SI KWELI Muonekano wa Mabasi mapya ya Mwendokasi yaliyoletwa na DART

SI KWELI Muonekano wa Mabasi mapya ya Mwendokasi yaliyoletwa na DART

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Inadaiwa Mwendokasi mpya zimefika leo kwenye roro.

Je, zitadumu?

mwendokasi_mpya1.jpg

mwendokasi_mpya2.jpg

Mwendokasi_mpya4.jpg
 
Tunachokijua
Mei 25, 2024, baadhi ya akaunti kwenye mitandao ya Kijamii kwa nyakati tofauti zilichapisha taarifa inayodai kuwa Serikali imeingiza nchini mabasi mapya yaendayo haraka, maarufu kama mwendokasi. Baadhi ya akaunti hizo ni hii, hii na hii.

Pamoja na mambo mengine, taarifa hii inadai mabasi haya yameletwa ili kuondoa changamoto ya usafiri jijini Dar es salaam.

Ukweli wake upoje?
JamiiCheck imezungumza na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (DART), William Gatambi aliyekanusha taarifa hizo.

"Inawezekana labda yanasafirishwa kwenda nchi nyingine, sisi hatuna taarifa hayo mabasi kama ni ya kwetu, tumeona picha zikisambaa Mtandaoni lakini hatuna taarifa rasmi juu ya Mabasi hayo" amesema Gatambi.

Aidha, Taarifa za ukakika kutoka vyanzo vya Bandarini ambazo JamiiCheck imezipata ni kuwa mabasi hayo yalikuwa safarini kuelekea Nchi nyingine na yalishushwa hapo ikiwa wakati wa mchakato wa kushusha mizingo mingine kisha yakarejeshwa ndani ya meli husika.

Wakala ya Mabasi Yaendayo Haraka (DART) ni taasisi ya serikali iliyoundwa kwa mujibu wa tangazo la serikali No. 120 la tarehe 25 Mei 2007 chini ya sheria No. 30 ya Wakala za Serikali ya mwaka 1997 na marekebisho yake.
Mtu ukisema hujawahi kufika Mbagala kuna watu wanaona kama kejeli
Binafsi ni kama wewe,siwezi kwenda sehemu bila sababu
Nikweli japo kuna wengi hufanya kwa kukejeli has naona wanaotokea upande wa kaskazini mwa DSM kwamaana Kimara, Mbezi, Tegeta.

Kijiografia DSM imekaa kama mkono ina njiia kuu tano (Mbagala, Gongo Mboto, Mbezi, Tegeta na Njia Kigamboni) ambazo zote zina Converge katikati ambapo no City Centre, asiliamia kubwa ya wa watu wa njia moja ngumu kufika njia nyengine bila bila kuwa na sababu ya ndugu, kazi nk.

Mimi nasihi Kigamboni tangu nizaliwe hadi huu umri wa 30 Tegeta nimepita na gari mara moja tu kuelekea Bagamoyo kishuleshule, Gongo la mboto ni lamia ngoja niende bila sababu, bila kwenda bila sasababu nisingefika sehemu nyingi.

Ni kawaida mtu wa Tegeta mbezi kutokufika mbagala kabisa, kingine watu wa mbaga rahisi sana kupata sababu ya kwenda Mbezi na Tegeta kuliko wa Tegeta kwenda Mbagala kwasababu Mbagala kuna fursa ndogo sana za ajira ukilinganisha na Mbezi huko, hata ukiangalia Jukwaa lile la ajira huon kazi hata moja mbagala ila Mbezi kawaida.
 
IMG-20240628-WA0010.jpg

IMG-20240628-WA0038.jpg

Kama kweli haya Mabasi yaliyopo bandarini ni mali ya UDART,

Basi miongoni mwakazi muhimu za PPP itakuwa ni haya magari mapya ambayo ni full AC wale wakupanda na samaki kutoka Feri mjitafakari.

Tetesi ni kwamba tayari bandarini yameingia Mabasi zaidi 80 Je, ni yetu?

Kwa mara ya kwanza Tanzania tutaanza kuona faida za PPP-Cetre kama kweli haya Mabasi yatakuwa ni mali yetu.

Kama Mabasi haya si yetu basi PPP wachukue mfano huu wa Mabasi kwani unavutia sana.

Tanzania, kama ni kweli Mabasi haya ni yetu au yale yetu yaliyoko njiani na kwa mambo mazuri kama haya ya bandari yetu tunamwachaje Rais Samia 2025?​
 
View attachment 3027985

Miongoni mwakazi muhimu za PPP ni haya magari mapya ambayo ni full AC wale wakupanda na samaki kutoka Feri mjitafakari.

Tayari yameingia zaidi 80 wakati mengine zaidi 100 yako njiani,

Kwa mara ya kwanza Tanzania tunaanza kuona faida za PPP-Cetre.

Kwamambo mazuri kama haya tunamwachaje Samia 2025?​
Kama kweli yataendelea kuwa hivi itakuwa njema sana
 
View attachment 3027985

Miongoni mwakazi muhimu za PPP ni haya magari mapya ambayo ni full AC wale wakupanda na samaki kutoka Feri mjitafakari.

Tayari yameingia zaidi 80 wakati mengine zaidi 100 yako njiani,

Kwa mara ya kwanza Tanzania tunaanza kuona faida za PPP-Cetre.

Kwamambo mazuri kama haya tunamwachaje Samia 2025?​
Acha upuuzi.
Hayo mabasi yapo huku Mwandiga?
Sisi mabasi hayo hayatuhusu,sukari Fake tuliyolishwa ndiyo inatutesa.
 
2025 nitakapokuwa rais.cha kwanza kabisa ni kuutupilia mbali huu mradi wa kihuni.mradi umeonesha failure 100%
 
Sio mali yetu. Sisi tunachukua EV za Uganda.
 
View attachment 3027985

Kama kweli haya Mabasi yaliyopo bandarini ni mali ya UDART,

Basi miongoni mwakazi muhimu za PPP itakuwa ni haya magari mapya ambayo ni full AC wale wakupanda na samaki kutoka Feri mjitafakari.

Tayari yameingia zaidi 80 wakati mengine zaidi 100 yako njiani,

Kwa mara ya kwanza Tanzania tunaanza kuona faida za PPP-Cetre kama kweli haya ni Mabasi yetu.

Kwamambo mazuri kama haya tunamwachaje Samia 2025?​
Yatafika mikoani ???!
 
Kwan pesa anatoa ktk mfuko wake huyo mama Samia? Pesa zinatoka kwa wanachi wenyewee. Lol
Ndio ni zetu ila akizitumia vizur lazima tumpe pongezi
Maana akifanya vibaya tunamsema asa kwann akifanya vizur tusimpe big up
 
Ndio ni zetu ila akizitumia vizur lazima tumpe pongezi
Maana akifanya vibaya tunamsema asa kwann akifanya vizur tusimpe big up
Kwanini afanye vibayaa? Sisi tunataka mazuri tyuuh.
 
Back
Top Bottom