Uzi mzuri sana huu ila tunaomba utuwekee na upande wa pili... Mambo ya kuzingatia unapouza gari! . Mimi nauza Spacio new model, sasa nimekutana na mambo kadhaa. Hapo kwenye namba 3. wameshakuja madalali kama watatu, wote wanakwamia bei ya 6.5m, mwingine 7m, mwingine 7.5m. Mimi nimetangaza 8m siyumbi. Maana yake ni kwamba dalali ataenda kutangaza 8m au zaidi huku mimi naambulia 7, ujinga kabisa. nimewatimua.
Namba 5. Kuna watu wananishauri nipige rangi gari wakati halijagongwa wala halina mbamizo wowote, sana sana kuna vimistari vidogo sana ambayo labda ukute nilipita sehemu ikaguswa na kitu kama mwiba ukaweka alama, sasa vitu kama hivyo mimi nimekataa kwenda kupiga rangi ili mteja akija aone gari katika uhalisia wake.
No.8. Madalali wengi wanaangalia plate no. Anakuja anasema bro hiyo gari yako namba C huwezi pata mteja wa 8m, mimi ukinipa 7.5m nakuletea IST yenye namba D. Wanasahau factors zingine kama utunzaji wa gari, mileage, ajali, na imetumika barabara zipi na kwa matumizi gani kabla haijauzwa. Unaweza kuletewa namba D mbovu kuliko hata namba C au B.