Muongozo wa kununua vifaa vinavyotumia processor za intel

Muongozo wa kununua vifaa vinavyotumia processor za intel

bajeti yangu ni laki8 naweza kupata yenye specification za juu zaidi ya hiyo
Unapata kibao mkuu

Gen ya 8 minimum kwa budget yako, na ukipata yenye dedicated graphics ya Nvidia ama Radeon ni plus..

Mfano hii
 
Unapata kibao mkuu

Gen ya 8 minimum kwa budget yako, na ukipata yenye dedicated graphics ya Nvidia ama Radeon ni plus..

Mfano hii
sawa mkuu nimekuelewa shukrani sana
 
Wakuu msaada kidogo ninahitaji kununua Playstation 4...Nimefanya survey kwa sellers wengi kidogo(kwenye page za Instagram) na nimegundua kuna tofauti kubwa ya bei kati ya sellers wa Kenya na TZ kitu amnacho kinanipa wasiwasi kidogo...mfano; playstation 4 Pro sellers wengi wa tanzania wanauza kuanzia laki 8 na 50 na kuendelea ila kuna sellers wa kenya wawili mmoja laki 5 na 40 na mwingine laki 6: Sasa je hizi bei za wakenya ziko real kweli kwa PS 4 Pro tena unapewa 2 Pads na Parcel yako isafirishwe kwa DHL kwa gharama zao?? Hakuna utapeli kweli hapa? Maana this offer is too good to be true..Mwenye experience ya haya masoko ya Instagram hasa Kenya anisaidie
 
Tapeli huyo.

Pro ni around $350 hivyo 8 na nusu ina make sense zaidi
 
Tapeli huyo.

Pro ni around $350 hivyo 8 na nusu ina make sense zaidi
Kweli asee nimeangalia zinakotoka huko amazon ebay Ali na hata market za dubai kote bei ni kubwa how come Kenya bei ziwe low vile..NI MATAPELI
Tena yeyote akiona kwenye business pages za Instagram wamepost products ila wamerestrict watu wasicomment basi kuna dalili za utapeli hapo
 
Ameshaiuza, nilisubiria kidogo nikampigia kama hujaichukua nichukue, alinijibu ameuza.
Mkuu kuna swali kidgo hapa hivi katika hizi API direct x 11 direct x 12 na vullkan which is better for gaming? Vulkan nimejalibu kutumia imenishinda sijajua inafanyaje kazi msaada plz; coz kuna baadh ya game vullkan ina run smooth sana
 
vulkan na direct x12 ni version mpya, zimekuja kureplace version za zamani kama Open GL na direct x11, sema bado zipo katika early stage na si kila game itakupa perfomance kubwa.

kwa wewe mwenye GPU ya Amd vulkan ina possibility kubwa kukupa perfomance nzuri, Amd ni katika kampuni zilizotengeneza Vulkan hivyo wanaisuport. Kwa Nvidia wana drivers nzuri za Open Gl.

na pia Faida kubwa ya Vulkan/direct x12 ni
-kutumia multi core
-ku access low level hardware kama vile console (ps3 ps4 etc)

hivyo games za kizamani ambazo zilikuwa zinatumia core moja hazitapata perfomance kubwa sana, ila games za kisasa zinazotumia core nyingi kuna uwezekano mkubwa kupata boost.

mwisho wa siku mkuu direct x11 ni ya zamani na ipo stable sana, hivyo kila game jaribu vulkan ama directx12 ukiona inazingua rudi direct x11, game halitarun kwa speed sana ila itakuwa stable.
 
Mimi mkuu bado natumiaga director x 11_ mpk leo cjawahi kujaribu kutuma director x 12_ ila vulkan inanishida jinsi ya kuitumia alafu ajabu hata kua stail direct x 11_ swez niweke 12_inanishida hebu nipe msaada kidgo hapa mkuu
 
Computer nyingi tunazonunua huwa zinatumia processor za intel au amd, lakini ni intel ambaye ametawala sana kushinda amd kwenye computer zetu. Leo nimeamua niandike uzi huu kuhusu hizi processor za intel na namna ya kuzichagua ili kuwasaidia watu wanapotaka kununua laptop/desktop mpya wafanye maamuzi sahihi.

Processor ni nini?

Labda utakuwa unajiuliza kwa nini ukitaka kununua laptop mpya unatakiwa uangalie processor? Nini cha muhimu kuhusu hii processor?

-Kwa lugha rahisi processor ni kifaa ndani ya computer yako kinachobeba maagizo ya program za computer. Maagizo hayo yanaweza kuwa ya kimahesabu, kimantiki, maagizo yanayoingia kwenye computer na yanayotoka.

-jinsi processor inavyokuwa na speed kubwa ndio jinsi maagizo yatakavyofanywa haraka na ndio jinsi program za computer zitakavyofanya kazi upesi.
processor_01.jpg

Familia ya processor za intel

Intel wana processor za aina nyingi na ni ngumu kuzitaja kwa pamoja, ila wameturahisishia kwa kuzipanga processor zao kwenye familia. Na hii ndio familia yao.

1. Atom processor- processor hizi hutumika kwenye vimini laptop na tablet ni ndogo kiumbo ndio maana hata vifaa vyake ni vidogo, processor hizi hazina nguvu sana na vifaa vyake hukaa sana na chaji.

2. Celeron processor- Haina tofauti sana na atom ila hii ina afadhali kidogo. Inatumika kwenye vifaa vikubwa kuliko atom kama vile laptop kubwa na desktop

3. Pentium- hii ina speed kuliko celeron na atom pia inatumika kwenye vifaa vikubwa.

4. Core 2 duo- hii ni maarufu kwa perfomance yake ya multitasking, inauwezo wakufanya mambo mengi kwa wakati mmoja ila nyingi ni za kizamani.

5. Core i3- hii ni processor latest za intel ni dual core lakini core zake zina perfomance kubwa na pia inakuwa na thread 2 kwenye kila core, ni nzuri kwa wanaotaka perfomance kubwa kwa bei rahisi.

6. Core i5- ya laptop ni dualcore na ya desktop ni quadcore isiyokuwa na thread, software nyingi kubwa duniani zimekuwa optimized kutumia core kama za i5, ni nzuri sana kwa watu wanaotumia software zinazodemand perfomance lakini hawafanyi multitasking.

7.Core i7- hii inakuwa na quadcore processor na thread 8 kwenye desktop na pia inaweza kuwa dualcore kwenye laptop. Hii ndio processor nzuri zaidi kwa watu wa kawaida na inafanya multitasking hata kama software zinademand sana.

8. Xeon- hii ndio processor yenye speed zaidi kwenye processor za intel lakini imekuwa designed kufanya kazi kwenye computer kubwa kama vile server. Unapohost website processor kama hii ndio inayoprocess webpages.

Generation ya processor(muhimu)

Ni muhimu sana kujua processor inatokea generation ipi kuna processor zenye i7 ya 2010 ambazo zipo slow vibaya mno, na pia kuna uwezekano i3 kuipita i7 kwenye perfomance kama zinatoka generation tofauti. Hivyo eneo hili inabidi uwe makini kuepuka kuuziwa mbuzi kwenye gunia. Hivyo unaponunua laptop/desktop ni lazima ujue ipo generation gani la sivyo upo hatarini na hivi ndio namna ya kujua.

- Processor yenye namba inayoanziwa na elfu nne ni fourth generation(4xxx)
Mfano Intel i3-4130.

- Processor yenye namba inayoanziwa na elfu tatu ni third generation (3xxx)
Mfano i3-3130.

- Processor inayoanziwa na elfu mbili ni second generation(2xxx)
Mfano i3-2140

Sishauri kabisa kununua processor ya first generation, mtu unatakiwa atleast ununue ya second generation na pia bei inatakiwa iwe ndogo kwa hii second compare na third/fourth.

Processor ndogo kama atom na celeron zina generation zake ambazo ni
-clover trail
-bay trail

Processor za zamani za atom zilikuwa mbaya sana na zipo slow ila baytrail ikaja kuzipa nguvu na kuzifanya ziwe na perfomance kubwa, hivyo kama unataka kifaa cha atom/celeron make sure processor yake iwe inatoka generation ya baytrail.

Herufi za mbele ya processor(muhimu)

Kama umechunguza mbele ya processor kunakuwa na herufi mbali mbali hizi pia ni muhimu sana kuzijua kwani usipozizingatia unaweza kujuta.

Mfano processor inaweza kuitwa i5-4000m au i5-4000u au i5-4000y je nini kinatofautisha hizi processor?

1. Herufi kwenye processor za desktop.

Bila herufi – hii inakuwa na speed halisi ya processor mfano i7-4770

K- herufi hii inamaanisha processor ipo unlocked na unaweza kui over clock na kuongeza speeed. Processor yenye 3.5ghz unaweza kui overclock ikafika 4ghz. Jina lake linakuwa mfumo huu i7-4770K. ni nzuri sana kwa wanaocheza magame na kufanya rendering.

R- herufi hii inamaanisha processor hii ni ndogo sana na inaweza kutumika kwenye videsktop vyenye umbo dogo hali ya kuwa ina graphic kubwa kama iris pro. Jina lake linakuwa mfumo huu i7-4770R hii ni nzuri kwa wale wenye ofisi ambazo ni safi hawataki mawaya mengi na desktop kubwa kukaa kwenye meza. angalia picha hapo chini uone desktop ndogo.

brix1_s.gif

S- herufi hii inamaanisha hiyo proceesor wame optimize perfomance mara nyingi wanai underclock kuzuia processor kupata joto sana. Mfano i7-4770 ina 3.4ghz lakini i7-4770S ina 3.1ghz tu, ina maana hapa wamepunguza 300mhz kutoka stock kuja S.

T- herufi hii inamaanisha processor inatumia power ndogo, kwa wale wenzangu wanaotumia luku kama unataka desktop isiokula umeme basi hii ndio yenyewe ila perfomance nayo itapungua kidogo. Mfano wa jina ni i7-4770T

2. Herufi mbele ya processor za laptop(mobile)

Tumeshaona herufi mbele ya desktop, sasa hivi tuangalie herufi mbele ya processor za laptop ambazo pia zinaweza kutumika kwenye home theatre pc (htpc) au wengine wanaita mini desktop.

M- herufi hii inamaanisha hio processor ni mobile, ndio herufi common kwenye processor za laptop mfano i5-4000M

U- herufi hii inamaanisha processor ya laptop inatumia power ndogo hizi processor zinatumika sana kwenye vilaptop vyembamba (ultrabook). Kwa sababu zinakaa na chaji kutokana na kutumia power ndogo, perfomance yake nayo pia ni ndogo. Mfano i5 4250U

Y- hii ni ultra low power yaani inakula umeme mdogo kushinda hata U lakini vile vile perfomance inazidi kushuka nayo mfano i7-4610Y

HQ- herufi hii inamaanisha high perfomance, zinauzwa bei ghali sana na power yake inashindana na desktop. Usije ukajaribu kuieka kwenye mapaja laptop ya design hii maana zinashika moto upesi sana kutokana na quality ya processor. Ni nzuri kwa wale wanaopenda kucheza game, kutumia software kubwa wakiwa kitandani. Mfano ni i7-4700HQ

MQ- herufi hii inamaanisha hio procesor ni quad core. Kama umesoma vizuri juu i5 na i7 za desktop ni quadcore lakini za laptop ni dualcore, hivi processor hii inamaanisha unaweza tumia quadcore kwenye laptop yako kama unataka mfano i7-4900MQ

MX- herufi hii inamaanisha ni xtreme edition, processor hii unaweza kui over clock kama vile K series ya desktop na ina perfomance kubwa sanaaa, ila kuwa makini na mapaja tu.
Mfano i7-4940MX

Huu ndio muongozo wa kununua processor za intel, kama kuna sehemu hujapaelewa unaweza kuuliza nitaelezea zaidi.
Ahsante sana hivi bado upo humu Chief.maana uzi naona wa 2014 upo?
 
Mimi mkuu bado natumiaga director x 11_ mpk leo cjawahi kujaribu kutuma director x 12_ ila vulkan inanishida jinsi ya kuitumia alafu ajabu hata kua stail direct x 11_ swez niweke 12_inanishida hebu nipe msaada kidgo hapa mkuu
Option unazikuta ndani ya Game husika. Na drivers zipo installed automatic unless wakwambie otherwise.

Na si kila game lina vulkan ama direct x12

Fungua game lako nenda setting za video ama graphics Utakuta setting za Api

Settings.png

Game gani Unataka kubadili.
 
View attachment 1890573

Game gani Unataka kubadili.
Sawa mkuu ivi ile monitor ya nuc haina 4k sio
Maaan nataka niichukue sehem kuna tv nnch 32 nataka nimpe aniachie ile so naogopa nisije kuchoma
 
Sawa mkuu ivi ile monitor ya nuc haina 4k sio
Maaan nataka niichukue sehem kuna tv nnch 32 nataka nimpe aniachie ile so naogopa nisije kuchoma
Ile NEC ni Full HD. 4k Mara nyingi bei ndefu sana.
 
Tv inaniumiza sana macho ndio maana nataka nibadiri now mkuu
Mimi pia Napenda monitor kubwa ila quality wise kibongo bongo Ukitaka Monitor nzuri kwa bei nafuu ni za inch 24.

Utapata resolution nzuri, zenye ips na bezel less display, kwa around laki 2.

Kama huangalii muonekano na tech za kisasa mpaka 100k-150k Unapata.
 
Hivi mkuu muziki ya nyumbani kama vile home theater music system ubora wake huwa unapimwa kwa kuangalia vitu gani?
 
Hivi mkuu muziki ya nyumbani kama vile home theater music system ubora wake huwa unapimwa kwa kuangalia vitu gani?
Mimi si mtaalam wa muziki mkuu ila ninachofahamu ki layman unaangalia

1. Sorrounding sound, hapa kunakuwa na idadi maalum ya spika kutengeneza effect mbalimbali, mfano kuna 5.1 chanell, 7.1 etc. Speaker hizi zinawekwa pembe mbalimbali za sebule ama chumba kama vile kulia mbele, kushoto mbele, katikati, kulia nyuma, kushoto nyuma etc, hii inakupa uhalisia fulani, mfano kama unaangalia movie na mtu ana tokea kulia amevaa viatu vinakanyaga sakafu utasikia kabisa sauti inatoka kulia kwenda kushoto.

Ukienda sehemu kama cinema sound system inakuwa complicated zaidi spika zaidi ya 20 wanaeka hadi za juu na chini kwenye sakafu.

2.kuna vitu vinaongeza ladha ya music tech kama Dolby Atmos zikiwepo ni muhimu.

3.then mambo mengine ya quality za speaker kama bass, loudness na mengineyo.

Sema ninavyoona mimi wengi wanatengeneza huko Ughaibuni, mtu ananunua Amplifier na subwoofer lile tu spika la kati na zile za pembeni wananunua separate.
 
Shukrani mkuu
 
Back
Top Bottom