- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Inadaiwa Mwendokasi mpya zimefika leo kwenye roro.
Je, zitadumu?
Je, zitadumu?
- Tunachokijua
- Mei 25, 2024, baadhi ya akaunti kwenye mitandao ya Kijamii kwa nyakati tofauti zilichapisha taarifa inayodai kuwa Serikali imeingiza nchini mabasi mapya yaendayo haraka, maarufu kama mwendokasi. Baadhi ya akaunti hizo ni hii, hii na hii.
Pamoja na mambo mengine, taarifa hii inadai mabasi haya yameletwa ili kuondoa changamoto ya usafiri jijini Dar es salaam.
Ukweli wake upoje?
JamiiCheck imezungumza na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (DART), William Gatambi aliyekanusha taarifa hizo.
"Inawezekana labda yanasafirishwa kwenda nchi nyingine, sisi hatuna taarifa hayo mabasi kama ni ya kwetu, tumeona picha zikisambaa Mtandaoni lakini hatuna taarifa rasmi juu ya Mabasi hayo" amesema Gatambi.
Aidha, Taarifa za ukakika kutoka vyanzo vya Bandarini ambazo JamiiCheck imezipata ni kuwa mabasi hayo yalikuwa safarini kuelekea Nchi nyingine na yalishushwa hapo ikiwa wakati wa mchakato wa kushusha mizingo mingine kisha yakarejeshwa ndani ya meli husika.
Wakala ya Mabasi Yaendayo Haraka (DART) ni taasisi ya serikali iliyoundwa kwa mujibu wa tangazo la serikali No. 120 la tarehe 25 Mei 2007 chini ya sheria No. 30 ya Wakala za Serikali ya mwaka 1997 na marekebisho yake.