Punguza stress ndugu yangu!!
Punguza chuki zako dhidi ya serikali na wananchi wanaoipenda au kuifurahia serikali yao.
Punguza hasira na wamachinga,mamalishe na wengine wanaopambana kupata tonge.
Pita nchi nzima,machinga na mama ntilie biashara zao wanafanya stendi ama pembezoni mwa barabara....ama mahali popote penye shughuli zinazofanya watu kupatikana kwa wingi...mfano viwandani na maeneo yanapopatika wanachuo au hata ndani ya fensi za baadhi ya shule za msingi na sekondari.
Ni upumbavu kutaka watu waruhusiwe kufanya shughuli hizo kwenye viwanja vya ndege au ikulu. Na pia,natiliashaka uelewa wako wa mambo. Jaribu kuwa na akili ya ziada kwenye kupambanua mambo.
ACHA HASIRA NA CHUKI.