MUONGOZO: Mambo ya kuzingatia unaponunua gari lililotumika ndani ya Tanzania

Kuagiza gari Japan inashauriwa mileage yake isizidi ngapi,?
 
Hilo linafanyika sana! Lakini mileage nyingi sio issue as long as gari limehudumiwa vizuri! Wengi wanauziwa magari mabovu kwa kuangalia low mileage,kuna vitu vingi vya kuangalia zaidi ya odometer readings.
Kwa kuagiza Japan inashauriwa Mileage isizidi ngapi??
 
Kwa kuagiza Japan inashauriwa Mileage isizidi ngapi??
Mileage sio kigezo kwasababu inaweza kuchezewa. Unaweza kuona gari inasoma 45000km wakati kiukweli ina 145,000km.
Au inaweza kuwa na 60,000km genuine lakini mmiliki hakuwa anatunza gari, gari ingine ina 90,000km lakini mmiliki analitunza na ana dealer service history ya gari tangu ameinunua mpaka inafikisha hio 90,000km.(service history itakuonesha matengenezo yote gari iliofanyiwa,risiti na dealer aliefanyia,unaweza kuwapigia simu wakakuthibitishia).

Kwangu mimi afadhali ninunune gari lenye 100,000km na dealer service history yake kuliko lenye 40,000km bila service history.
 
Kuna rafiki yangu aliniomba ushauri kuhusu gari fulani,nikamwambia usinunue lakini baada ya wiki nikamuona nayo!!! Sasa hivi nimekuwa mshauri wake wa kiufundi,kila siku majanga! Papaara mbaya sana
gari gani hyo mkuu..utuokoe na wengine
 
Nice
 
Kwani ikitembea km 100,000 tatizo nini? Nina gari ina km 230,000+ na iko vizuri popote naenda muda wowote.
Haina shida kubwa bali ubora/uzima wa engine hutegemea km na mwaka gari ilipotengenezwa .Wewe hiyo ya kwako hukununua km ikiwa hivyo na pia labda unazingatia service kwa wakati ndio maana ukinunua gari mikononi mwa mtu au used kutoka nje nunua chini ya km 100,000 utakuwa umepata kilicho bora zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajuaje hizo km chini ya 100,000 ni za kweli? Labda ina 250,000km wameichezea wamekuwekea 50,000km.

Ubora na uzima wa engine hautegemei mwaka na km za gari. Unategemea matunzo ya gari. Unaweza kuwa na gari ya mwaka 2010 ina km150,000 ikawa na hali nzuri kuliko 2010 yenye km 80,000.
 
Kk gari ambayo km zake zinasoma kidigital huwezi chakachua km kwani ukichakachua lazima uguse control box na bei yake sijui kama unaijua?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Reactions: Atn
Asante kwa kutufungua macho mkuu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…