Muonekano wako ni kama unavokula... Pia akili yako ni kama unavoilisha

Natty Bongoman

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2008
Posts
648
Reaction score
384
Ule msemo wa wadhungu 'you are what you eat' ni kweli kabisa... muonekano na afya yako vinaendana na tabia zako za kula - espesheli aina ya vyakula unavokula.
  • ukila haraka haraka bila kutafuna vizuri unaingiza mabonge tumboni, hivyo tumbo na mwili vyatumia nguvu kubwa kusaga, na labda kushindwa kusaga mabonge yote ivo hupati vitamini na faida ya huo msosi - yaani mwili kunyonya virutubisho (absorption). Pia yaezekana unatanua tumbo.
  • ukila kitimoto kwa wingi utanenepeana ka nguruwe. Pia ukila vingine vyenye mafuta mengi au vya kukaangwa mafutani.

Unachoangalia mara nyingi humo televisheni (tell a vision) unachosikiliza mara nyingi (muziki NK) afu unakirudia kichwani, kwa mfano kuimba ule wimbo ulozama kichwani - maneno ya muziki yanazama ubongoni na matendo ya sinema na televisheni nayo yanazama. Pia unachosoma vitabuni nk
*** chagua vzr, wachagulie watoto vzr ili akili isivurugwe na wahuni washetwan. Moja ya silaha kubwa mzungu anatumia kutuharibu akili hata mila zetu nzuri, na kutopotosha ni hayo - sinema/tamthilia nk, nyimbo na vitabu.

  • Unafuatilia series kama dini, inakuingia akilini… Je inakufundisha nn kizuri maishani mwako? Chaguo ni lako wewe na Kwa wanao
  • Unaimba wimbo wa msanii flani kila siku, wanao pia… je unakufundisha nn bora maishani mwenu? Chaguo ni lako
Mfano mzuri ni vijana weusi kizazi kipya marekani... watawala wa muziki, yaani maproducer na mapromoter waliingilia RAP (HIP HOP) makusudi kwa kushurtisha nyimbo zenye maneno mbaya na video matusi na kukataa nyimbo zenye mantiki ama ujumbe mzuri kama enzi za kina Tupac na Public Enemy. Madhara yake ni wazi mno sasa ivi... vijana wao akili yao eti kuwa bora ni ugangsta, kuuza madawa levya, na wasichana kuwa biatches. Walopona ni wale ambao wazazi walikataza ama walifafanua kwa kufundisha hiki si bora. Wazungu nao kwa vizazi vingi, wanaamini wanachokiona sinemani na ndani ya televisheni na sasa mitandao. Ndio maana, kwa mfano, wazungu miaka nenda rudi wanafikiri Afrika yetu haina miji ni pori na watu kutembea uchi ka vile waonyeshwavo na masinema, vitabu mashuleni, nk

***Pia utajikuta unafagalia mafreemason bila kujitambua huku ukipaza sauti kusali nao ama kumtukuza shetwan... manyimbo tutayapenda tunapoyasikia ghafla, ila kazi kwetu ni kuelewa nini wanaimba na kina manufaa gani maishani mwako ukishaingiza kichwani ka vile ni mahubiri ya dini. Mimi ni mtu mzima na naburudishwa na uzuri wa kina Zuchu na nyimbo zao ngono/mahaba ILA binti akianza kuimba maneno hayo namuweka pembeni na kumfafanulia ubaya wa kuiga maneno ya tabia hizo. Hatuna njia nyingine ya kuzuia watoto wasisikie nyimbo hizo na wengine wetu tunaruhusu ama kuangalia sinema mbaya za utu uzima na watoto bila kuzuia ama kufafanua... dawa ya kuepusha akili zao zisipotoke ni kuweka mipaka ya wanachoangalia, wanachosoma, na wanachosikiliza - kudadisi na kufundisha mazuri pale tunaposhindwa kuzuia

Your browser is not able to display this video.
 
Mkuu Ukiangalia pia series za Mbinguni utaenda Mbinguni?
 
Mkuu Ukiangalia pia series za Mbinguni utaenda Mbinguni?
Mkuu, Inawezekana, ila kwa uhakiki akili yako itakuwa balanced na utaishi righteous kadri ya ubinadamu unavoruhusu. Swala kubwa hapa ni kuepuka kulisha mwili na akili sumu, haijalishi dini yako ama ukosefu
 
Yah! wataalam wa ubongo wanaita
Neuroadoptation.. unaweza kuwa mzungu kama kuongea and so on!
Haha unachekesha sana! Neuroadaptation inahusika zaidi na jinsi ubongo unavyozoea vitu kama vile dawa za kulevya au maradhi baada ya muda mrefu.

Sasa mzee tangu lini kuangalia tamthilia ikawa ni ugonjwa wa ubongo au madawa? Usikariri maneno bila kuyaelewa kwa upana kwanza.
 
Ok! mkuu mbona mimi kuna mengi nime ya adopt kutokana na kuangalia tu! kama jinsi ya kuzungumza british english?
 
Ok! mkuu mbona mimi kuna mengi nime ya adopt kutokana na kuangalia tu! kama jinsi ya kuzungumza british english?
Mzee kujua kuongea hicho kiingereza ni stadi tu ya lugha. Mbona kasuku naye akiishi na binadamu huwa anajifunza kusalimia? Kwani akili yake huwa inakuwa ya binadamu kweli?
 
 
Ukitazama sinema za kizungu na wewe unakuwa mzungu?
Nimeongelea tabia na sio muonekano wa mwili... hujaiga hata kitu kimoja cha sinema za kizungu ulizoangalia?

Pia kuna kuangalia sinema ukijua ni sinema, na kuna kuangalia sinema ukimeza kama ni ukweli
 
Mzee kujua kuongea hicho kiingereza ni stadi tu ya lugha. Mbona kasuku naye akiishi na binadamu huwa anajifunza kusalimia? Kwani akili yake huwa inakuwa ya binadamu kweli?
huyo huyo kasuku akiangalia sinema mbovu ama akisikiza maneno ya matusi ... anayarudia kuyatamka - kafundishwa na hilo
 
Nimeongelea tabia na sio muonekano wa mwili... hujaiga hata kitu kimoja cha sinema za kizungu ulizoangalia?

Pia kuna kuangalia sinema ukijua ni sinema, na kuna kuangalia sinema ukimeza kama ni ukweli
Mzee, wewe mwenyewe umekiri hapo mwishoni kuwa kuna kuangalia sinema ukijua ni sinema sasa mbona unajipinga mwenyewe?

Mimi huwa naangalia nikiwa najua kabisa ni uongo wa Hollywood na stori za kutungwa simezi kitu! Kama wewe huwa unaangalia hadi tabia zako zinabadilika, hiyo ni shida yako binafsi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…