POTOSHI Muonekano wa sasa hivi wa Justin Bieber amedhohofika kwa sababu ya dawa za kulevya

POTOSHI Muonekano wa sasa hivi wa Justin Bieber amedhohofika kwa sababu ya dawa za kulevya

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Wakuu,
Kwenye pitapita zangu nimekutana na hii post uko mtandaoni, jamani kama hali yake ndo hii inasikitisha sana na inaumiza hatima ya madawa ya kulevya

Naomba mnisadie kutambua kama ndo hali aliyofikia kwa sasa, ili tujifunze jamani

Bieber July 7, 025.jpg
Bieber July 7.jpg
 
Tunachokijua
Justin Drew Bieber ni msanii wa muziki kutokea Canada licha ya kuwa na uwezo mkubwa wa kuimba muziki aina ya ‘Pop’ lakini anajulikana pia kwa uwezo wake mkubwa wa kutumbuiza aina mbalimbali za muziki. Justin alijizolea umaarufu akiwa bado kijana mdogo, licha ya kazi zake za muziki lakini alijizolea umaarufu kutana na muonekano wake unaovutia.

Madai

Kumekuwepo na na picha zinazosambazwa katika mitandaoya kijamii zikimuonesha Bieber akiwa kwenye hali ya kudorora na kukosa nuru husasani usoni. Mtumiaji mmoja wa mtandao wa Instagram alichapisha picha ya aina hiyo huaku akiambatanisha na ujumbe uliosomeka “HALI ANAYOPITIA JUSTIN BIEBER WASANII MJIFUNZE” huku akisisitiza kuwa hali hiyo ni kutokana na madawa anayotumia msanii huyo.

Uhalisia wa picha hizo

JamiiCheck imefuatilia na kubaini kuwa picha hizo si za hivi karibuni na pia zimehaririwa ili kupotosha uhalisia.

Ufuatiliaji kwa njia ya google image reverse JamiiCheck imebaini kuwa picha hizo si za hivi karibuni mathalani picha ya upande wa kulia ni ya Oktoba 18, 2018 iliyopigwa huko Los Angles nchini Marekani ambapo Bieber alikuw ana mchumba wake Hailey Baldwin.

Picha ya kushoto ni ya mwezi Februari, 2025 ambapo Bieber alikuwa na mchumba wake kwenye mgawa huko New York Marekani ambapo picha halisi pamoja na video zinamuonesha Justin akiwa na afya njema si kama picha potoshi zinavyomuonesha.

Aidha Bieber kupitia ukurasa wake wa Instagram amekuwa akichapisha picha zake mara kwa mara ambazo zinamuonesha akiwa na muonekano tofauti na unaonekana kwenye picha hizo.
ni kweli anatumia drugs ila hana muonekano huo
 
Back
Top Bottom