio utashi wake alitumwa na nani? Ka ujira gani? Mbona huyo aliyemtuma akaponde afya ya Lowassa hakumsaidia Chid kuimarisha afya yake kwanza?

‪#‎March_22_mwaka_2013‬,
Chid wakati huo akiwa na nguvu nyingi na afya nzuri alimpiga msanii mwenzake Marehemu "Ngwair" katika ukumbi wa "Ammbassador Luongue" uliopo kwny jengo la Benjamin Mkapa Tower jijini Dar. Sina hakika kama Chid aliweza kumuomba Ngwair msamaha kabla ya kifo chake.

‪#‎June_20_mwaka_2012‬
Chid Benz akiwa bado na afya nzuri alimtukana msanii mwenzie Profesa Jay na kutaka kumpiga ktk ukumbi wa Dar-West Park Tabata, kabla hawajaamuliwa na mashabiki.

Sababu ya kufanya hivyo Chid alidai ni Prof.Jay kusema ktk kipindi cha "Mkasi" kuwa yeye ndio alimuibua Chid na alimuombea ruhusa kwa mama yake ili amruhusu Chid kufanya muziki.

Sina hakika kama Prof.Jay alisema Manento hayo au Labda Chid alikua anatafuta tu sababu ya kufanya fujo maana alishazoea fujo.

Lakini hata kama Jady hakusema, je ukweli ni upi? Ukweli ni kwamba Prof.Jay ndiye aliyemuibua Chid. Hata jina "Chid Benz" alipewa na Prof.Jay.

Wakati anaanza muziki alikua anajiita "Benzino" jina la msanii wa Marekani. Professor Jay akamshauri atafute identity yake. Baadae akajiita "Chidi" kama kifupisho cha jina lake Rashid Abdala Makwiro.

Professor Jay akamsaidia kuunganisha jina "Chid" ambalo ni kifupi cha "Rashid" na jina "Benz" ambalo ni kifupi cha "Benzino", hivyo akapata "brand name" yake "Chid Benz" ambayo anaitumia hadi leo.

Najaribu kujiuliz hivi Chid angeambiwa anaweza kuwa ktk hali hii aliyonayo leo halafu yule aliyetaka kumpiga akawa Mbunge angeamini? Anyway maisha ni safari yenye mafunzo mengi njiani.

‪#‎May_05_mwaka_2013‬
Chidi alijaribu kumfanyia fujo msanii mwenzie wa BongoFleva "KalaPina" kwa kuvamia steji katika ukumbi wa Maisha Club Msasani. Lakini Kalapina alimdhibiti na Chid akaishia kupigwa yeye. Kala Pina alimwambia "usidhani mimi ni Ngwair"

‪#‎January_05_mwaka_2015‬
Chidi alijaribu kumpiga mwandishi wa habari kwa madai kuwa alimripoti vibaya alipokamatwa na madawa ya kulevya. Inadaiwa alimtwanga mwandishi huyo kabla "Babu Tale" kuingilia kati na kumuokoa.

Ripoti ya matukio ya Chid ni ndefu sana na pengine tunaweza kuelezea orodha ya matukio yake ya utukutu bila kumaliza maana ni ndefu sana.

Lakini kwanini Chid alikua mtukutu kwa kiwango hiki? Je ni sababu ya nguvu alizokua nazo? Je ni kiburi, ubabe, majivuno, fedha au wapambe? Je hakuwahi kufikiri kuwa siku moja anaweza kudhoofu na akashindwa kumpiga hata mtoto mdogo licha ya watu wazima aliokuwa akiwapiga?.

Chid amedhoofika kabisa kiafya kwa kile kinachodaiwa ni athari za madawa ya kulevya. Chid amechoka sana. Madawa yamemmaliza kabisa.
Daaa umetoa historia nzur sana na ya kweli.

Nadhani itoshe kujifunza kuwa hujafa hujaumbika.
Inauzunisha na Pia Inakasirisha!
 
Atapewa msaada
Lakini hayo yaliyo mfanya hivyo haya achi
 
Back
Top Bottom