Muonekano mpya wa Chidi Benz baada ya kutumia unga

asmaa80 kubaliana na Mimi huwa unataka watu wanaomshutumu huyo jamaa waache Mara moja kwa sababu hakuna ushahidi wa moja kwa moja. Lakini uelewe hapa dunani lisemwalo lipo hakuna linalozuka bila kuwa na chanzo. Picha uliyonifurahisha ni kwamba hupendi madawa na madhara yake unayajua jinsi yanavyoumiza ndugu na jamaa zetu.

Ngwea,langa,banza, na wengine wanaoendelea kutumia ambao definitely mwisho wao ni mbaya wakuguse na wewe na usimtetee mtu yeyote anayehusishwa na kuharibu jamaa simply anatengeneza millions of money. Pesa na vyote tutaviacha Ona wazazi wa hawa waathirika hasa mamake chid anavyolia, it hurts
 

Ni kweli lakin humu JF kuna tabai moja Akitajwa huyo mtu unaedai namtetea kila mtu anatiririka kwamba ni kweli japo hawana ushahidi hata chembe, Lakin kuna baadhi ya majina yakitajwa wanakuwa wakali ati watu walete ushahidi, Hii inaonyesha huyu kijana kinachomponza ni siasa na hakuna kingine, leo kuna Thread imewekwa jinsi Mange kimambi alivyoweka majina hadharani badala ya kuongelea hiyo issu wanataka Mange alete Ushahidi, basi na huyu nae akitajwa pia mlete ushahidi kama hatuna ushahidi tukae kimya, nina uhakika Kitengo husika wapo, kama kuna ukweli watalifanyia kazi, Narudia tena simtetei, na wala sitamtetea mtu yoyote wa aina hiyo, na sitaki kumnyoonshea kidole mtu kwa jambo kubwa na baya kama hilo.
 
Mi ni mwepesi wa kuelewa, nimekuelewa kwamba unakuwa mkali kwa sababu kuna watu wamekaa humu kisiasa zaidi na siyo kiuhalisia, hilo ni kweli na nakubaliana na wewe na naunga mkono msimamo wako
 
Chidi bila kujitafakari wewe mwenyewe Na kuto kutoa kisingizio chochote sijui mbona fulani wanakula asemwi sijui kuna MTU kaniloga watu hawanipendi jua wewe mwenyewe ndio mchawi Wa maisha yako akuna mchawi aliyekuloga ukale unga akuna mchawi aliyekuloga ukane uli unga upige watu wanaokushauri Chidi jua uwezi kuomba usaidiwe kurudi bila kujisaidia wewe kuacha unga kwanza kuanza kufikiriwa afya yako kabla ya kufikiriwa mziki wewe msaada unaotaka ni kurudi katika mziki Na si kuacha unga unavyoenekana ndio maana unasema Fulani hivi Fulani hivi jisaidie mwenyewe mchawi wako ni wewe mwenyewe Chidi najua utasoma au watu wakaribu yako watasoma wakufikishie ukikubali mchawi Wa maisha yako ni wewe mwenyewe nakuhakikishia watu watakushangaa utakavyorudi fasta kuanzia kiafya hadi kimafanikio
 
Sasa anafanyiwa fitna au analogwa na nani? Eti anadai anazungukwa na watu wanaotaka kumuona ye yuko vile. Huyu hawezi kuacha huyu.
 
Wasanii wa Bongo asilimia kubwa wakishapata kick kidogo, chochote wanachopata ni kukiwekeza kwenye starehe, kupiga unga na ngono...kati ya kumi, wasanii 8 watakuwa wanapiga ganja na ngada, ngono ndio usiseme, kila wakati elimu inatolewa juu ya madhara ya hivi vitu na wanaona jinsi ambavyo wenzao walivyoathirika lakini bado wanaendeleza, ikifika hatua wakishaona yamewapata ndipo wanaanza kuhangaika kutafuta msaada! Haya yanayotokea kwa hawa iwe fundisho kwa wale wanaoanza au wanaojaribu kutumia ngada, iwe wasanii au watu wengine! Ngada na kuendekeza ngono sio issue kabisa, mwisho utaonekana kero mbele ya macho ya wale watakaokuwa wakikuhudumia angali tahadhari ulipewa, Mambo ya kusema "Mama nimeharisha tena" daah, inauma sana...
 
"CHID GOOO YEAH I'M GOING NAPOKAMATA MIC NAWAKATA VILIMILIMI,CHID FLOWWWWW YEAH I'M FLOWING NAPATA HESHIMA MAFANS WA KILA AINA SILII NJAA NIPO PEACE LINANILINDA JINA, CLASSMATE LAMAR ILALAAAAAA MIKONO MFULULU YANII PAPAA PAPAAA WAMEKAAAAA."........Inasikitisha sana nikisikiliza mipini ya CHID.
 
"CHID GOOO YEAH I'M GOING NAPOKAMATA MIC NAWAKATA VILIMILIMI,CHID FLOWWWWW YEAH I'M FLOWING NAPATA HESHIMA MAFANS WA KILA AINA SILII NJAA NIPO PEACE LINANILINDA JINA, CLASSMATE LAMAR ILALAAAAAA MIKONO MFULULU YANII PAPAA PAPAAA WAMEKAAAAA."........Inasikitisha sana nikisikiliza mipini ya CHID.
 
Chidbenz ni wakuhurumiwa,mie sio shabiki wake but kama binadam na kijana mwenzie nasema hatua aliyoipiga jamaa inamuumiza na mwenyewe ashalijua hilo.kingine laana sometimes tunajitafutia wenyewe,haya mambo yakusema sijui fulani anaumwa fulani dhaifu ngoja nimpige nitafute kiki sio mazuri,,mengine Mungu anakuonyesha hapa hapa duniani ili yule uliemhisi vibaya akikuona apate japo faraja,Chid wamsubiri akisanue mtaani huko wamtupe jela mwaka na kazi ngumu akitoka mamake awe nae karibu na asisitizwe ubaya wa cocaine hii yaweza msaidia kurudi kwenye game.
 
Takuombea kwa mungu Chidi Benz kama ndugu na kama Mtanzania mwezangu ili mungu akupe nguvu za kuyashinda majaribu japo mimi na Bongo fleva ni vitu viwili tofauti. Nishakuona siku moja kanda ya ziwa una kipaji na unaweza. Umeteleza simama kaka kwa kuwa umetubu.
 
Daah huyu jamaa alikuwa na body flan hivi akipiga kila pamba inamkaa vizuri na alkuwa anajua kuvaa.....had akawa model wangu,lakini sasa hv kwisha kaz.Nakuombea kheri brother urudi kwenye hali yako ya kawaida yote haya maisha,kukiri makosa ni mwanzo wa kujirekebisha na kusonga mbele.God be with you.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…