Muonekano wa Wema Sepetu wazua gumzo mitandaoni, Mashabiki wamuandama na kumwambia maneno haya

Muonekano wa Wema Sepetu wazua gumzo mitandaoni, Mashabiki wamuandama na kumwambia maneno haya

KITAULO

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2018
Posts
1,926
Reaction score
2,797
Msanii wa filamu na Miss Tanzania mwaka 2006 Wema Sepetu, amezua gumzo mitandaoni baada ya kupost picha kwenye ukurasa wake wa Instagram ikimuonyesha mwili wake kuonekana kuzidi kupungua, Wema Sepetu ambae aliamua kupunguza mwili wake kwa madai ya kuwa unamnyima raha hasa katika kazi zake za kisanaa.
1582029643358.png
Screen-Shot-2020-02-18-at-13.58.19.png


Ikumbukwe kuwa katika mahojiano aliyoyafanya kupita App yake ya Wemapp alisema, ameamua kupunguza mwili wake kwa sababu ulikua unamletea shida sana hasa kwa upande wa filamu kuna mavazi alikua hawezi kuyavaa na kuna baadhi ya Scenes zilikuwa zinampa shida kuigiza kulingana na mwili aliokuwa nao kipindi cha mwanzo

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Wema aliamua kupost picha akiwa na wadada wengine wawili akiambatanisha na ujumbe kuwa “Alhamdulillah Rest Easy kaka” picha hii ilimuonyesha akiwa ametoka kwenye msiba wa kaka ake anaeitwa Mkusa Sepetu, ambaye alikuwa Jaji wa Mahakama kuu Zanzibar ambaye alipoteza maisha asubuhi ya Feb 16, 2020.

1582029687284.png


Wema baada ya kupost picha hiyo mashabiki wake wakaanza kumuandama kwa maneno mengi huku wakimwambia ameathirika, wengine wakamuambia ajitahidi kula maana wakikutana nae barabarani wanaweza kumsahau kabisa kutokana na mwili wake unavyozidi kuisha. Baada ya comment za mashabiki kuzidi Wema hakukaa kimya aliamua kuwajibu na kuwaambia kuwa Ni kweli ameathirika na kama watamsahau basi yeye ndivyo anavyotaka.

 
Nilikuwa nasikiliza BBC leo asubuhi, muimbaji Billie Eilish alikuwa anahojiwa kuhusu wimbo wake mpya wa movie ya James Bond "No Time To Die".

Alikuwa analalamika jinsi internet trolls wanavyomsakama, akasema siku hizi hata hasomi maneno ya mtandaoni.

Trolls wengi sana.

It is the price of fame.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kukonda ndio afya etii... tuulize vibonge tunavyohangaika...

Wema fanya hivii

Kunywa maji mengi ngozi yako itang’ara

Kabla ya kulala osha uso kutoa make up

Lala muda wa kutosha

Acha kutumia lotions zenye kuchubua/ chemicals kali,

Tumia moisturisers
 
Umaarufu na karaha zake.
Kuna tofauti ya mtu kuwa maarufu na mtu kuyafanya maumbile yake kuwa maarufu. Umaarufu wa maumbile ni umaarufu kunuka.

Mfano wa mtu maarufu ni Bob Marley...katangulia mbele za haki miaka mingi sana imepita, lakini bado tunamkumbuka. Hawa maarufu wa mwili siku tukiacha kuona miili na maumbile yao basi nao wanasahaulika kwani hakutakuwa na video chapa connection za kuwaibua kaburini
 
Back
Top Bottom