SI KWELI Muonekano wa Mabasi mapya ya Mwendokasi yaliyoletwa na DART

SI KWELI Muonekano wa Mabasi mapya ya Mwendokasi yaliyoletwa na DART

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Inadaiwa Mwendokasi mpya zimefika leo kwenye roro.

Je, zitadumu?

mwendokasi_mpya1.jpg

mwendokasi_mpya2.jpg

Mwendokasi_mpya4.jpg
 
Tunachokijua
Mei 25, 2024, baadhi ya akaunti kwenye mitandao ya Kijamii kwa nyakati tofauti zilichapisha taarifa inayodai kuwa Serikali imeingiza nchini mabasi mapya yaendayo haraka, maarufu kama mwendokasi. Baadhi ya akaunti hizo ni hii, hii na hii.

Pamoja na mambo mengine, taarifa hii inadai mabasi haya yameletwa ili kuondoa changamoto ya usafiri jijini Dar es salaam.

Ukweli wake upoje?
JamiiCheck imezungumza na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (DART), William Gatambi aliyekanusha taarifa hizo.

"Inawezekana labda yanasafirishwa kwenda nchi nyingine, sisi hatuna taarifa hayo mabasi kama ni ya kwetu, tumeona picha zikisambaa Mtandaoni lakini hatuna taarifa rasmi juu ya Mabasi hayo" amesema Gatambi.

Aidha, Taarifa za ukakika kutoka vyanzo vya Bandarini ambazo JamiiCheck imezipata ni kuwa mabasi hayo yalikuwa safarini kuelekea Nchi nyingine na yalishushwa hapo ikiwa wakati wa mchakato wa kushusha mizingo mingine kisha yakarejeshwa ndani ya meli husika.

Wakala ya Mabasi Yaendayo Haraka (DART) ni taasisi ya serikali iliyoundwa kwa mujibu wa tangazo la serikali No. 120 la tarehe 25 Mei 2007 chini ya sheria No. 30 ya Wakala za Serikali ya mwaka 1997 na marekebisho yake.
Ukicompare na Mchina tena? Hahaa

Hayo mabasi hata Ulaya, Middle East na Latin America wanayanunua sana sema tu kule ziko katika mfumo wa electric buses

Tena kama Yutong na BYD ziko nyingi tu katika majiji ya Ulaya

Ina maana yame-comply with European market standards
Sema wenzetu wanajali sana service, professionalism ya uendeshaji, miundombinu gari inayopitia na muda wa chombo kutumika. Gari linaweza kufanyiwa service za kawaida ndani ya miaka 2 basi halitumiki tena, wana expose kabla hata halijabadilishwa chochote, likija huku tunasema gari mpya kabisa. Sisi tunatumia gari mpaka life, ambapo utakuta vitu vyote vilishabadilishwa, huwezi ukakuta spare iliyokuja na gari.
 
hayo mabasi wanadai ni ya nchi jirani nyie bongo endeleeni kusifiana tu wakati mibarabara mnajenga mji mzima lakini magari hamna , yaani wabongo tunaweza uchawa tu na kusifiana ila masuala ya msingi walaaaaaa hatumo.POLENI
 
Ukicompare na Mchina tena? Hahaa

Hayo mabasi hata Ulaya, Middle East na Latin America wanayanunua sana sema tu kule ziko katika mfumo wa electric buses

Tena kama Yutong na BYD ziko nyingi tu katika majiji ya Ulaya

Ina maana yame-comply with European market standards
N kweli yapo mengi. Lakini mimi naona hata Europe yanachakaa haraka sana. Kuna nchi moja niliona walinunua mengi mwaka juzi sasa hivi ni kama yamechakaa hivi.
 
Udart haitunzi mabasi. Viti vinapasuka hakibadilishwi, mabasi hayaoshwi, camera zinaning'inia tu. Wanachojua ni kujaza mafuta tu. Gari likipata tatizo kila mfanyakazi anajifanya fundi.
 
Eeh Mungu usiyeshindwa kitu ninakuomba unipatie gari yangu mwenyewe iwe ist au raumu au wish ila tu isiwe Passo ili hayo magari niyaonee tu yakipita kwa mbaliii. Sipendi Kubanana na lile jasho la mwendokasi. Yani unibariki kama ikitokea nimeyapanda basi iwe kwa kupenda mwenyewe ila sio kwasababu Sina mbadala. Amen
 
Omba pikipiki
 
Maisha yangu yote Dar ila sijawai kufika Tegeta na nisingeamua kwenda bila sababu pia nisingefika Gongo la mboto.

Mtu ukisema hujawahi kufika Mbagala kuna watu wanaona kama kejeli
Binafsi ni kama wewe,siwezi kwenda sehemu bila sababu
 
Back
Top Bottom