Muonekano mzuri wa Stendi mpya ya Mbezi umeharibiwa na Siasa zetu za kutafuta sifa kwa Wanyonge waliobatizwa Masikini

Muonekano mzuri wa Stendi mpya ya Mbezi umeharibiwa na Siasa zetu za kutafuta sifa kwa Wanyonge waliobatizwa Masikini

Wangendaliwa utaratibu mzuri tu sio kuwabeza na wao ni watanzania kama watanzania wengine, Mh.Rais alikua sahihi kabisa maana sio kila mmoja mwenye uwezo wa kula ama kununua vitu kwenye supermarkrts Malls na Hoteli kubwa kubwa kadhalika na wamachinga wanahitaji pia kuuza ndizi, mahindi, karanga bidhaa za mkononi e.t.c
 
Anaejua shida za watu wake Ndio kesharuhusu.

Wengine/mnaokereka mnatakiwa mpande ndege huko Airport.
 
Wewe ni maskini au tajiri?
Tumzungumzie bakhresa ndugu, mimi siwezi kuja kuwa masikini wa kulia lia na serikali ili nipewe uhuru wa kuharibu mali za taifa langu. Watanzania wenzangu wanafanya kazi kwa bidii wanalipa kodi zinatengeneza mali anakuja mtu analipa 20k mwaka mzima, hanunui simu ya gharama, hasomeshi mtt kwa gharama, hanunui chakula cha gharama, haendi tour hata siku moja, hapandi ndege hata siku moja, haagizi gari hata siku moja, haagizi mzigo hata siku moja, halafu anachafua na kuharibu vile wanavopigania wenzie. Kesho inakuja gharama ya ukarabati anatoa 20k serious!?

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app
 
Viongozi wa awamu hii ni malofa na wapumbavu! Wanajipendekeza kwa wananchi ili waonekane wanapendwa kumbe wanatuchafulia miji yetu!
 
Anaesema wanyonge na masikini aseme suu nimpige makopo na matusi, wattu tunalipa nauli tunasafiri unasema maskini wanyonge!!!
 
Nimesema huwezi linganisha airport na stand ya mabas, huelewi😎
Umesema ujinga kwa sababu maeneo yote mawili yanahudumia wasafiri wenye mahitaji sawa ya safari yanayopatikana kwa Machinga na Mamalishe. Msafiri Msukuma kama wewe anasafiri toka Dar es Salaam madege ya Magufuli yapo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa anakata tiketi yake, atanunua zawadi huyooo anatelemka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Chato na zawadi alizonunua kwa Machinga. Mlugulu anakwenda kwao Mji kasoro Bahari kusalimia ndugu anakata Tiketi yake Magufuli Bus Stand huyooo na Hood Bus Service mpaka Moro Stand ya Kisasa iliyofunguliwa na Magufuli, anatelemka na zawadi alizonunua kwa Mamantilie. Kila kitu Magufuli hata ile Nyumba ya TANU Lumumba iliyofunguliwa karibuni!
 
Umenikubusha mbali tulipokuwa tunachanganyika skuli kuna kabila lilikuwa linapanda juu ya vyoo vya kukaa tulikuwa tunapata tabu sana mpaka walipo elewa matumizi ya vyoo hivyo hivyo kwenye hili tutaelewana baada ya hasara
Na wewe unanikumbusha mbali miaka hiyo tulipokwenda kusoma Ulaya, mwanafunzi mwenzetu Msukuma alipata shida sana kula kwa uma na kisu hasa wali maana chakula chote kikawa kinadondoka sakafuni mwisho akaanza kula kwa mikono, wanafunzi wenyeji wakawa wanatucheka na kutukejeli sana wakituita nyani. Wenzake tulitahayari sana kwa sababu ya Msukuma mmoja lakini bahati nzuri alikuwa msomi akajifunza haraka kula chakula cha wenyeji kama mwenyeji mpaka akabaki huko hadi leo kama yuko hai. Tatizo letu ni elimu hata viongozi wetu imewapiga chenga.
 
Kweli wanapiga vibanda vya mama ntilie, pale parking, wauze mitumba na 'kalcha' mbele na nyuma ya maviete.😂😂

Stendi yenyewe finyu sana kwa nafasi parking ya mabasi, pale asubuhi sijui inakuwaje?? Nafikiri wenye ofisi zao Shekilango na Ubungo kama Allys, BM, Kilimanjaro, ABC wataendelea kupakia abiria huko, kuepusha aibu ya basi kutokutosha hapo.

Everyday is Saturday............................... 😎
Kama ndio hivi nitaendelea kupanda mabasi yanayoshukia Shekilango
 
Back
Top Bottom