MUSSA ALLAN
JF-Expert Member
- Oct 13, 2013
- 18,925
- 13,267
Huyu akapime kisukari.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
hawa watu ni watumishi wa shetani lazima ahakikishe mwisho wao unakuwa mbaya.Kuna nini katika tasnia ya muziki wa bongo flava?Nikimuangalia Chidi Benz, Mr Nice, Ray C nakuwa kama napoteza hope.
Akiongea kwa uchungu kwenye kipindi cha Da Weekend Chat Show cha Clouds TV jana, Chidi ambaye mwili wake umepungua kwa kiasi kikubwa, amesema bado uwezo kimuziki anao lakini wale aliowaita wadau walioushikilia muziki wamemtupa.
Amesema wakati wa kilele chake, alikuwa akifanya show kila siku katika wiki, lakini kwa sasa mambo yamebadilika kabisa.
“Matatizo yangu na stress zangu ambazo niko nazo zinanisababishia mwili wangu unapungua kwasababu siko okay, siko poa, siko sawa yaani,” alisema.
Katika hatua nyingine Chidi alisema pamoja na afya yake kuzorota, hivi karibuni alipiga show kwa masaa mawili hadi mama yake akalia.
“Mama yangu akaniambia mwanangu unafanya show two hours, show kali watu wanapenda unachokifanya lakini sioni mwamko wa watu kutokea kukusaidia, kwahiyo tufanye mpango watu wakusaidie’ na mimi namuambia nataka watu wanisaidie, natamani kusaidiwa, natamani kupata mafanikio anayopata Diamond,” alisisitiza.😀
Huyu uenda anaendelea au ana matatizo mengineau labda ndio effect za rehab
Duuh.... Tusije tukampoteza kama NGWAIR